Tatizo la kutokwa Jasho lisilo la kawaida katika sehemu mbalimbali za mwili (Hyperhydrosis)- Fahamu Chanzo, tiba, ushauri

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
9,296
7,666
1590036070559.png

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI
JF Doctor na wapendwa wengine,

Hivi ninapoandika niko katika nchi yenye baridi kali sana inayoambatana na barafu. juzi usiku nikiwa nimelala nikaota ndoto iliyonishtua usingizini na nikajikuta nimejaa wasiwasi na papo hapo jasho jingi likaanza kunitoka.

Japo si mara yangu ya kwanza kupatwa na hiki kitu lakini safari hii nimelazimika kuuliza kwa daktari kwa sababu jasho lilikuwa jingi kupita kawaida na hasa ukizingatia kuwa kwa baridi ya huku wakati huu, sikutegemea kabisa kutoka jasho jingi kiasi hicho hata kunilazimu kufikiria kuoga kabla sijarudi tena kitandani kulala.

1. Je, mtu kutoka jasho jingi akiwa na wasiwasi kunasababishwa na nini?

2. Je, kuna hatari yoyote ya kiafya kwa hali kama hii na hasa kama inampata mtu mara kwa mara?

naombeni msaada wa elimu wapendwa

Mungu awabariki sana

Merry Christmas and Happy New Year 2012!!
---
Heshima mbele wandugu,

Nimekuwa na tatizo la kutoka jasho sana kila wakati hata kama hali ya hewa ni ya kawaida, tunapokuwa na wenzangu wao wanakuwa katika hali ya kawaida, lakini mimi nakuwa nasikia joto sana na natokwa na jasho jingi, hali hii imekuwepo kwa muda mwingi sasa.

Naomba msaada kwa anaefahamu, kama ni mwanzo wa tatizo gani na nifanye nini.

Wasalaam.
---
Habari zenu ndugu zanguni.

Nina mtoto mwenye umri wa miaka mitatu. Mtoto huyu amekuwa akitokwa na jasho jingi iwe asubuhi, mchana, jioni hata usiku. Akila anatokwa na jasho. Akilala jasho linammwagika na akilia pia jasho linamfumuka.

Hata kama ni kipindi cha baridi yeye huwa anatokwa na jasho.

Mtoto huyu si mlaji sana ila ni mnywaji sana wa maji.

Je, hali hii ni kawaida au kuna tatizo? Nini chanzo?

UFAFANUZI WA JUMLA WA TATIZO HILI
Tatizo la kutokwa ana jacho mwilini, mikononi na miguuni:

Ugonjwa huo unaitwa HYPERHIDROSIS.

Kawaida tunatoka jasho ili kuupoza mwili.Mwili unapokuwa na joto nervesystem inatuma ujumbe automatic kwenye sweatglands ili kupunguza joto.Unapokuwa na hyperhydrosis hizi nervesystem zina kuwa zinafanya kazi pasipo na mpangilio na zinatuma ujumbe wakati wote kwahio jasho linatoka hata kama mwili hauna joto.

Hali hio pia inaweza kusababishwa na mtu kuwa na sukari ya chini,hyperthyroidism au side effects za dawa.

Zipo njia tofauti za kutibu kama.
  1. Aluminium chloride solution ambayo unaweka kwenye viganja vya mikono na miguu.
  2. Potassium permanganate.
  3. Nimeshawahi kuona botox ikitumika pia lakini ni tiba ya muda hali hio hujirudia.
  4. Iontophoresis:Njia inayotumia kupitisha maji chini ya ngozi kwa kutumia umeme.
  5. Upasuaji kwenye nerve ambazo zinahusika na jasho.
Hizo njia nilizokutajia zinapunguza dalili za ugonjwa huo lakini haziondoi tatizo,njia kama za upasuaji na umeme sidhani kama
zinatumika!

1592744320653.png

UFAFANUZI WA TATIZO HILI ULIOTOLEWA NA WADAU
Hyperhidrosis ni ugonjwa wa kutokwa na jasho jingi kuliko kawaida. Kutokwa na jasho ni hali ya kawaida kwa binadamu na wanyama na kazi kubwa ya jasho ni kupoza mwili unapopata joto kubwa. Kwa kawaida mwili wa mwanadamu hutengeneza wastani wa lita moja ya jasho kila siku.

Kiwango cha jasho huweza kutofautiana kutokana na mazingira na hali ya mwili kwa mfano kipindi cha joto ama maeneo yenye joto kali, au kufanya mazoezi ya mwili kama kukimbia hufanya mwili kutoa jasho jingi zaidi ya kawaida ili kupooza mwili.

Ugonjwa wa hyperhidrosis hutokea pale mwili unapotengeneza jasho jingi zaidi ya linalohitajika kupoza mwili. Mfano ni kutoka jasho ukiwa umepumzika sehemu isiyo na joto au kutoka na jasho jingi unapoingiwa na hofu nk

Kitaalamu ugonjwa huu umegawanyika katika makundi mawili. Kuna primary hyperhidrosis na secondary hyperhydrosis. Primary hyperhydrosis huanza mara nyingi kipindi cha balehe na husababishwa na urithi wa vinasaba (genetics). Secondary hyperhidrosis huanza kipindi chochote cha maisha na husababishwa na magonjwa mengine ya mwili mfano kisukari, magonjwa ya tezi ya shingo na kadhalika.

