Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,156
- 31,047
Mkuu mimi nina tatizo hili una solution yake. Yani nikijisugua kwa dodoki nikimaliza nawashwa kweli.Unatumia dodoki?
Je BAdo muwasho unakuepo bila ya dodoki?
Mkuu mimi nina tatizo hili una solution yake. Yani nikijisugua kwa dodoki nikimaliza nawashwa kweli.Unatumia dodoki?
Je BAdo muwasho unakuepo bila ya dodoki?
Naoga ya baridi, ila hata hayo moto hali mbona inakuwepo tu hivyo hivyoHiyo hali ilkuja kuisha yenyewe sikumbuki iliishaje,by the way unaogaga maji baridi ama warm?
Mkuu yaani nimebadili sabuni mpaka nimechoka, lakini hali iko hivyo hivyo
Duuh, Ahsante kwa ushauri mkuu.Pole sana ndugu, JARIBU KWENDA KUPIMA LIVER TEST FUNCTION, inaweezekana hepatits A, B, C. n.k, pamoja na figo
Ninayo hiyo hali huu mwaka wa 20 sasa, imebidi nizoee tuOkay, wakuu kicha cha uzi hapo juu kinahusika.
Iko hivi, nina changamoto ya kuwasha wote kila baada kwenda kukoga.
Sasa hali hii imekua ikinisumbua kwa muda sasa, hivyo naombeni ushauri wenu kama kuna mtu ambae ameshawahi kupitia changamoto kama hii ninayopitia mimi.
Ili niweze kuiepuka maana imekuwa kero sasa.
Uzi tayari
Sawa mkuu nitajaribu hiyo ya kutojikausha mwiliSabuni unayotumia inaweza kusababisha kuwashwa Mwili, jaribu kubadilisha sabauni ya kuogea.
Vyanzo vya Maji vinaweza kusababisha kuwashwa kwa Mwili punde unapomaliza kuoga.
Kama ni mtumiaji wa Maji ya moto mara kwa mara, nayo inaweza kuwa ni moja ya sababu ya wewe kuwashwa Mwili.
Taulo unalotumia inaweza ikawa ni moja ya sababu ya wewe kuwashwa Mwili unapomaliza kuoga. Anzisha utaratibu mpya wa kufua Taulo kila unapomaliza kuoga, kama kuna uwezekano jitahidi uwe na mataulo japo mawili nikiwa na maana, taulo utakalotumia kujifutia liwe limekauka, usijifute na Taulo bichi au lenye unyevunyevu.
Kuanzia hivi sasa ninapotoa haya maelezo anza kufanya hivi, usijikaushe unapomaliza kuoga, acha Maji yakukaukie Mwilini, ikiwezekana wewe jikaushe kichwani ikiwemo na uso, pamoja na sehemu za siri tu, sehemu nyingine ya Mwili iache Maji yakaukie Mwilini.
Ukiwa unasubiri mbadala, anza na zoezi hili la kutojikausha Mwili utakuja kunipa marejesho, tatizo limekwisha
Duu, nilijua hapa duniani ni mimi tu ninaeteseka na hii issue , , maana nikioga huwa natenga kabisa nusu saa ya kujikuna, hatari sana
Okay mkuu, shukraniKuna uzi nime post link yake wadau wa JF walisha wai kujadili Hili swala kwa kina hakika JF ni kisima Cha maarifa..
Tatizo la kuwashwa mwilini baada ya kuoga: Fahamu chanzo, ushauri na tiba | JamiiForums Tatizo la kuwashwa mwilini baada ya kuoga: Fahamu chanzo, ushauri na tiba
Mkuu hizi sabuni watu wengi tunazoogea zinawasha mwili, kila mmoja anajua inapoingia machoni. Kuna body wash fluids ambazo hazina sabuni (soap free body wash fluids) ambazo unaweza kuogea...pia kama ngozi yako inakauka sana baada ya kuoga maji ya moto kwa muda mrefu, punguza muda wa kuoga maji ya moto au yasiwe ya moto sana, mfano zisizidi dk 5.....oga kwa muda mfupi sepa badala ya kunogewa na kuoga karibu robo saa hadi nusu saa hali itakayopelekea ngozi kupoteza maji mengi (moisture) na kuwa kavu. Kama ngozi inakuwa kavu unaweza kutumia pia lotion ambazo zinaongeza unyevunyevu wa ngozi (moisturizing lotion/cream).Mkuu yaani nimebadili sabuni mpaka nimechoka, lakini hali iko hivyo hivyo
Fanyia kazi utakuja kuniambia, haya maudhi yalishawahi kunikuta nafahamu kero zake vizuri sana.Sawa mkuu nitajaribu hiyo ya kutojikausha mwili
Mi ilikuwa zaidi nikioga maji ya moto ndo nawashwa, sijui iliishaje hiyo hali maana Siku hizi siwashwi tens,Naoga ya baridi, ila hata hayo moto hali mbona inakuwepo tu hivyo hivyo
Hii nimeshamsikia mtu pia yeye akinyeshewa na mvua anawashwa mwili mzimaMimi shida iko nikioga maji ya mvua nawashwa sana...
Sema wabongo tuna ka uchawi flani cha asili,,,yaaani mtu anakazania kabisa eti anashukuru Mungu hayuko mwenyewe,jins unavyoteseka ukiona na mwenzio anateseka ndio unafurah.?Daaah aisee nlijuaga npo pekeyng nakumbuka hii Hali ya kuwashwa nlianza kuipata miaka fulan kpnd npo advance school nilikuwa nikioga tu asee nawashwa bac nikitoka bafun nakimbilia kitandan najikuna mwili mzima Sasa nkichungulia nje ya kitanda nkiona uchafu tu bac mwili unazidi kuwasha yaan mpk ikafka kpnd naona bora nkae wiki nzima pasipo kuoga lakn tatz wap bado lipo sema co kila siku now nkarud nyumban Hali bado yaan inafka hatua nkitaka kuoga bac nahakikisha chumba kisaf nguo kila kitu kiwe sawa then nkimaliza kuoga najifunika shuka gubigubi najikuna nmebadilisha san taulo nlijua ndo sababu ila wap hamna ktu sahv nmeamua tu nkimaliza kuoga najifuta kuanzia kiunon kushuka chini bac cku nyngne najikausha na shati tu. Daah hii Hali inatesa sana sema nmeshkuru kumbe cpo mwnyw