Tatizo la Ethiopia ni nini hadi raia wake kuikimbia nchi yao kwa mamilioni?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,626
46,271
Kwa miaka mingi imekuwa kawaida sana kusikia taarifa za raia wa Ethiopia wakikamatiwa Tanzania na nchi mbalimbali za Kusini mwa Africa kama wahamiaji haramu.

Hata huko Uarabuni katika nchi kama Saudia Arabia wahamiaji haramu wa Ethiopia ni wengi sana na kila mara huwa wanateswa na wanarudishwa nchini mwao ila bado hawaachi kuzamia huko!

Kwa nini raia wengi wa Ethiopia wanakimbia sana nchi yao hasa ukizingatia matatizo waliyo nayo Ethiopia ni sawa na matatizo ya nchi nyingi za Africa, wana rasilimali nyingi sana lakini pia inasemekana serikali wana jenga sana nchi yao kwa miondombinu?
 
Ethiopia bado kwa kiasi kukubwa wana mfumo wa uchumi unaopangwa na Serikali kuu kama ilivyo China au North Korea ila kwao bado haujafaulu kama China, hivyo maisha ya mtu moja mmoja ni duni sana japo kuwa Serikali yao ina hela sana.

Hii hali inapelekea wengi kuamua kwenda nje kujaribu bahati ya kufanikiwa kimaisha.
 
Wana uchumi wa vitu kama infrastructures sio uchumi wa watu
Uchumi wa watu ndio nini acha kukariri hakuna nchi yoyote hapa afrika mashariki inayoikaribia Ethiopia kwa lolote kuanzia iq, gdp, population, purchasing power, infrastructures nk.

Kinachowakimbiza waethiopia kwao ni majanga ya asili kama ukame yanayopelekea njaa na kingine ni damu tu ya upambanaji ndio sababu huwezi kukuta waethiopia wanakimbilia kwenye nchi kama Tanzania, msumbiji, uganda, zambia.

Waethiopia wamejazana sana uarabuni na marekani na kwa hapa Afrika sauzi tu. Nchi yao ni landlocked na kipindi hichi wanafosi kupata eneo la bahari watakuwa wanazamia kupitia meli.
 
Inaonekana wewe ndio umekariri mkuu…uchumi Ethiopia wane-hold watu wachache sema baada ya bwana Ahmed kuingia amejitahidi ku-bridge gap la wasiokuwa nacho na ma don
 
Ethnic violence ni moja wapo ya issues pia….huwezi kukaa sehemu hakuna amani. Kuna ethnic groups zaidi ya 80 na karibia zote zinai-confront serikali
 
Uchumi wa watu ndio nini acha kukariri hakuna nchi yoyote hapa afrika mashariki inayoikaribia Ethiopia kwa lolote kuanzia iq, gdp, population, purchasing power, infrastructures nk.

Kinachowakimbiza waethiopia kwao ni majanga ya asili kama ukame yanayopelekea njaa na kingine ni damu tu ya upambanaji ndio sababu huwezi kukuta waethiopia wanakimbilia kwenye nchi kama Tanzania, msumbiji, uganda, zambia.

Waethiopia wamejazana sana uarabuni na marekani na kwa hapa Afrika sauzi tu. Nchi yao ni landlocked na kipindi hichi wanafosi kupata eneo la bahari watakuwa wanazamia kupitia meli.
Nakazia hapo mkuu, kutoka Ethiopia mpaka kufika Afrika kusini muEthiopia mmoja anatumia sio chini ya milioni 5 hesabu ya haraka haraka

Hawa jamaa wanalipa pesa ndefu sana kwa watu wanaowasafirisha kutoka huko wanakotoka mpaka kufika Afrika Kusini

Kuna jamaa mmoja aliacha magunia ya mchele Arusha akachagua kuwabeba waiEthiopia kuwapeleka mpakan Tunduma

Kiufipi jamaaa wanalipa pesa ndefu sana ni juzi tu hapa limekamatwa V8 likiwa na bendera ya CCM likiwasafirisha, jamaa anaweza kudhani waliomba lift bila shaka

Mtu atumie zaidi ya mil 5 kama nauli tu kisha useme atokako hakuna hela? Ni nadhani itakuwa ni changamoto zingine tu ndio zinawakimbiza
 
mahala popote pale duniani pakishakuwa na mizozo ya mara kwa mara pamoja na njaa sababu ya ukame.. hakuna mwanadamu atapafurahia kukaa hapo.
 
Back
Top Bottom