Pole sana ndugu
tatizo hilo kweli ni kubwa na lina kera sana japo kwa afrika hatulipagi uzito unaostahili
pili nikupe pongezi kwa kutambua kuwa ni tatizo, na kuwa tayari kulitatua ama kuondokana nalo
moja wapo ya jinsi ya kulitatua ni kutafuta jambo la kufanya au kufanya jambo unalopenda pale unapohic kuudhika. kwa mfano mimi napenda sana muziki na novel, so nikowa bored au nikizingulia hasa home na ma wife, huwa naingia zangu chumbani then full blast ya muziki wa raggae au rnb. au nikiona siku hiyo hata mziki hauingii, nachukua zangu kitabu nachopenda au nilichowahi kusoma hata kama nakisoma kwa mara ya saba, then natafuta kakivuli murua, nakula zangu novel
njia ya pili ni kufanya mazoezi, trust me! wakati mwingine hasira inatokana na mwili kuwa na nguvu nyingi isiyotumuka (un-burned energy), hivyo kufanya mazoezi; kwanza kutafanya mwili wako uwe poa yaani fit, na pili kuna activate mind sana, just try this, you will tell me
tatu ni kubadili mtazamo tu, think positive. mfano rais lincolin wa marekani aliwahi kupokea barua ikiwa na neno moja tu "stupid", badala ya kukasirika alisema hivi, "nimewahi kupokea barua nyingi sana, lakini zote zilikuwa zinaanza na ujumbe kisha jina la muhusika mwishoni, lakini barua hii ya leo imeanza na jina kisha aliyeandika akasahau kuweka ujumbe" so my ndugu, think positively, hakuna atakaye kuona zoba bali utaonekana mwenye hekima
karibu katika ulimwengu huru wa msongo