Hyperhydrosis ni kilema kilichojificha

Mgonjwa wa hyperhidrosis hupata shida kuendana na shughuli za kawaida za maisha. Wengi hupatwa na aibu pindi jasho jingi linapolowanisha nguo au kushindwa kushikana mikono pindi viganja vinapolowa jasho jingi. Pia kuna baadhi ya shughuli humwia vigumu mfano jasho jingi mikononi husababisha ugumu wa kushika vifaa kipindi cha kazi. Ugonjwa huu huweza kusababisha msongo wa mawazo.

Tiba

Kuna tiba mbalimbali ya ugonjwa huu. Secondary hyperhidrosis hutubiwa kirahisi kwa kutibu ugonjwa unaosababisha secondary hyperhidrosis kama ilivyoelezwa hapo juu. Kwa hiyo ni muhimu kumuona daktari pindi unapopata na tatizo hili na kufanya vipimo ili kugundua magonjwa sababishi mfano kisukari na Magonjwa sababisha yakitibiwa na ugonjwa huu huisha mara moja.

Nitazungumzia zaidi primary hyperhidrosis ambayo husababishwa na vinasaba. Tiba yake nimeigawanya mara tatu. Kwanza ni kubadili mfumo wa maisha, pili ni dawa na tatu ni upasuaji.

Tukianza na kubadili mfumo wa maisha. Mgonjwa mwenye hili tatizo yampasa kubadili mfumo wake wa maisha ili kuendana na tatizo.

Kwanza inashauriwa kunywa maji mengi. Maji husaidia kupoza mwili na hivyo kupunguza kutokwa kwa jasho. Pia inashauriwa kupunguza vyakula vyenye viungo vingi, vinjwaji kama kahawa, pombe, sigara na vinywaji vichangamfu(energy drinks) maana vyakula na vinywaji hivi husababishwa mwili kutengeneza jasho.

Pia inashauriwa kuoga angalau mara mbili kwa siku kwa kutumia maji safi na sabuni yenye dawa mfano dettol.

Pia paka baking soda sehemu zinazotoa jasho jingi pindi tu umalizapo kuoga. Baking soda huharakisha kukauka kwa jasho kwa sababu ya alkalini iliyonayo.

Tumia vitoa harufu (antiperspirants/deodorants) vyenye aluminium chrolide ambayo huharakisha kukauka kwa jasho.

Tumia vikinga jasho (sweat pads) sehemu zinazotoa jasho jingi mfano sehemu za kwapa na kadhalika. Unaweza kununua vikinga jasho madukani au kutengeneza mwenyewe nyumbani kwa kutumia nguo na sponji na kuvaa ndani ya nguo.
hyperhidrosis-liners.jpg

Pia chai ya mmea uitwao salvia officinalis usaidia kupoza mwili na inashauriwa kunywa kwa watu wenye tatizo hili.

Kwenye upande wa dawa, dawa ziitwazo kitaalamu anticholinergic husaidia wenye tatizo la kutokwa na jasho hasa wanaopata tatizo hili wanapoingiwa na hofu ya kitu fulani.

Pia kwenye nchi zilizoendelea huduma ya upasuaji hutumika kwa wenye tatizo kubwa ambalo haliwezi kutibika kwa njia nyingine. Tiba hii inajumuisha kuingilia na kufunga kwa njia ya upasuaji mifumo ya fahamu inayosababisha kutoka kwa jasho.

Ukiachana na upasuaji, tiba ya kubadili mfumo wa maisha na dawa husaidia kwa kiwango kikubwa kwa mazingira yetu hapa Tanzania.

Dr Luhaja Nginila, MD
---
Wasi wasi na hofu husabaisha mwili kutoa adrenaline hormone, ambayo husabaisha shinikizo la damu (BP) kuongezeza, na basal metabolic rate (BMR) pia huongezeka mwili hutoa joto jingi sana kutokana na kuongezeka kwa BMR, hiyo taarifa hupelekwa kwenye ubongo , na ubongo unatuma taarifa kwenye tezi za jasho ( sweat glands) jasho hutoka ili kuupoza mwiliendapo hii itajirudia mara kwa mara huweza kusabisha High blood pressure, stroke, heart attack na hata sudden death.

Ni vizuri kufanya uchunguzi zaidi na kuizuia hii hali isijirudie
.
---
Nimonia esinofili (EP) ni ugonjwa ambapo aina fulani ya seli nyeupe za damu ziitwazo eosinofili hukusanyika kwenye mapafu. Seli hizi husababisha kuvurugika kwa nafasi za kawaida za hewa (alveoli) ambako oksijeni huzinduliwa kutoka kwa anga. Aina mbalimbali za nimonia esinofili huwepo na zinaweza kutokea katika kundi la umri wowote. Dalili zinazojitokeza sana sana ni pamoja na kikohozi, homa, tatizo la kupumua, na kutokwa na jasho usiku. EP hutambuliwa kwa kutumia mchanganyiko wa dalili mbalimbali, matokeo ya ukaguzi wa afya unaofanywa na mtoa huduma za afya, na matokeo ya vipimo vya damu na eksirei. Ubashiri huwa bora wakati sehemu kubwa ya EP imetambuliwa na matibabu kwa kutumia kotikosteroidi yameanzishwa.

