Tatizo la Ethiopia ni nini hadi raia wake kuikimbia nchi yao kwa mamilioni?

Kwa miaka mingi imekuwa kawaida sana kusikia taarifa za raia wa Ethiopia wakikamatiwa Tanzania na nchi mbalimbali za Kusini mwa Africa kama wahamiaji haramu.

Hata huko Uarabuni katika nchi kama Saudia Arabia wahamiaji haramu wa Ethiopia ni wengi sana na kila mara huwa wanateswa na wanarudishwa nchini mwao ila bado hawaachi kuzamia huko!

Kwa nini raia wengi wa Ethiopia wanakimbia sana nchi yao hasa ukizingatia matatizo waliyo nayo Ethiopia ni sawa na matatizo ya nchi nyingi za Africa, wana rasilimali nyingi sana lakini pia inasemekana serikali wana jenga sana nchi yao kwa miondombinu?
Tatizo Ethiopia ni mji mkuu tu
 
Tatizo la Ethiopia,
Uchumi umeshikiliwa na serikali kwa kiasi kikubwa so wananchi hawana pesa, ni kawaida kabisa kwenda hotelini Addis na kuombwa pesa na mhudumu,

Pia mishahara ya serikalini ni midogo hata kwa wenye elimu kubwa , mishahara Yao ni mbuzi tu,

Shida nyingine ni vita vya wenyewe kwa wenyewe

Hivo watu wanakimbia kutafuta greener pastures, waethiopia wengi wapo abroad US wapo wengi sana na wamesoma so inawezekana wanawatumia pesa ndugu zao kuwasaidia wahame,

Wanatumia njia haramu kwa sababu kuna baadhi ya maeneo kuna vita baina ya raia na serikali so usitarajie mtu wa hivi ataweza kupata vibali vya kusafiria,
 
Sababu moja kubwa ni kutafuta maisha na pia Wa Ethiopia wengi walio nje ya Ethiopia wana Uchumi mzuri kutokana na Umoja wao na ndio wafanyabiashara wakubwa hasa huko Kusini wameweza kununua majengo makubwa ya Bree Street na kuweka maduka sasa kinachofuata ni kuwaita ndugu zao ili wawape kazi za kufanya ndio maana unaona Wa Ethiopia wengi wakiitafuta SA na Nchi zingine wengine wenye uwezo wanatumia Ndege yao wale wengine wasio na Connection ndio wanatumia hizo safari za kuungwa ungwa na Wasomali..
 
Kwa miaka mingi imekuwa kawaida sana kusikia taarifa za raia wa Ethiopia wakikamatiwa Tanzania na nchi mbalimbali za Kusini mwa Africa kama wahamiaji haramu.

Hata huko Uarabuni katika nchi kama Saudia Arabia wahamiaji haramu wa Ethiopia ni wengi sana na kila mara huwa wanateswa na wanarudishwa nchini mwao ila bado hawaachi kuzamia huko!

Kwa nini raia wengi wa Ethiopia wanakimbia sana nchi yao hasa ukizingatia matatizo waliyo nayo Ethiopia ni sawa na matatizo ya nchi nyingi za Africa, wana rasilimali nyingi sana lakini pia inasemekana serikali wana jenga sana nchi yao kwa miondombinu?
Tatizo kubwa ni idadi ya watu. Ni nchi chache zinaweza kuwa na idadi kubwa ya watu na maisha mazuri.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Nakazia hapo mkuu, kutoka Ethiopia mpaka kufika Afrika kusini muEthiopia mmoja anatumia sio chini ya milioni 5 hesabu ya haraka haraka

Hawa jamaa wanalipa pesa ndefu sana kwa watu wanaowasafirisha kutoka huko wanakotoka mpaka kufika Afrika Kusini

Kuna jamaa mmoja aliacha magunia ya mchele Arusha akachagua kuwabeba waiEthiopia kuwapeleka mpakan Tunduma

Kiufipi jamaaa wanalipa pesa ndefu sana ni juzi tu hapa limekamatwa V8 likiwa na bendera ya CCM likiwasafirisha, jamaa anaweza kudhani waliomba lift bila shaka

Mtu atumie zaidi ya mil 5 kama nauli tu kisha useme atokako hakuna hela? Ni nadhani itakuwa ni changamoto zingine tu ndio zinawakimbiza
hata mabaharia wetu enzi zile wanazamia walikua wanauza chochote home wapate fungu la safar haimaanishi walipotoka kulikua na neema kisa wana hela ya kuhonga njiani
 
Kwa miaka mingi imekuwa kawaida sana kusikia taarifa za raia wa Ethiopia wakikamatiwa Tanzania na nchi mbalimbali za Kusini mwa Africa kama wahamiaji haramu.

