Tatizo la kuwashwa mwilini baada ya kuoga: Fahamu chanzo, ushauri na tiba

Shinto

Shinto

JF-Expert Member
1,781
0
BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA KUHUSU TATIZO HILI
Wakuu, nina tatizo la mwili kuwasha baada ya kumaliza kuoga tu. Hili tatizo lilijitokeza kama miaka mitatu iliyopita likatoweka lenyewe, sasa naona limerudi tena.
  1. Je, nini chanzo cha hii hali, ni maji ninayoogea?
  2. Ni sabauni ninazo tumia? Sina sabuni specific
  3. Ni maradhi ya ndani ya mwili
  4. Nini tiba yake?
---
Habar ndugu zang. Ninaomba ushauri kwa wenye kujua suluhisho la kuwashwa mwili baada ya kuoga. Najarbu kutumia sabun za aina mbalimbal lakini tatzo bado liko vilevile.

Please wana JF naitaji msaada wenu kwa wenye kujua.
---
Duh!! Hadi nilikuwa naona aibu kusema!! Yaani hili tatizo limenitesa kwa miaka mingi,nimejaribu dawa kadhaa za hospitali bila mafanikio,ila niligundua njia moja ambayo kidogo inanisaidia,nikioga asubuhi tatizo linakuwa kubwa zaidi,ila nikioga jioni/usiku huwa napata nafuu kidogo,

Hasa nikioga na kuwahi kujifuta na kuingia kitandani ASAP na kujifunika gubigubi,huwa pia nikiwa katika hali hiyo ya kuwashwa napata kichefuchefu sana, sitki nione kitu chochote kichafu wala sitaki niguswe na kitu nilicho na mashaka nacho,hali hiyo huwa inadumu kwa dakika kumi hadi thelathini!! Ni shida wakuu.
---
Habarini za saa hizi wapendwa katika Mungu aliye hai,

Husika na kichwa hapo juu. Nimekuwa na tatizo hili la kuwashwa mwili mzima hadi mistari ya uvimbe kama nimetambaliwa na mdudu hujitokeza kwa miaka minne sasa, naumia mnoo!

Kwa matitabu niliyowahi kufanya ni ya St. Joseph hospital MOSHI mwaka 2015 hii haikuzaa matunda, niligongwa sindano nyingi lakini haikisaidia.

Matibabu mengine ni mitishamba flani hivi nilinunua sokoni mgandini(TANGA) mwaka Jana haikusaidia nayo, yani ndo tatizo linazidi nawashwa mpaka najisikia vibaya kufika mahali hadi nauchukia mwili wangu so saaad!!!.

Naombeni sana tena sana msaada wa nini nifanye kuondokana na shurba hii jamani.


Thanks in advance.
---
Nini kinasababisha kuwashwa mwili baada ya kutoka kuoga? Tatizo limenisumbua miaka 10 sasa.. Nikijisugua ndo nawashwa kabisa, nisipojisugua nawashwa kidogo afadhali lkn mtu huwezi kuoga bila kujisugua.

Najisugulia kitambaa laini kabisa, nikitoka kuoga nachanganyikiwa kwa kuwashwa mno na daktari aliniambia ninywe piriton kila kabla sijatoka kuoga na nikitoka kuoga lkn haikunisaidia kabisa.

Naombeni ushauri nifanye nn manake nimekata tamaa sina raha ya kushika maji hata kidogo. Mvua ikininyeshea nawashwa haswaa. Mwili unatutumka unavimba kila nikijikuna.
===
UFAFANUZI WA JUMLA JUU YA TATIZO HILI

“Wataalamu wa afya ya ngozi pia wanabainisha kuwa kuoga muda mrefu na mara kwa mara, matumizi ya sabuni zenye harufu kali na povu jingi ni mambo mengine yanayochangia kutokea kwa mzio pamoja na ukavu wa ngozi kutokana na uwezo wake wa kuondosha kiasi kikubwa cha mafuta yanayolinda ngozi.

Ili kupunguza hali ya muwasho, “Tumia sabuni zenye mafuta, lakini zisiwe na marashi makali.”