Aina za nimonia esinofili
Ugonjwa wa nimonia esinofili umegawanyika katika makundi mbalimbali kulingana na kama kisababishi kinaweza kutambuliwa au la. Visababishi vinavyojulikana ni pamoja na baadhi ya dawa au vichochezi vya kimazingira, maambukizi ya vimelea, na saratani. EP pia inaweza kutokea wakati mfumo wa kinga umeshambulia mapafu, ugonjwa uitwao tatizo la Churg-Strauss. Wakati kisababishi hakipatikani, EP hupachikwa jina la "idiopathiki." EP ya idiopathiki inaweza kugawanywa katika "nimonia esinofili kali" (AEP) na "nimonia esinofili sugu" (CEP) kulingana na dalili ambazo mtu anapata

Dalili[hariri
Visababishi vingi vya nimonia esinofili vina dalili zinazofanana. Kikohozi, homa, kuongeza kwa tatizo la kupumua, na kutokwa na jasho usiku ni dalili maarufu na hujitokeza kwa karibu kila mtu anayeugua. Nimonia esinofili kali kwa kawaida huendelea kwa kasi sana. Homa na kikohozi zinaweza kutokea wiki moja au mbili tu kabla ya matatizo ya kupumua yameendelea na kufikia hatua ya kushindwa kupumua hivyo basi kuhitaji uingizaji hewa kwa kutumia mitambo. Nimonia esinofili sugu kwa kawaida huendelea polepole. Dalili hujilimbikiza katika kipindi cha miezi kadhaa na huwa ni pamoja na homa, kukohoa, tatizo la kushindwa kupumua, kukorota, na kupungua kwa uzito. Watu walio na CEP mara nyingi hupatikana kuwa na pumu kabla ya CEP hatimaye kutambuliwa.

EP inayotokana na dawa au vitu mbalimbali kwenye mazingira ni sawa na hutokea baada ya kufichuliwa kwa kitu kinachojulikana kusababisha. EP inayotokana na maambukizi ya vimelea ina dalili za mwanzo pamoja na dalili nyingi tofauti zinazohusiana na aina mbalimbali za vimelea vya msingi. EP katika mazingira ya saratani mara nyingi huendeleza katika muktadha wa utambuzi unaojulikana nwa habari ya uvimbe wa kansa, kansa ya kizazi, nk.

Kumekuwa na matukio ya nimonia esinofili kinachosababishwa na madawa kama vile daptomycin (Cubicin). Mbili za kesi hizi zimebainishwa kuwa kesi sugu zinazotegemea steroidi. (Rejea Clinically Infectious 2010:50 (1 Machi) pp735-739.

Chanzo: Nimonia esinofili - Wikipedia, kamusi elezo huru
---
Kutokwa na jasho ni njia mojawapo ya mwili kutoa taka na pia ni mfumo unaotumiwa na mwili ili kuupooza pale hali ya hewa au joto la mwili linapokuwa lipo juu.

Katika hali ambayo ni ya kawaida, mwili hutoa jasho baada ya mtu kufanya shughuli fulani ya kufanya joto lake lipande na ili kuliweka katika kiwango cha kawaida, mtu atatokwa na jasho, au yawezekana ikawa siyo kufanya kazi, bali kutokana na mtu kuwa na msisimko fulani, basi jasho linaweza kumtoka.

Kuna baadhi ya watu mpenzi msomaji, ambao mbali na sababu hizo hapo juu, huwa wanatokwa na jasho jingi bila ya kujali kama mtu huyo kakaa amepumzika, hana msisimko wowote, hali ya hewa kuwa nzuri bila joto, yaani haijalishi, wao hutokwa na jasho jingi muda wote. Hili ni tatizo kiafya ambalo kwa kitaalamu hujulikana kama, Hyperhidrosis.

Mpenzi msomaji, baadhi ya matatizo ya kiafya yanayoweza kumfanya mtu apate au awe na tatizo hili la kutokwa na jasho jingi muda wote ni haya yafuatayo:

Pamoja na tatizo hili kuwa gumu kitaalamu, mambo ambayo huhusishwa na tatizo hili ni matatizo ya neva zinazohusiana na glandi za jasho katika mwili na kuzifanya glandi zifanye kazi zaidi ya inavyohitajika, pia tatizo hili huhusishwa na kurithi.

Mambo mengine ambayo husababisha tatizo hili ni matumizi ya baadhi ya dawa, mfano dawa za kuondoa msongo wa mawazo, dawa za kutibu matatizo ya kansa, dawa zinazotumika kutibu magonjwa ya uzazi.

Kuna baadhi ya magonjwa ambayo pia humfanya mtu apate tatizo hili, mfano kifua kikuu, Parkinson, matatizo ya glandi (Over active thyroid gland.

Pia kwa watu wazima na hasa wanawake, hukumbwa na tatizo hili pale umri wao wa kuzaa unapokuwa umeisha (Menopause).

