Kwani kuna shida kukumbuka vitu vilivyotokea zamani, mimi ni mmoja wao, huwa ninakumbuka vitu na matukio mbali mbali vilivyonitokea zamani wakati nakua, nina uncle wangu alifunga ndoa mwaka 1983 kijijini, juzi hapa tukawa tunapiga story za miaka ya nyuma nikamkumbusha juu ya harusi yake ilivyokuwa na sare ambazo mama zangu walishona, siku hiyo, akawa anashangaa bado nakumbuka wakati nilikuwa binti mdogo sana huo mwaka......Binafsi huwa naona ni NEEMA ambayo Mungu ameiachilia kwangu kukumbuka matukio vya miaka ya nyuma