Hata huko Uarabuni katika nchi kama Saudia Arabia wahamiaji haramu wa Ethiopia ni wengi sana na kila mara huwa wanateswa na wanarudishwa nchini mwao ila bado hawaachi kuzamia huko!

Kwa nini raia wengi wa Ethiopia wanakimbia sana nchi yao hasa ukizingatia matatizo waliyo nayo Ethiopia ni sawa na matatizo ya nchi nyingi za Africa, wana rasilimali nyingi sana lakini pia inasemekana serikali wana jenga sana nchi yao kwa miondombinu?
Huko kwao pagumu sana nasikia aliye nacho anacho wewe hata upambane vipi huwezi kuja kupata kitu wanaishi kikoo na kikabila yaani kama kwenu ni masikini basi sahau kutoboa nchini humo ni kama umeshapigwa mihuri kwa hiyo wengi bora afe kiba afe beki waondoke tu huko maana hata ukibaki haina maana sanasana utakufa na umasikini wako..

Kingine wanasprit ya upambanaji hatari hawa watu wasomali wanasubili.
 
Kwa miaka mingi imekuwa kawaida sana kusikia taarifa za raia wa Ethiopia wakikamatiwa Tanzania na nchi mbalimbali za Kusini mwa Africa kama wahamiaji haramu.

Hata huko Uarabuni katika nchi kama Saudia Arabia wahamiaji haramu wa Ethiopia ni wengi sana na kila mara huwa wanateswa na wanarudishwa nchini mwao ila bado hawaachi kuzamia huko!

Kwa nini raia wengi wa Ethiopia wanakimbia sana nchi yao hasa ukizingatia matatizo waliyo nayo Ethiopia ni sawa na matatizo ya nchi nyingi za Africa, wana rasilimali nyingi sana lakini pia inasemekana serikali wana jenga sana nchi yao kwa miondombinu?
Wana hali ngumu sana sana yani njaa ya kufa mtu viongozi wao wamekosa vision tundu lissu aliwahi kusema wamewekeza kwenye vitu badala ya watu, wana mandege matreni ya umeme toka enzi ila njaa imekithiri wengi wao ni masikini wa kutupwa
 
Sera ya Ethiopia kuwalazimisha vijana kujiunga na jeshi kwa mujibu wa sheria imekuwa ni moja ya chanzo cha vijana wengi kuikimbia nchi pia
 
Uchumi wa watu ndio nini acha kukariri hakuna nchi yoyote hapa afrika mashariki inayoikaribia Ethiopia kwa lolote kuanzia iq, gdp, population, purchasing power, infrastructures nk.

Kinachowakimbiza waethiopia kwao ni majanga ya asili kama ukame yanayopelekea njaa na kingine ni damu tu ya upambanaji ndio sababu huwezi kukuta waethiopia wanakimbilia kwenye nchi kama Tanzania, msumbiji, uganda, zambia.

Waethiopia wamejazana sana uarabuni na marekani na kwa hapa Afrika sauzi tu. Nchi yao ni landlocked na kipindi hichi wanafosi kupata eneo la bahari watakuwa wanazamia kupitia meli.
Umeshawahi fika Ethiopia au umeishia kusoma mtandaoni?
 
Hata Mimi miaka kadhaa Before nilikua nashanga na bado nashangaa Hadi sasa, ikabidi nifuatilie kidogo kulikoni. Iko hivi Waethopia kwao wanaubaguzi mkubwa wa kikabila na koo, hii ni asili ya jamii zote za wahabeshi kuanzia Somalia, sudani, Eritrea na hawa jirani zetu kwa mzee tolu pale. Pia Wingi wa watu, ardhi kame, Vita vya kikanda kugombea ardhi hizi no baadhi ya sababu zinazo wafanya wahabeshi wanaona Bora wakafe mbele kwa mbele. Ila jamaa ni wapambanaji.
 