Katika hali ya kawaida kitendo cha kuoga kinapaswa kuchukuliwa kama jambo la kufurahisha kutokana na ukweli kwamba huufanya mwili uburudike na kuwa safi. Lakini kwa baadhi ya watu mambo ni tofauti. Kuoga huwa sawa na karaha.

Moja ya matatizo ya kiafya ambayo yanayosumbua watu wengi duniani na kuwanyima raha ya maisha, ni tatizo la mwili kuwasha mara baada ya kuoga. Muwasho baada ya kuoga unaweza kujitokeza mwili mzima au unaweza kuhusisha baadhi ya sehemu.

Hali hii inaweza kuwa inajitokeza kwa muda wa dakika chache au inaweza kuchukua muda mrefu na kwa baadhi ya watu, hili linaweza kuwa tatizo sugu. Ingawa tatizo hili la kiafya ni kama mengine, lakini baadhi ya watu kwa kukosa taarifa sahihi, hulihusisha na imani potofu.

Ukweli wa mambo ni kwamba kuna sababu nyingi zinazochochea kutokea kwa tatizo hili na baadhi hazina madhara makubwa kama vile kuhatarisha kwa maisha.

Pamoja na ukweli wa kisayansi kwamba asilimia 70 ya mwili wa binadamu ni maji, kwa upande mwingine yanaweza kuwa chanzo cha matatizo ya kiafya hasa pale yanapokuwa na vitu vinavyosisimua mwili au kuchochea hali ya kutokea kwa mzio. Siyo jambo la kushangaza kuona kuwa maji ambayo ni safi na salama kwa kunywa yanaweza kuwa siyo salama kwa kuoga.

SABABU ZA MUWASHO MWILINI
Miongoni mwa sababu za kutokea kwa muwasho wa mwili baada ya kuoga ni za kimazingira na sababu zingine zinahusiana na hitilafu za urithi wa vinasaba vya kijenetiki katika mfumo wa kinga ya mwili wa mhusika.

Wakati mwingine tatizo hili linaweza kuwa ni dalili muhimu inayoonyesha baadhi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kama vile matatizo ya figo, ini, tezi shingo, matatizo ya mfumo wa damu, kisukari, saratani ya mitoki na msongo wa mawazo.

Baadhi ya tafiti zinabainisha kuwa sababu nyingine ni pamoja na uchafuzi wa mazingira ya hewa kwa kemikali zenye sumu zinazopatikana katika moshi wa tumbaku, mifuko ya plastiki, dawa za kufanyia usafi majumbani, dawa za kuua wadudu, vumbi ya ndani ya nyumba yanayobeba vimelea vya magonjwa pamoja na uchafuzi wa hewa kwa moshi wa magari na ule unaozalishwa na viwanda katika maeneo ya mijini.

Vitu hivi huufanya mwili kuathirika na kutengeneza mazingira ya ndani ambayo yanachochea kutokea kwa muwasho pindi mwili unapopata msisimuko, hali ambayo hujulikana kama mzio.

Mzio huanza pale mfumo wa kingamwili unapobainisha kemikali hizi kama mvamizi wa mwili na kuamuru askari wake wajulikanao kama seli za T-lymphocites na B-lymphocytes kujibu mapigo ya wavamizi kwa kuzalisha kemikali maalumu zijulikanazo kama immunoglobulin E na prostaglandins ambazo husababisha kuzalishwa kwa kemikali nyingine kama vile histamine, tryptase na chymase, kwa lengo la kuvunja nguvu za kemikali vamizi.

NI KWA NAMNA GANI?
Baadhi ya watafiti wanabainisha kuwa kutokana na hitilafu za vinasaba vya kijenetiki kunakuwa na ongezeko la kemikali aina ya Cyclic Adenosine Monophosphate Phosphodiesterase ambayo inaharibu mfumo wa udhibiti wa seli za kinga mwili aina ya basophils na seli za mast na kusababisha zisisimuke kupita kiasi na kuzalisha histamine nyingi ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa mzio.

