Tatizo la kuwashwa mwilini baada ya kuoga: Fahamu chanzo, ushauri na tiba

aisee nilijua nipo peke yangu kwa hili tatizo yani mwenzenu najikuna miguu na mapajani mpaka nakuwa mwekundu kila nikioga maji ya bomba na ya mvua

nikiwa dar na moshi siwashwi hata maji ya bahari siwashwi nimejaribu ya kisima siwashwi ila tofauti kuna baadhi ya kisima kingine yananiwasha mpaka sina raha ya kuoga natamani hata kulia ikifika muda wa kuoga

na hali hii inazidi asubuhi kukiwa na ubaridi ukijaribu kuoga mchana hauwashwi sana

huwa nameza prednisolone kidonge 1 nikitoka tu kuoga japo ukitoka kuoga ukinywa maji yanaongezea kuwashwa ukikanyaga mchanga ndo kabisa au ukijifutia nguo mbichi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm tatizo hilo limenikuta ssna ila nikaja kugundua kuwa ni aina ya maji ninayo yatumia.nikiogea maji ya mvua nawashwa sana mwili...ila nikiogea maji mengine tuu mwili unakuwa shwar sana..sometime naona ni aleji ya aina fulani ya maji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Doctor Aghakhan aliniambia inaitwa AQUAGENIC PRURITAS, ipi ni ipi??
Pole sana, hilo tatizo kitaalam linaitwa AQUAGENIC URTICARIA, ni kwamba mwili wako unakuwa na allergy ya maji, nijuavyo mimi tatizo hili halina tiba ila unaweza kulipunguza sana kwa kuoga maji ya moto au vugu vugu na pia hakikisha unaoga kwa muda mfupi kadiri iwezekanavyo na jitahidi ukishamaliza tu kuoga hakikisha mwili umeufunika vizuri usipate upepo au baridi,( nunua bathrobe) adha ya muwasho ikizidi tafuta strong anti allergies kama LORATIDINE au nyingine yeyote, nirudie kukupa pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna dada alisumbuliwa na shida hiyo
Lakini alivyo acha pombe akapona
Naye alikuwa ni mlevi haswa siyo mchezo!
Mimi nisipo kunywa pombe ndo huwashwa mwili wrote mpaka hapa naaandika lkn nawashwa tuu nikinywa tu baasi tatizo hakuna hii inanikera sana has a wakati wa usiku ndo huwa silali kabisa nakesha tuuu ama nikishiba sana muwasho hupungua na tumbo huunguruma sana pia hujaaa gesi hivyo hupelekea kujitapisha kabisa na nikinywa pombe haja kubwa hutoka ya kawaida Ila. Nisipokunywa haja hutoka muharisho

Samahani kwa muandiko mbaya ila naombeni ushauri
 
Duuh tupo wengi Mkuu. But mim huwa nikwa msimu, alafu nikianza dalili za kuashwa huwa najiskia vibaya kwenye mind. Yaan nawaza kila kitu ni kichafu. Nilisha acha kujisugua na aina yoyote ile ya kitu mwilini mwangu pale napooga. Hii ndo dawa iliyosababisha kutoka daily kuwasha na sasa ni kwa msimu
Daaaah yaan tatizo lako ni Kama langu...sijui dawa yakeee ni Nini
 
Daaaah yaan tatizo lako ni Kama langu...sijui dawa yakeee ni Nini

Minyoo sugu, Tumia dawa ya minyoo Zentel. Kunywa Chupa moja asubuhi kabla ya kula. Then Tumia tena baada ya siku 7.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nini kinasababisha kuwashwa mwili baada ya kutoka kuoga? Tatizo limenisumbua miaka 10 sasa.. Nikijisugua ndo nawashwa kabisa, nisipojisugua nawashwa kidogo afadhali lkn mtu huwezi kuoga bila kujisugua. Najisugulia kitambaa laini kabisa, nikitoka kuoga nachanganyikiwa kwa kuwashwa mno na daktari aliniambia ninywe piriton kila kabla sijatoka kuoga na nikitoka kuoga lkn haikunisaidia kabisa.
Naombeni ushauri nifanye nn manake nimekata tamaa sina raha ya kushika maji hata kidogo. Mvua ikininyeshea nawashwa haswaa. Mwili unatutumka unavimba kila nikijikuna.

Hiyo skin allergy. Miye ni asthma ya ngozi, napatwa sana na hiyo shida. Oga maji moto yanayochoma mwili kila uogapo, hata kama kuna joto. Ukioga maji baridi, utawashwa zidi. Usisugue mwili kabisa. Oga kwa sabuni za mche za kufulia nguo. Au tumia dermatologically tested shower gel.

Meza antihistamine, paka mafuta yasiyo na harufu...vaseline blue seal, Johnsons baby oil. JD Pharmacy wana choice kubwa kwa ajili ya sensitive skin...shower gels, lotions etc.
Pole sana.
 
Usiku mwema kwenu madactari wa jamii forums

Nimekua napata miwasho ,.ambayo nikiikuna inatoa ngozi nyeupe ukanda wa kiunoni

Sijajua Ni Nini na Ni kiunoni tu sio mahari pengine

Ahsanten
1587065936476.jpeg


kelphin kepph
 
kelphin kepph,
Angalia sabuni unayoogea acha kutumia na shuka ulozoea maji ya kuoga pia kama yamekaa muda mrefu acha kutumia iache uone hali itabadilika?
 
Siku mbili hizi nimefanya ka research kadogo kuhusu miwasho, nadhani hiyo yako inaweza kuwa inasababishwa na ngozi kuwa dry so ukitoka kuoga jipake mafuta fasta na pia ukijifuta na taulo usijisugue fanya kama una ji sponge kwa kugusia gusia kwenye mwili.
Uko sahihi....kwenye kujifuta ndiyo shida.. sponging uko sahihi..
 
Okay, wakuu kicha cha uzi hapo juu kinahusika.

Iko hivi, nina changamoto ya kuwasha wote kila baada kwenda kukoga.
Sasa hali hii imekua ikinisumbua kwa muda sasa, hivyo naombeni ushauri wenu kama kuna mtu ambae ameshawahi kupitia changamoto kama hii ninayopitia mimi.

Ili niweze kuiepuka maana imekuwa kero sasa.

Uzi tayari
 
Laana hizo zinapuputika unaonekana ulikuwa hauna adabu kwa wazazi na jamii yako

Ingekuwa kijijini huko mkoani wangekwambia hivyo



Ila professional zaidi ni vyema ukaenda hospitali pia ukute maji yana kitu ambacho Ni allergy kwenye mwili wako


Sometimes kuwashwa sana pia ni moja ya associated side effects or symptoms ya allergy
 
Back
Top Bottom