Mpenzi msomaji, ni vyema kama unalo tatizo hili ukawaona wataalamu wa afya ili kuweza kupata msaada unaostahili. Neva zinazotawala glandi za jasho hutumia kemikali asilia mwilini inayojulikana kwa jina la Acetylcholine, na kemikali hii pia huhusika katika mifumo mbalimbali mwilini. Kwa bahati mbaya, dawa zinazotibu tatizo hili huzuia utendaji kazi wa kemikali hii asilia na hivyo, baada ya mtu kutumia dawa huweza kupata madhara kama vile mdomo kuwa mkavu sana na matatizo katika kukojoa.

Chanzo: Tanzlife Company Limited
===
USHAURI WA NAMNA YA KUTIBU TATIZO HILI
Tiba mbadala ya kutokwa na jasho lisilo la kawaida, kwapani, usoni, viganjani n.k
Mwili wa binadamu hutoka jasho fulani jingi ukiwa upo katika mazingira ya jotoridi lililozidi kiwango, mwili unapokuwa katika kiwango fulani cha shughuli ya kukufanya utokwe jasho zaidi na wakati mwingine ukiwa na stress ya jambo fulani.

Sasa jasho linapotoka muda wowote bila activity, stress wala joto kuwa jingi basi kuna hitilafu.

Kitaalam hali hii ya kutokwa jasho kusiko kawaida kwa lugha ya kiingereza wanaita hyperhidrosis, hali hii huathiri baadhi ya maeneo mwilini hasa hasa usoni, kwapani, viganjani na kwenye nyayo.

Wataalam wanasema tatizo hili ni kijenetiki yaani linaweza kurithiwa. Tatizo la kutokwa jasho huchangiwa na overactivity kwenye neva jambo linalosababisha kutrigger tezi jasho.

Vichochezi ni pamoja na, matumizi ya madawa fulani fulani, kitambi, madawa ya kulevya ikiwemo pombe, kiwango cha chini cha sukari, malaria, kifua kikuu, shinikizo la damu na upungufu la virutubisho mwilini.

Tatizo la kutokwa jasho jingi humfanya mhusika ajisikie aibu na wakati mwingine mfadhaiko, wasiwasi na kujitenga, habari nzuri ni kuwa zipo tiba mdabala zinazopatikana kwa unafuu na urahisi ambazo mhusika anaweza kutumia nyumbani na kuondokana na kutokwa jasho jingi iwe viganjani, usoni, kwapani ama kwenye nyayo za miguu.

APPLE CIDER VINEGAR
Hii hupatikana madukani, mini supermakets ama kwenye supermarkets. Inafanya kazi kwa ufanisi kushughulikia tatizo la kutokwa jasho sababu ni kituliza nafsi cha asili kabisa,
Unaweza kuchagua kati ya yafuatayo:

1.Safisha eneo linalotokwa jasho kisha tumia pamba ama kitamba kisafi cha pamba kupaka apple cider vinegar kwenye hilo eneo, iwe viganjani, kwapani, nyayo ama usoni iache usiku mzima ( kama una ngozi sensitive na changanya maji na apple cider vinegar viwango sawa) baada ya kuoga asubuhi paka baby powder kwenye hilo eneo.

2. Changanya viwango sawa vya apple cider vinegar na maji ya uaridi ( Rosewater) na kupaka eneo linalotokwa jasho jingi, mara 2 hadi 3 kwa siku.

3.Tengeneza mchanganyiko wa wa apple cider vinegar kijiko 1 ama 2, asali mbichi kijiko 1 na maji vuguvugu glasi moja kunywa mara mbili kwa siku.
Apple cider vinegar ina manufaa mengi kiafya na pia inapambana na kitambi.

WANGA WA MAHINDI
Tiba Mbadala nyingine ni wanga wa mahindi, wanga wa mahindi unaweza kuutengeneza mwenyewe kutoka kwenye unga wa mahindi, ama kununua sokoni changanya viwango sawa vya wanga wa mahindi na baking soda, weka kwenye chupa ya powder, itumie kama powder maeneo yanayotoka jasho jingi.

MALIMAO
Malimao yapo masokoni na wengine wamepanda majumbani, ni tiba asilia ya majasho yanayotoka kwa wingi na pia inafukuza backteria wabaya, iko hivi

1.Kamua limao moja na lichanganye na baking soda vizuuri, futa jasho kwenye maeneo husika kisha paka, subiri dakika kumi ukiwa umepaka kisha safisha maeneo husika, fanya hivi mara moja kwa siku
2.Ama unaweza safisha maeneo husika chukua kipande cha limao lidondoshee chumvi na kisha paka kwenye hayo maeneo, kufanya hivi hupunguza utendaji kazi wa tezi jasho

NYANYA
Nyanya! huenda tunazitumia kila siku kwenye mboga, chakula, kwenye salad, Juisi na kadhalika lakini nyanya ni zaidi ya kiungo ni kituliza nafsi na inasaidia kurekebisha kutokwa jasho jingi ama hyperhidrosis kama wataalam wanavyoita.
Iko hivi,
1.Kata vipande viwili vya nyanya na paka sehemu husika subiri dakika 10 hadi 15 kisha safisha na maji ya uvugu vugu.