Watu wengi wana mzio wa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na dawa za tiba, kemikali zinazotumika kutengenezea sabuni, vipodozi, aina fulani za vyakula, kemikali kadhaa zinazotumika katika usindikaji wa vyakula, kemikali zinazowekwa katika maji kama vile chlorine (watergurd), maji ya kuoga yenye chumvi nyingi na kemikali zinazotumika katika utengenezaji wa nguo, ikiwa ni pamoja na mataulo ya kuogea.

Mapambano kati ya kinga mwili na kile ambacho mwili hukibainisha kwa makosa kama wavamizi, yanaweza kusababisha magonjwa ya pumu, muwasho wa ngozi, muwasho wa macho, mafua ya mara kwa mara na maumivu ya tumbo.

SABABU NYINGINE
Mapambano haya pia yanaweza kusababisha hali ya mzio dhidi ya vyakula kama vile mayai, maziwa, samaki, nyama, karanga, vyakula vitokanavyo na unga wa ngano, kahawa, pombe na baadhi ya vyakula na vinywaji vinavyotengenezwa au kusindikwa viwandani kwa kutumia kemikali. Hali hii pia inaweza kutokea kutokana na kula vyakula vyenye mchanganyiko wa vikolezo kama pilau na viungo vingi.

Ulaji wa vyakula vyenye upungufu wa viinilishe nao unatajwa kuwa unachangia kutokea kwa tatizo la mwili kuwasha wakati wa kuoga.
Watu wengi hawatumii kiasi cha kutosha cha matunda, mboga na mafuta salama yanayotokana na mimea au samaki, jambo ambalo huathiri vibaya afya ya ngozi.

Tatizo jingine linalochangia mwili kuwasha wakati wa kuoga ni kutokutumia kiasi cha kutosha cha maji ya kunywa kila siku. Hali hiyo inafanya mwili kuwa na upungufu wa maji na kuathiri vibaya afya ya ngozi na uwezo wake wa kuondosha sumu mwilini.

Ngozi isiyokuwa na afya njema inashindwa kutunza kiasi cha kutosha cha unyevu na kusababisha ukavu. Ngozi inapokuwa kavu husisimka kupita kiasi wakati wa kuoga na kusababisha muwasho. Sababu ya mwili kuwasha baada ya kuoga ni kuishi katika hali ya msongo wa mawazo inayosababishwa na hofu, wasiwasi na sonona.

Tatizo jingine linalosisimua mwili na kusababisha muwasho wakati wa kuoga ni kujisugua kupita kiasi au kujisugua wakati wa kujifuta kwa taulo baada ya kuoga. Kwa kawaida seli za ngozi zilizokufa, jasho na vumbi ndivyo vinasababisha mwili kuchafuka.

Lakini uchafu huo huondoka mwilini tunapooga na nguvu nyingi hazihitajiki ili kuondosha uchafu na taka mwili juu ya ngozi. Matumizi ya nguvu nyingi na kusugua ngozi sana, husababisha madhara kwenye ngozi na kusababisha muwasho au ukavu wa ngozi kwa kuondosha mafuta yanayolinda usalama wa ngozi.

Watu wenye tatizo hili wanaweza kufanya mazoezi mepesi kabla ya kuoga ili kupasha mwili joto au kupaka lotion ili kuifanya ngozi kuwa na unyevu na kupunguza hali ya ukavu wa ngozi

===
USHAURI NA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI

Muwasho baada ya kuoga yaweza kuwa ina sababishwa na maji unayotumia kuogea yana aina ya chumvi chumvi ambayo haipatani na ngozi yako. Hii ni kama unaogea maji ya kisima. Au inasababishwa na aina ya sabuni unayo ogea.

Ngozi yako iko sensitive kwa hiyo ina react na ngozi yako na baada ya muda inpozwa na mafuta ya mwili. Pia inweza kuwa unatumia taulo damp ambayo haikauki vizuri toka uitumie mara ya mwisho.

