Benatia
Senior Member
- Nov 14, 2019
- 122
- 274
Habari za wakati huu wakuu, natumaini sote humu ni wazima wa afya, na kama kuna ambao labda hali zao kiafya sio njema Mungu awasaidie ili muweze kupata unafuu.
Nimeamua niandike huu uzi nikiwa na huzuni kubwa sana moyoni kwa hili janga lililo nitokea.
Mwaka 2013 mwezi wa 8 nikiwa nasoma kidato cha pili niliugua Malaria kali sana iliyopeleka mpaka kufika hatua ya kutishia maisha yangu, naweza kusema zilikuwa zimebaki dakika kadhaa tu huenda nisingekuwepo tena hapa duniani.
Lakini Mungu ni mwema sana hatimaye niliweza kupona kabisa.
Sasa wakati naelekea kupona ghafla masikio yangu yalianza kupoteza usikivu. Yaani ilikuwa kama masihara tu masikio yangu yaliziba kabisa kiasi ambacho sikuweza kusikia mpaka muda huu ninapoandika hapa. Pia ikumbukwe kwamba nilizaliwa masikio yakiwa mazima kabisa bila tatizo lolote.
Halafu kuna jambo lingine ambalo huwa linanichanganya ni kwamba tangu nipoteze usikivu ndani ya masikio yangu kuna miungurumo fulani hivi ya ajabu ambayo huwa siielewi kabisa.
Kwa kweli naumia sana kila nikitafakari hatma ya maisha yangu ya baadae na ukizingatia mimi bado ni kijana mdogo tu mwenye miaka 22, ndoto zangu zote zimezima kabisa.
Msaada jamani kama kuna mtu yeyote mwenye utaalamu kuhusu masikio anisaidie please!
Asanteni!🙏