2.Ama unaweza kusaga juisi ya nyanya na kupaka sehemu husika subiri dakika 10 hadi 15 kisha safisha na maji ya uvugu vugu.

3.Ama unaweza kunywa kikombe cha juisi ya nyanya kila siku kisha ukiona tatizo linaanza kuondoka basi punguza na anza kunywa kila wiki, kisha nipigie na kusema asante.

MAJANI YA CHAI
Wengi hatufahamu lakini tumebarikiwa na majani ya chai Afrika ambayo pia ni ina ufanisi katika kuondoa hili tatizo la kutokwa na jasho hovyo,

Lowesha majani ya chai ama chukua majani ya chai yaliyotumika kisha pakaa kama hina kwenye viganja vya mikono na kuloweka miguu kwenye beseni lenye mchanganyiko wa maji ya vuguvugu na majani ya chai kibao walau kila siku kwa dakika 30, siyo tu ngozi ya miguu itakuwa laini pia tatizo la jasho miguuni litatoweka, usisahau kunywa chai ya sturungi asubuhi na jioni.

EPUKA
1.Vyakula vya pilipili
2.Mafuta ya mgando na mengineyo ya mwili yenye viambatanishi vya petroleum

Usisahau Kunywa maji mengi na yakutosha kila siku.

BAADHI YA USHAURI NA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU WA JF
Hyperhidrosis ni ugonjwa wa kutokwa na jasho jingi kuliko kawaida. Kutokwa na jasho ni hali ya kawaida kwa binadamu na wanyama na kazi kubwa ya jasho ni kupoza mwili unapopata joto kubwa. Kwa kawaida mwili wa mwanadamu hutengeneza wastani wa lita moja ya jasho kila siku.

Kiwango cha jasho huweza kutofautiana kutokana na mazingira na hali ya mwili kwa mfano kipindi cha joto ama maeneo yenye joto kali, au kufanya mazoezi ya mwili kama kukimbia hufanya mwili kutoa jasho jingi zaidi ya kawaida ili kupooza mwili.
what-is-botox-how-does-botox-work-axillary-hyperhidrosis.png

Ugonjwa wa hyperhidrosis hutokea pale mwili unapotengeneza jasho jingi zaidi ya linalohitajika kupoza mwili. Mfano ni kutoka jasho ukiwa umepumzika sehemu isiyo na joto au kutoka na jasho jingi unapoingiwa na hofu nk

Kitaalamu ugonjwa huu umegawanyika katika makundi mawili. Kuna primary hyperhidrosis na secondary hyperhydrosis. Primary hyperhydrosis huanza mara nyingi kipindi cha balehe na husababishwa na urithi wa vinasaba (genetics). Secondary hyperhidrosis huanza kipindi chochote cha maisha na husababishwa na magonjwa mengine ya mwili mfano kisukari, magonjwa ya tezi ya shingo na kadhalika.

Hyperhydrosis ni kilema kilichojificha
Mgonjwa wa hyperhidrosis hupata shida kuendana na shughuli za kawaida za maisha. Wengi hupatwa na aibu pindi jasho jingi linapolowanisha nguo au kushindwa kushikana mikono pindi viganja vinapolowa jasho jingi. Pia kuna baadhi ya shughuli humwia vigumu mfano jasho jingi mikononi husababisha ugumu wa kushika vifaa kipindi cha kazi. Ugonjwa huu huweza kusababisha msongo wa mawazo.

Tiba
Kuna tiba mbalimbali ya ugonjwa huu. Secondary hyperhidrosis hutubiwa kirahisi kwa kutibu ugonjwa unaosababisha secondary hyperhidrosis kama ilivyoelezwa hapo juu. Kwa hiyo ni muhimu kumuona daktari pindi unapopata na tatizo hili na kufanya vipimo ili kugundua magonjwa sababishi mfano kisukari na Magonjwa sababisha yakitibiwa na ugonjwa huu huisha mara moja.

Nitazungumzia zaidi primary hyperhidrosis ambayo husababishwa na vinasaba. Tiba yake nimeigawanya mara tatu. Kwanza ni kubadili mfumo wa maisha, pili ni dawa na tatu ni upasuaji.

Tukianza na kubadili mfumo wa maisha. Mgonjwa mwenye hili tatizo yampasa kubadili mfumo wake wa maisha ili kuendana na tatizo.

Kwanza inashauriwa kunywa maji mengi. Maji husaidia kupoza mwili na hivyo kupunguza kutokwa kwa jasho. Pia inashauriwa kupunguza vyakula vyenye viungo vingi, vinjwaji kama kahawa, pombe, sigara na vinywaji vichangamfu(energy drinks) maana vyakula na vinywaji hivi husababishwa mwili kutengeneza jasho.

Pia inashauriwa kuoga angalau mara mbili kwa siku kwa kutumia maji safi na sabuni yenye dawa mfano dettol.

Pia paka baking soda sehemu zinazotoa jasho jingi pindi tu umalizapo kuoga. Baking soda huharakisha kukauka kwa jasho kwa sababu ya alkalini iliyonayo.

