Sijui ni Marekani gani hiyo uliokuwa wewe,labda kwa vile mimi huishia mijini, ila nchi nyingi za wazungu,wako very economical kwenye kutumia maji,hata kwenye ile shughuli sisi tunatumia maji kujiswafi,wenzetu wanaogopa kushika hivyo wanatumia karatasi,tissue paper na wipes
Je, Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo Kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?
P
Kuna mdada mmoja tulisona nae Zanaki miaka hiyoo, tukapotezana tukajakutana yeye kaolewa Zanzibar halafu mie nilienda kule kwa kazi moja ya mradi.
Anaitwa Sophia, mwenyewe anajitupiaga ushungi wa nakshi aka wa kutupia sio ule wa kukaza.
Katika maongezi yetu ya hapa na pale ya wanawake akaniambia, shosti....
1. anza kunywa maji ya bamia utanishukuru miaka mia mbeleni..
2. Ukienda haja kubwa au ndogo tumia maji kwanza halafu ndo ufate hizo tishu zenu. Nakwambia maji ni dawa na kule kwa bibi hakutaki mambo mengi, maji tuu shwaaa, muda wowote ukipigwa kata funua uko safi...😅 sio hadi useme nakimbilia chooni kwanza akuuu.
3. Anayekupunguzia uzito mnyoane ukimaliza unamsinga na mafuta malainii yenye marashii, walahi usipofikishwa Kasinde njoo unikoe makwenzi....
Nilichekaaa ila niliyafanyia kazi maneno yake. Sikubahatika kuonana nae tena Bi Sophia natumai yu mzima ila, maneno yake hayakwenda bure. Nami niliyaendeleza kwa wamama wengine shurti shurtu.
Turudi kwenye mada, maji ni uhai.
Content ya maji ni hydrogen na oxygen.
Ila ili yawe maji safi yanaongezewa kemikali kadhaa mojawapo ni chlorine/chloride suna hakika na fluoride.
Wakemia waje watuelimishe maji salama yana content gani zaidi ya H2O.
Nilisikia mahali maji ya huko mambele yana madini ya copper na chuma ambazo kwa miaka mingi inawaletea magonjwa ya kansa....
Ni kusikia huku na kule sina ushahidi.
Kasinde.