Vyote hivi vinahitaji uchunguze mwenyewe na take actions acordingly.
---
sometimes pia ngozi ikipata rapid temperature change huwasha, mfano ulikua kwenye sehemu yenye AC na ghafla ukatoka nje kwenye jua kali ngozi huwasha sana, au ukitoka kwenye joto kali sana na ukaenda kuoga na maji baridi pia ngozi huwasha, despite tatizo la allergies pia hii nayo ni sababu, ngozi kuwa exposed to rapid temperature changes zile pores zinazohusika na kupitisha hewa zina 'shrink' kwa haraka na kusababisha hali ya muwasho wa ghafla.
---
Mimi pia nina hili tatizo na limekuwa ni tatizo la muda mrefu sana, na hasa nikioga maji ya baridi nimeenda hospital tofauti tofauti lakini tatizo liko pale jibu nililopata kwa hospital ni allergy. Kuhusu maji sijui kama ni kweli kwa sababu mimi naishi kanda ya ziwa so naoga maji ya ziwa hayana chumvi, kwenye maeneo ya maji chumvi nimefika lakini ni yale yale tu.

Mimi ninachofanya na kidogo tatizo limepungua kwa sehemu ni kwamba naoga maji ya moto, sijifutii taulo natumia khanga kujikausha na nikimaliza kuoga najikausha fasta, sikai na maji zaidi hata ya dk moja na kujikausha kwenyewe ni kama unajisponji sio kujifuta, nikishajikausha napaka mafuta kidogo sehemu ninazaowashwa, so inanisaidia kidogo angalau muwasho unakuwa si mkali sana, halafu mimi siwashwi mwili mzima nawashwa kwenye mikono na kwenye mapaja basi.
---
Ukimaliza kuoga hakikisha unajikausha mara unapomaliza na hakikisha taulo kavu, usijikaushe na taulo bichi bichi, bacteria huwa wanapenda kukaa kwenye ubichi ubichi. Anika taulo lako juani au sehemu ambayo haiweki unyevu.. Kingine hakikisha umekauka vizuri ndio uvae nguo, na nguo hiyo iwe kavu... Usipake mafuta ya mgando kama una tatizo la kuwashwa, tumia mafuta ya maji maji ama lotion..
Hope nimekusaidia..
---
Mkuu hiyo itakuwa ni Water allergy au Aquagenic urticaria. Ni allergy dhidi ya maji ya moto au baridi au yenye chlorine au yasiyowekwa chlorine. Ni kitu kinachotokea watu wachache sana. Tiba yake inaweza ikawa ni supportive zaidi, kama:

1. Ikiwa chanzo chake ni maji ya moto basi oga ya baridi, kama ya baridi tumia maji ya moto na kama shida ni chlorine inayowekwa kwenye maji basi huwa kuna shower gel ya kuondoa chlorine mwisho wa kuoga au utafute purifier ambayo itatoa chlorine. Hapo kwenye chlorine ni issue kubwa.

2. Ikiwa unapata allegy ukigusa tu maji, basi waweza tumia oily cream au gel kupaka mwilini kabla ya kuoga au kuogelea. Hupunguza muwasho kiasi kikubwa.

3. Epuka kukaa muda mrefu ndani ya maji.

4. Nguo za pamba na linen husaidia kupunguza dalili. Tumia taulo lenye pamba asilimia 100.

5. Epuka kutumia vyakula vyenye viungo vingi na vyakula vinavyokaangwa. Pia epuka kunywa pombe na kahawa, maana vitu hivyo vitaongeza tatizo.

6. Muone daktari wa magonjwa ya ngozi.
---
Nafikiri naweza kuwasaidia katika hili wale wote wenye tatizo la kuwashwa watumiapo maji ya baridi au ya chumvi: Tatizo hili mara nyingi linasababishwa na mambo makuu mawili

1) kuwa na minyoo
2) kuchafuka damu, yaani damu kuchafuka na wengine wanaota majipu kabisa.

SOLUTION: Hebu tumieni dawa moja ya kienyeji inaitwa Oloodwa(kwa kimasai) inachanganywa kwny chai ya rangi au kula hivyo hivyo japo inawasha sanaaa kwny koo.Tatizo likiwa chronic kuna nyingine wamama wa kimasai wanamix na hiyo kwa pamoja.

Hiyo ni dawa specifically kwa ajili ya kusafisha damu tu na pia kuupa mwili joto hata kama hali ya hewa nje ni ya baridi.