Tumia vitoa harufu (antiperspirants/deodorants) vyenye aluminium chrolide ambayo huharakisha kukauka kwa jasho.

Tumia vikinga jasho (sweat pads) sehemu zinazotoa jasho jingi mfano sehemu za kwapa na kadhalika. Unaweza kununua vikinga jasho madukani au kutengeneza mwenyewe nyumbani kwa kutumia nguo na sponji na kuvaa ndani ya nguo.
hyperhidrosis-liners.jpg

Pia chai ya mmea uitwao salvia officinalis usaidia kupoza mwili na inashauriwa kunywa kwa watu wenye tatizo hili.

Kwenye upande wa dawa, dawa ziitwazo kitaalamu anticholinergic husaidia wenye tatizo la kutokwa na jasho hasa wanaopata tatizo hili wanapoingiwa na hofu ya kitu fulani.

Pia kwenye nchi zilizoendelea huduma ya upasuaji hutumika kwa wenye tatizo kubwa ambalo haliwezi kutibika kwa njia nyingine. Tiba hii inajumuisha kuingilia na kufunga kwa njia ya upasuaji mifumo ya fahamu inayosababisha kutoka kwa jasho.

Ukiachana na upasuaji, tiba ya kubadili mfumo wa maisha na dawa husaidia kwa kiwango kikubwa kwa mazingira yetu hapa Tanzania.

Dr Luhaja Nginila, MD
---
Utokaji wa jasho mwilini una faida za kuboresha ngozi nakuondoa uchafu mwilini pamoja na kuratibu joto la mwili. Mnyama kama mbwaanategemea Zaidi ulimi wake manake hana sweatglands. Kama ambavyo mkojounapokuwa wa njano sana inaashiria upungufu wa maji na hata uti, miili yetuinatabia ya kutupa taarifa muhimu lakini tunaweza ku-respond ndivyo sivyo.

Kuzuia utokaji wa jasho mwilini kwa kemikalini kuhatarisha afya yako na ngozi yako. Mazoezi (especially jogging) huondoamafuta mwilini ndio njia bora ya kupunguza utokaji wa jasho mara nyingi ikiwemokupunguza unywaji wa bia na supu ikiwemo kula kupita kiasi.

Kujikinga ni pamoja na kuvaa vest kablahujavaa nguo kwa nje.kutumia kemikali ni sawa na kujichubua unajihatarisha nacancer za ngozi na complication zingine kama gharama n.k.tiba mbadala kuondoanana tatizo ni njia bora zaidi ya kufuata.tuache kuwaathiriwa na u-consumerism
---
Mimi ninao huo ugonjwa na huwa natokwa jasho hasa mikononi hadi naona karaha muda mwingine

Ni ugonjwa unaotuathiri psychologically zaidi; kujishtukia, kutotoa mikono wakati wa salamu n.k

Ngoja kwanza nifute jasho mikononi :A S cry:

Nimeshawahi kutumia hizo drysol (Aluminium chloride solution na Potassium permanganate) bila mafanikio yeyote

Botox ni temporary solution na ni gharama sana huku Iontophoresis inaelezwa kuwa njia bora zaidi ya kutibu na salama lakini sijui mahala wanapotoa huduma hii bongo

Cha muhimu kuwa msafi penda kuosha mikono yako mara kwa mara na kutumia hand sanitizer oftentimes na uwe na kitambaa cha walau kukausha mikono yako pindi jasho likizidi

Mwanamama wangu anapenda mikono yangu so far anadai ni laini (labda ananipaka mafuta kwa mgongo wa chupa sijui!!); thou kweli watu tulio na tatizo hili huwa na mikono laini

Muhimu: usiwe mtumwa wa tatizo hili fanya mambo yako na jamii itakuzoea tu. Nimefarijika kujua tuko wengi waathirika wa huu ugonjwa
 
Habari za mida wana JF.

Babu yangu ana tatizo sugu la kutokwa mafuta mwilini, sasa imefikia mpaka inambidi abadilishe nguo mara mbili au tatu kwa siku.

Amejaribu dawa za hospital na miti shamba lakini haikusaidia. Sasa nauliza wana JF je hili tatizo kwanza kitaalam linaitwaje?

Na je kuna yeyote mwenye idea ya tiba juu ya hili?
 
kutokwa mafuta kivipi labda?..usoni au yanatoka kama jasho?
 
kuna makundi matatu ya ngozi, kuna ngozi zenye mafuta, ngozi za kawaida yaani sio kavu sana wala zenye mafuta na ngozi kavu. Sasa babu yako atakuwa kwenye kundi la ngozi zenye mafuta mengi.

Awe anaoga mara nyingi kwa siku (sio kubadili nguo tu) kwa kutumia sabuni maalum kwa ajili ya ngozi zenye mafuta. Pia apake mafuta ambayo hayana grisi (non grease) ambayo pia ni maalum kwa ngozi kama yake.

Aepuke kuacha kupakaa mafuta mwilini eti kwa sababu ngozi yake ina mafuta kwani kwa kufanya hivyo huongeza ukubwa wa tatizo.
 
