Kwa taarifa yako ripoti ya Mwakyembe haikumtaja Lowassa. Acha habari za kusikia. Fuatilia mambo vizuri. Kama unao huo waraka uliomtaja Lowassa, uambatanishe kwenye uzi huu tafadhali
Nitaitwa Mad man vilevile kama nitamchagua mmoja wa wagombea urais kutoka ukawa ambaye ni mshiriki mkuu katika kusababisha tatizo hili la umeme kwa watanzania na pia aliuza moja ya mgodi na rafikiye.. pia anachangiwa na matajiri kwenda ikulu,,, karibu tuichagie ACT au Fahim dovutwa rais..
Bila shaka we ni mad man kwa kushindwa kujifikirisha kama mtunzi wa Richmond kaondoka kwenye mfumo mbona wasafi waliobaki wameshindwa kurekebisha hali? Ukweli unaujua, Waliobaki CCM ndiyo wenye Richmond!
richmond imetuua kwa miaka 8 na mgombea urais wa ukawa ndiye mmiliki...
Hivi hadi leo unafikiria kuipa ccm kura? we mzima kweli ndugu?
ok brother. kwa hiyo kweli unataka kunishauri niipigie kura ccm kwa sababu richmond ni ya lowassa?Bro ripoti ya Mwakyembe ni ndefu sana itafute uisome mwenyewe vizuri usiwe mvivu kwani binafsi hata jana usiku nimeisoma,, kwa kukukumbusha tu alipohojiwa Msabaha alisema yeye ni banguchiro ( yaani mbuzi wa kafara) muhusika ni waziri mkuu na pia alipohojiwa katibu mkuu alisema dili ni ya LOwassa na mshirika mwenzie kibiashara yaaani Rostam AZIZ,, kuna mahali mchakato walinyang'anywa tanesco ukabaki wizara ya nishati mpaka Tume ikajiuliza kiburi hicho wizara inapata wapi, na utakuta kuna barua wazir mkuu alizisaini na kuwaambia tanesco wakae pembeni,, utakuta kuna ushauri mzuri kutoka PPRA na tanesco lakini wizara ya nishati iliukataa na ofisi ya waziri mkuu ikabariki mchakato uendelee.. hata Msabaha alipoondoka akaja Karamagi bado OFisi ya waziri mkuu kushirikiana na karamagai ikawainaendelea kuissuport richmond vs dowans,, NENDA KAIPITIE USIKU HUU NA UISOME KWA MAKINI NENO MPAKA NENO UTAELEWA,, PIA TAFUTA DOCUMENTS ZIHUSUZO MGODI WA BUZWAGI NAZO ZISOME PIA UONI NI NINI KILITOKEA CHURCHILL HOTEL...
ok brother. kwa hiyo kweli unataka kunishauri niipigie kura ccm kwa sababu richmond ni ya lowassa?
je escrow nani mmiliki?
PAC ya ZZK ilieleza kila kitu kama Mwakyembe alivyoeleza kila kitu... ishi kwa uhalisia usipende kuishi kwa hisia...
Teh..teh..teh...WATANZANIA HATUDANGANYIKI NG'O...hatuwapi kura CCM wezi wa mali za umma kwa miaka zaidi ya 50.
Ha ha ha nimecheka sana mkuu itakuwa wafanyakazi wenyewe tu mkuu wameichoka CCM.Mhhhhh ccm haikosi sababu. Kwa hiyo chadema ndio wanakata umeme. 
huku kwet tegeta wamishakata, ccm inabidi iondoke tu! maana hakuna namna
Mkuu Tabora na Geita ni zaidi juzi usiku wa jumamosi kuamkia jumapili walikata umeme alfajiri ya kumi na moja mpaka naondoka jumatatu asubuhi umeme ulikuwa haujarudi na jana usiku hapa Tabora kulikuwa hakuna umeme .ha ha haa ni sheda, moro tushazoea..