Nawatakia mpole salama.
---
Mimi ni medical student na pia ni muathirika was tatizo hilo. Nilianzwa na tatizo hilo nikiwa kidato cha kwanza mwaka 2005 na ilikua sababu kubwa ilionipelekea kupata hamu ya kusoma udaktari kwan nilihangaika vya kutosha.

Tatizo hilo linaitwa urticaria linaweza kua acute or chronic na linasababishwa na uzalishwaji wa chemically iitwayo histamine kwa wingi ambayo pia husababishwa na pressure, coldness, n.k Tiba sahihi ya matatizo haya ya allergy inapatikana kwenye clinic za magonjwa ya ngozi yan dermatology department ambako kuna madaktari bigwa yan specialists kwa ajili ya ngozi tu hawa ndio wanaweza kukupa tiba sahihi.

Kwa DSM tembelea hospital ya muhimbili jengo la wagonjwa was nje (new OPD). kanda ya kaskazini tembelea hospitali ya KCMC kitengo cha dermatology.
---
Pole sana!
Tuwe na busara kumshauri mtu anapohitaji msaada wa kimatibabu. Imani ina nafasi yake katika uponyaji na matibabu yana nafasi yake katika uponyaji.

Imani katika kuomba ni jambo jema lakini pia matibabu ni muhimu ndio maana Mungu aliwapa watu wengine uwezo wa kuwa Madaktari.

Allergies inaweza kuwa sababu kubwa kama ulishatibiwa bila mafanikio. Ingawa unaweza kucheck organs zako kidney, liver magonjwa mengi yanajificha huko. Ni ushauri tu mpendwa!

Allergy inaweza kutokana na mimea inayokuzunguka chakula mafuta ya kupikia au ya mwili, sabuni, dawa, perfumes au air freshners.
---
Mkuu hiyo itakuwa ni Water allergy au Aquagenic urticaria. Ni allergy dhidi ya maji ya moto au baridi au yenye chlorine au yasiyowekwa chlorine. Ni kitu kinachotokea watu wachache sana. Tiba yake inaweza ikawa ni supportive zaidi, kama:

1. Ikiwa chanzo chake ni maji ya moto basi oga ya baridi, kama ya baridi tumia maji ya moto na kama shida ni chlorine inayowekwa kwenye maji basi huwa kuna shower gel ya kuondoa chlorine mwisho wa kuoga au utafute purifier ambayo itatoa chlorine. Hapo kwenye chlorine ni issue kubwa.

2. Ikiwa unapata allegy ukigusa tu maji, basi waweza tumia oily cream au gel kupaka mwilini kabla ya kuoga au kuogelea. Hupunguza muwasho kiasi kikubwa.

3. Epuka kukaa muda mrefu ndani ya maji.

4. Nguo za pamba na linen husaidia kupunguza dalili. Tumia taulo lenye pamba asilimia 100.

5. Epuka kutumia vyakula vyenye viungo vingi na vyakula vinavyokaangwa. Pia epuka kunywa pombe na kahawa, maana vitu hivyo vitaongeza tatizo.

6. Muone daktari wa magonjwa ya ngozi.
===
PIA UNASHAURIWA KUSOMA MADA HII
- Tatizo la kuwashwa mwili mara kwa mara linasababishwa na nini? - JamiiForums
 
Maundumula

Maundumula

JF-Expert Member
7,045
1,225
Siku mbili hizi nimefanya ka research kadogo kuhusu miwasho, nadhani hiyo yako inaweza kuwa inasababishwa na ngozi kuwa dry so ukitoka kuoga jipake mafuta fasta na pia ukijifuta na taulo usijisugue fanya kama una ji sponge kwa kugusia gusia kwenye mwili.
 
Angel Msoffe

Angel Msoffe

JF-Expert Member
6,790
1,225
Bwana we hata mi hili tatizo ninalo na linanikera sana na linanitokea nikioga maji baridi yani nawashwa naskia kero vby sana, lakini nikikoga maji moto siwashwi, nilichoamua kufanya ni kuweka maji yangu detol ya maji na kuyaogea sasa tatizo limepungua.
 
doctorz

doctorz

JF-Expert Member
907
195
Muwasho baada ya kuoga yaweza kuwa ina sababishwa na maji unayotumia kuogea yana aina ya chumvi chumvi ambayo haipatani na ngozi yako. Hii ni kama unaogea maji ya kisima. Au inasababishwa na aina ya sabuni unayo ogea.