JF Doctor na wapendwa wengine,

Hivi ninapoandika niko katika nchi yenye baridi kali sana inayoambatana na barafu. juzi usiku nikiwa nimelala nikaota ndoto iliyonishtua usingizini na nikajikuta nimejaa wasiwasi na papo hapo jasho jingi likaanza kunitoka.

Japo si mara yangu ya kwanza kupatwa na hiki kitu lakini safari hii nimelazimika kuuliza kwa daktari kwa sababu jasho lilikuwa jingi kupita kawaida na hasa ukizingatia kuwa kwa baridi ya huku wakati huu, sikutegemea kabisa kutoka jasho jingi kiasi hicho hata kunilazimu kufikiria kuoga kabla sijarudi tena kitandani kulala.

1. Je, mtu kutoka jasho jingi akiwa na wasiwasi kunasababishwa na nini?

2. Je, kuna hatari yoyote ya kiafya kwa hali kama hii na hasa kama inampata mtu mara kwa mara?

naombeni msaada wa elimu wapendwa

Mungu awabariki sana

Merry Christmas and Happy New Year 2012!!
 
Kwa Mujibu ulivyoeleza ni kuwa hiyo ni dalili ya wewe kufuatwa na Pepo Mchafu ndani ya usingizi wako. Kutokwa na jasho na wasiwasi mwingii ni Shetani mbaya anaye kufuata ndani ya huo usingizi wako. Sio ugonjwa ikikutokea siku nyingine jaribu unapoamka Treament

kama weweni mkristo soma biblia na chini ya mto wako jaribu kuweka kipande kimoja cha kitunguu saumu pamoja na mkaa mweusi mmoja na mvuje funga katika kitambaa cheusi matatizo ya kuota ndoto mbaya yatakuondokea. La kama wewe ni muislam itabidi

kila unapo taka kulala ushike Udhu kisha kichwa chako uelekee upande wa kibla unapolala kisha usome Ayatil Qursiyu mara 3,Alhamdu mara 1,ikhlaswi mara 3, Suratil falaki mara3,na suratil nasi mara 3, na uwe unataja jina la Allah unapo lala mpaka usingizi ukupate hutoota ndoto mbaya tena .
 
Pole sana, nijuavyo mimi kutokwa jasho hasa kunakotokana na hofu hutokea namna hii,hofu ni njia ya mwili kukabiliana na hali inayoukabili kwa wakati huo, hivyo sympathetic nervous system huuandaa mwili ama kupigana, kukimbia au kuzimia.

Kutokwa na jasho jingi kunatokana na mwili kuandaliwa kupigana ambapo joto hupanda juu, unapogundua kumbe hakuna lolote mfano ukitoka kwenye ndoto ,sweat glands hutoa jasho jingi ili kupoza mwili kwani tayari joto lilikuwa limepanda juu ukiwa kwenye ndoto,

kazi mojawapo ya kutoka jasho ni kuupoza mwili unapochemka,hivyo hata ukiwa nchi za baridi jasho litakutoka kwa hofu, ni mechanism ya mwili.cha msingi ni kutawala hofu na kama imekuwa inajirudiarudia waone wataalamu wa hospital DK,psychologist nk.
 
Kwa Mujibu ulivyoeleza ni kuwa hiyo ni dalili ya wewe kufuatwa na Pepo Mchafu ndani ya usingizi wako. Kutokwa na jasho na wasiwasi mwingii ni Shetani mbaya anaye kufuata ndani ya huo usingizi wako. Sio ugonjwa ikikutokea siku nyingine jaribu unapoamka Treament ...

Mpendwa mzizimkavu,

Asante sana kwa ushauri wako. mimi ni mkristu ila hapo pa kutumia kitunguu swaumu na vitambaa vyeusi, mara mkaa, ndo sijaelewa kama bado ni ndani ya wigo wa ukristu. au ndo kusema nijaribu kitu mbadala?

be blessed

pole sana,nijuavyo mimi kutokwa jasho hasa kunakotokana na hofu hutokea namna hii,hofu ni njia ya mwili kukabiliana na hali inayoukabili kwa wakati huo,hivyo sympathetic nervous system huuandaa mwili ama kupigana,kukimbia au kuzimia..

Mpendwa,

Asante sana kwa mchango wako. mie kwa baiolojia yangu ya primary na sekondari, nilikuwa naamnini kuwa mchakato wa kutoa jasho wakati wa hofu ni kama ulivyofafanua. Ila nilishangaa kwa mazingira ya baridi kali kama haya kumwaga jasho hadi kutamani kuoga maji baridi usiku!! siyo siri, niliogopa hadi kudhani nimepata ugonjwa fulani mbaya. au labda hali kama hii ikijitokeza mara kwa mara inaweza kusababisha ugonjwa fulani kwenye mfumo wa damu, fahamu etc. ndo hapo nikataka kujuzwa zaiodi na wataalam

Asante kwa kunitia moyo

ubarikiwe sana
 
mpendwa mzizimkavu,

asante sana kwa ushauri wako. mimi ni mkristu ila hapo pa kutumia kitunguu swaumu na vitambaa vyeusi, mara mkaa, ndo sijaelewa kama bado ni ndani ya wigo wa ukristu. au ndo kusema nijaribu kitu mbadala?....
ushaambiwa ni mambo ya autonomic nervous system ambayo ni kitu cha kawaida kutokea katika hali kama hiyo na haijalishi uko kwenye baridi ama joto, mechanism is the same. kwa maana hiyo hali kama hiyo ya majasho kama ulivyosema isipotokea ujue kuna shida na inabidi upate ushauri wa kitaalamu.
 