Uchumi wa watu ndio nini acha kukariri hakuna nchi yoyote hapa afrika mashariki inayoikaribia Ethiopia kwa lolote kuanzia iq, gdp, population, purchasing power, infrastructures nk.

Kinachowakimbiza waethiopia kwao ni majanga ya asili kama ukame yanayopelekea njaa na kingine ni damu tu ya upambanaji ndio sababu huwezi kukuta waethiopia wanakimbilia kwenye nchi kama Tanzania, msumbiji, uganda, zambia.

Waethiopia wamejazana sana uarabuni na marekani na kwa hapa Afrika sauzi tu. Nchi yao ni landlocked na kipindi hichi wanafosi kupata eneo la bahari watakuwa wanazamia kupitia meli.
Mkuu kwanza nikupongeze....yaani umeongea ukweli mtupu....hawa jamaa nilikuwa nao gerezan...kwanza yatupasa tufahamu kiuchumi Ethiopia ipo mbali sana hata kenya hatii mguu....kwanza wanatushangaa Tz kwa nn sis tupo karibu na South Africa afu tunalega...kwanza watambue hawa jamaa kwa kichwa kimoja anaandaa zaidi ya mil 20 ili tu afike south Africa kule wana ndugu zao ambao nao walifanikiwa kuzamia...na niwachapa kaz sana sana na wakikutanq nje ya Ethiopia bila kujali ukabila wana shirikiana sana sana...wanakamatwa watahukumiwa mwaka mmoja na nusu na watakaa mwaka mmoja...watarudi kwao na watajipanga tena kwa safar nyingine...yaan wanakuambia Tz ndio pagumu kupitika ila ukifanikiwa kupita tuu...wanatoboa na Target yao ni ulaya
 
Sababu moja kubwa ni kutafuta maisha na pia Wa Ethiopia wengi walio nje ya Ethiopia wana Uchumi mzuri kutokana na Umoja wao na ndio wafanyabiashara wakubwa hasa huko Kusini wameweza kununua majengo makubwa ya Bree Street na kuweka maduka sasa kinachofuata ni kuwaita ndugu zao ili wawape kazi za kufanya ndio maana unaona Wa Ethiopia wengi wakiitafuta SA na Nchi zingine wengine wenye uwezo wanatumia Ndege yao wale wengine wasio na Connection ndio wanatumia hizo safari za kuungwa ungwa na Wasomali..
Mkuu kwanza nikupongeze....yaani umeongea ukweli mtupu....hawa jamaa nilikuwa nao gerezan...kwanza yatupasa tufahamu kiuchumi Ethiopia ipo mbali sana hata kenya hatii mguu....kwanza wanatushangaa Tz kwa nn sis tupo karibu na South Africa afu tunalega...kwanza watambue hawa jamaa kwa kichwa kimoja anaandaa zaidi ya mil 20 ili tu afike south Africa kule wana ndugu zao ambao nao walifanikiwa kuzamia...na niwachapa kaz sana sana na wakikutanq nje ya Ethiopia bila kujali ukabila wana shirikiana sana sana...wanakamatwa watahukumiwa mwaka mmoja na nusu na watakaa mwaka mmoja...watarudi kwao na watajipanga tena kwa safar nyingine...yaan wanakuambia Tz ndio pagumu kupitika ila ukifanikiwa kupita tuu...wanatoboa na Target yao ni ulaya
umeandika mataputapu
 
Unasifia upuuzi.
 
Hata hapa nchini kuna hali ngumu ila raia wanabanana tu hapa hapa.
... UKIONJA DHIKI YA ETHIOPIA HUTADIRIKI KULALAMIKIA TENA UGUMU WA MAISHA BONGO!
NB: THE HORN OF AFRICA IS A DESERT THAT'S TOO OVERPOPULATED!
... MASS STARVATION IS PRESSURING THE YOUTH OUT!
 
Back
Top Bottom