Ngozi yako iko sensitive kwa hiyo ina react na ngozi yako na baada ya muda inpozwa na mafuta ya mwili. Pia inweza kuwa unatumia taulo damp ambayo haikauki vizuri toka uitumie mara ya mwisho.

Vyote hivi vinahitaji uchunguze mwenyewe na take actions acordingly.
 
NusuMutu

NusuMutu

JF-Expert Member
421
0
Hebu fuatilia ushauri wa Doctorz natumaini utakusaidia.lakin pia kunawatu wanatumia vitu vigumu kujisugua mwilini kama unafanya hivyo hebu acha na tumia kitambaa/taulo ndogo laini
 
bucho

bucho

JF-Expert Member
4,911
2,000
Mimi nikioga na maji moto nawashwa kwa dk kama 15 alafu inaacha . Sijui hata nini ?
 
Shinto

Shinto

JF-Expert Member
1,781
0
Ahsanteni wakuu, nitajaribu ushauri wenu
 
Obe

Obe

JF-Expert Member
9,225
2,000
Doctorz, umesema vema sana, binafsi huwa nina tatizo hili na nitafuatilia ushauri wako
 
Iron Lady

Iron Lady

JF-Expert Member
4,071
1,250
Wakuu, nina tatizo la mwili kuwasha baada ya kumaliza kuoga tu. Hili tatizo lilijitokeza kama miaka mitatu iliyopita likatoweka lenyewe, sasa naona limerudi tena.
  1. Je nini chanzo cha hii hali, ni maji ninayoogea?
  2. Ni sabauni ninazo tumia? Sina sabuni specific
  3. Ni maradhi ya ndani ya mwili
  4. Nini tiba yake?
Maji hayo unayoyaoga yawezekana kabisa yakawa si masafi na kusababisha ngozi yako kureact.na maji yetu tuogayo si masafi kwa sababu water system zetu ni za zamani sana na kusababisha maji kuchafuka kabla ya kuwafikia watumiaji.
 
K

Kakalende

JF-Expert Member
3,256
1,225
doctorz,
Doctorz umesema kweli, hiyo kuwashwa ni reaction ya mwili kwa alergy; yaani kunakuwa na aina ya chumvi kwenye maji ambazo mwili wako haukuzoea. Hivyo kuwasha, hakuna dawa ila jaribu kuchemsha maji ya kuoga kila inapowezekana vinginevyo ya baridi yatakuwasha lakini ukiyatumia muda mrefu taratibu mwili unazoea na hali hiyo inaisha.
 
marejesho

marejesho

JF-Expert Member
6,647
2,000
Kumbe siko peke yangu? Mie nawashwa baada ya kuoga haswa mikono na miguu!!
 
Don Mangi

Don Mangi

JF-Expert Member
2,204
1,250
Sometimes pia ngozi ikipata rapid temperature change huwasha, mfano ulikua kwenye sehemu yenye AC na ghafla ukatoka nje kwenye jua kali ngozi huwasha sana, au ukitoka kwenye joto kali sana na ukaenda kuoga na maji baridi pia ngozi huwasha.

Despite tatizo la allergies pia hii nayo ni sababu, ngozi kuwa exposed to rapid temperature changes zile pores zinazohusika na kupitisha hewa zina 'shrink' kwa haraka na kusababisha hali ya muwasho wa ghafla.
 