Kitaalam wasiwas una increase heart beats consequently high blood pressure,.bas kama tujuavyo blood ina certain fixed temp then blood pressure and blood temperature leads to body reaction esp sweating. Sory if i am too shallow,'just using my high school knowledge....,sign off
 
Tiba Mbadala hiyo mambo ya Dini soma biblia kila usiku japo AYa 10 kabla hujalala.

Heshima yako mkuu! Katika suala zima la tiba mbadala uko juu sana! Nadhani tiba zako zitatusaidia sana kupunguza matumizi ya hizi sumu kutoka kwa wazungu.Usichoke kutupatia tiba mbadala kila tunapohitaji.

Kuhusu issue ya Miss Judith nadhani ndoto aliyoota ilipelekea kuongezeka kwa msukumo wa damu ktk mwili wake ndo maana baada ya kushtuka akajikuta anatoka jasho.Huenda alikuwa anaota anafukuzwa na Simba mnyama!
 
Kitaalam wasiwas una increase heart beats consequently high blood pressure,.bas kama tujuavyo blood ina certain fixed temp then blood pressure and blood temperature leads to body reaction esp sweating. Sory if i am too shallow,'just using my high school knowledge....,sign off

safi sana mkuu kwa maelezo yaliyomafupi na yanayoeleweka. kuhakikisha wengine mwaweza google.

sio ushauri wa wengine waliovutishwa mibangi ya dini na wanaamini mambo ya kitoto ya eti uchawi, shetani, mungu etc. upuuzi tu.
 
Wasi wasi na hofu husabaisha mwili kutoa adrenaline hormone, ambayo husabaisha shinikizo la damu (BP) kuongezeza, na basal metabolic rate (BMR) pia huongezeka mwili hutoa joto jingi sana kutokana na kuongezeka kwa BMR, hiyo taarifa hupelekwa kwenye ubongo, na ubongo unatuma taarifa kwenye tezi za jasho ( sweat glands) jasho hutoka ili kuupoza mwiliendapo hii itajirudia mara kwa mara huweza kusabisha High blood pressure, stroke, heart attack na hata sudden death.

Ni vizuri kufanya uchunguzi zaidi na kuizuia hii hali isijirudie.
 
Asasnteni sana wapendwa.

baada ya kusoma ushauri wa members wenzangu, ninadhnai ni metabolism activity ya kawaida tu na nitaendelea na afya ya kawaida kama siku zote. ila kwa kweli nilishtuka sana.

Thanks mzizimkavu kwa ushauri mbadala. nashukuru umeshauri nijisomee biblia ila sijajua aya gani na kwa nini niisome kabla ya kulala tu. vipi nikiisoma nyakati nyingine, itasaidia?

Mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God!
 
Ebwana tatizo hilo linampata mwanangu ambae ana mwaka sasa na miezi 9 kwa kweli anatokwa na Jasho usiku mpaka namuonea huruma na hili linatokea mchana na usiku linatokea ;naomba msaada wenu wakuu tatizo ni nini hasa?
 
Heshima mbele wandugu,

Nimekuwa na tatizo la kutoka jasho sana kila wakati hata kama hali ya hewa ni ya kawaida, tunapokuwa na wenzangu wao wanakuwa katika hali ya kawaida, lakini mimi nakuwa nasikia joto sana na natokwa na jasho jingi, hali hii imekuwepo kwa muda mwingi sasa.

Naomba msaada kwa anaefahamu, kama ni mwanzo wa tatizo gani na nifanye nini.

Wasalaam.
 
Mkuu unaonaje kwa kuanzia ukajibu maswali yafuatayo:
1.Tatizo limeanza lini?
2.Wewe una umri gani+jinsia?
3.Unaishi wilaya/mji gani?
4.Hamu yako ya kula ikoje,imeongezeka au imepungua?
5.Uzito wa mwili wako unauonaje,umeongezeka,uko kawaida au umepungua?
6.Unatoka jasho zaidi wakati gani,machana,usiku au wakati wote?

Ukijibu hayo kwa usahihi,naamini madaktari watakusaidia humu,pengine hata kabla ya kwenda hosp.
 
binafsi ili mwili uwe fiti na ngozi jasho likitoka ndo vizuri. sijui kwanini tunalizuia na madawa. isije ikawa promoshen
 
Kwwa wale ambao wanatokwa jasho ,ya aina yoyote dawa ni Driclor,,kwa hapa bonngo maduka mengi hayauzi..hemu icheki kwenye picha na usome maelezo yake kwa ku search na google

images

KWA ANAYE ITAKA PIGA 0753932250 au 0657209956 utaipata kwa 30,000-32,000/= kutegemea na stock imetoka wapi?
siyo vizuri kuwakamua masikini na wenye matatizo, kwani ukiuza 15000/= utapata hasara gani?
 
Back
Top Bottom