M

MaMkubwa1

Member
17
20
Siku mbili hizi nimefanya ka research kadogo kuhusu miwasho, nadhani hiyo yako inaweza kuwa inasababishwa na ngozi kuwa dry so ukitoka kuoga jipake mafuta fasta na pia ukijifuta na taulo usijisugue fanya kama una ji sponge kwa kugusia gusia kwenye mwili.
Pia jaribu kutumia sabuni 'gentle' na zenye mafuta .... kama DOVE (huu ni mfano tu bila shaka kuna aina nyingine. Check with your pharmacist)
 
MATESLAA

MATESLAA

JF-Expert Member
1,247
0
Tatizo kama hili ninalo kaka yani wakati mwingine huwa nawashwa mpaka najikuna na kisoda ila nikijipaka mafuta vaselin inakwisha
 
DaMie

DaMie

JF-Expert Member
684
195
Nadhani ni sabuni, hasa hivi za manukato. Mimi baada ya kuanza kutumia sabuni jamaa hakuna tena.
 
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
9,476
2,000
Kumbe huwakumba wengi nilidhani Peke yangu!
 
ram

ram

JF-Expert Member
7,942
2,000
Mimi pia nina hili tatizo na limekuwa ni tatizo la muda mrefu sana, na hasa nikioga maji ya baridi nimeenda hospital tofauti tofauti lakini tatizo liko pale jibu nililopata kwa hospital ni allergy. Kuhusu maji sijui kama ni kweli kwa sababu mimi naishi kanda ya ziwa so naoga maji ya ziwa hayana chumvi, kwenye maeneo ya maji chumvi nimefika lakini ni yale yale tu.

Mimi ninachofanya na kidogo tatizo limepungua kwa sehemu ni kwamba naoga maji ya moto, sijifutii taulo natumia khanga kujikausha na nikimaliza kuoga najikausha fasta, sikai na maji zaidi hata ya dk moja na kujikausha kwenyewe ni kama unajisponji sio kujifuta, nikishajikausha napaka mafuta kidogo sehemu ninazaowashwa, so inanisaidia kidogo angalau muwasho unakuwa si mkali sana, halafu mimi siwashwi mwili mzima nawashwa kwenye mikono na kwenye mapaja basi.

Muwasho baada ya kuoga yaweza kuwa ina sababishwa na maji unayotumia kuogea yana aina ya chumvi chumvi ambayo haipatani na ngozi yako. Hii ni kama unaogea maji ya kisima. Au inasababishwa na aina ya sabuni unayo ogea. Ngozi yako iko sensitive kwa hiyo ina react na ngozi yako na baada ya muda inpozwa na mafuta ya mwili. Pia inweza kuwa unatumia taulo damp ambayo haikauki vizuri toka uitumie mara ya mwisho. Vyote hivi vinahitaji uchunguze mwenyewe na take actions acordingly.
 
ram

ram

JF-Expert Member
7,942
2,000
Hata sabuni sidhani kama ni sababu, mimi nina hili tatizo zaidi ya miaka 10. Hospital nilishauriwa kuacha kitu kimoja baadya ya kingine matokeo yake yalikuwa ziro, ilifikia hatua nachemsha maji ya kuoga yanachemka kama ya ugali then unaacha yanapoa unaenda kuoga lakini wapi.

Sabuni ndo usiseme nilianza na gwanji, ilula, kwanga hadi sabuni ya mbuni inayosemekana haina kemikali ilikuwa ni kazi bure, nowdays naogea sabuni ya dettol na ninafanya kama nilivyosema kwenye post yangu ya mwanzo ndo angalau tatizo limepungua, nawashwa lakini si sana. Mimi hata kama kuna baridi kama mikono iko wazi chamoto nitakiona, nitajikuna balaa


Nadhani ni sabuni, hasa hivi za manukato
Mm baada ya kuanza kutumia sabuni jamaa hakuna tena.
 
KILITIME

KILITIME

JF-Expert Member
265
195
Pole sana ni tatizolinalosababishwa na mambo mengi ambalo jibu la jumla ni tabia ya mwili mimi pia nlikua na tatizo hilo nkatumia sabuni fulani ya kichina kutoka kampuni inaitwa TIENS sabuni yenyewe inaitwa Spirulina body wash ilinisaidia sana pia nlikua natumia majani ya chai yao kiukweli imeniondolea tatizo hilo na mengine sasa najsikia fresh itumie na wewe!
 

Forum statistics


Threads
1,424,580

Messages
35,067,513

Members
538,026
Top Bottom