Tatizo la Biashara haramu ya binadamu na Viungo vyake kwa Tanzania na Afrika

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Salaam Wakuu,

Inadaiwa kuna watu zaidi ya milioni 45 ambao wametumbukizwa katika biashara hii inayoingiza kiasi cha dola bilioni 32 kwa mwaka, na hivyo, kuchuana kwa karibu sana na biashara haramu ya silaha na dawa za kulevya. Wanawake, na watoto wadogo ndio walengwa wakuu.

Kundi hili la Wanawake na Watoto, wanawachukua na kutumikishwa katika kazi ngumu, utalii wa ngono pamoja na biashara haramu ya viungo vya binadamu. Hali hii inachukuliwa kama ukatili dhidi ya utu na heshima ya binadamu na haki za Binadamu

Chanzo kikubwa cha biashara haramu ya binadamu na viungo vyake ni mifumo ya utumwa mamboleo, umaskini wa hali na kipato, Vita, Migogoro kwenye Jamii, Kutokuwepo Usawa na Watu kujitenga katika baadhi ya Jamii.

Hali hii ya biashara ya binadamu inachukuliwa kama ni kukosekana kwa maadili na utu wema. Watu wanaoingizwa kwenye biashara ya biandamu au utumwa mamboleo ni wale wanaokabiliwa na mambo kama baa la ujinga, ukosefu wa fursa za ajira au majanga na matamanio ya kutaka kuwa na maisha bora zaidi.

Wakimbizi na wahamiaji duniani wanaosababishwa na Vita na ghasia, ni vichocheo vya biashara haramu ya binadamu.

Makundi ya wahalifu wa kimataifa wameendelea kupandikiza mbegu ya chuki na uhasama katika jamii na kusababisha vita, ghasia na mipasuko ya kisiasa, kikabila na kijamii ambapo watu wanakimbia Nchi zao. Ripoti mbalimbali zinaonesha wasafirishaji wa biashara haramu wa binadamu huwanyonya wahanga wa biashara hiyo.

Nchini Tanzania, Usafirishaji haramu wa ndani ni mkubwa zaidi kuliko usafirishaji haramu wa nje ya Nchi. Ndani ya Nchi Tanzania, Wanaoshiriki kwenye biashara ya Binadamu ni Waanafamilia wa wahanga, marafiki au madalali wanaowarubuni kwa ahadi za kuwapa msaada wa elimu au kuwapatia ajira katika maeneo ya mijini. Watoto maskini kutoka sehemu za ndani ndani vijijini wapo katika mazingira hatarishi ya kusafirishwa kiharamu.

Wasafirishaji haramu huwanyonya wasichana kwa kuwafanyisha kazi za majumbani kote nchini na katika madanguro ya kuwafanyisha matendo ya kingono hasa katika maeneo ya Utalii.

Wasafirishaji haramu wanawalenga wasichana wadogo kutoka mashambani na kwenye vijiji maskini, kwa kuwalipa wazazi wao pesa kidogo, na kuwatumia vibaya wasichana hao katika utumwa wa kingono kwa kwa wafanyabiashara ambao wana Imani potofu kwamba kufanya mapenzi na msichana ‘bikira’ kutasaidia biashara zao kushamiri.

Wasafirishaji haramu wengine wanawaingiza watoto katika ajira za lazima kwenye mashamba ikiwa ni pamoja na ufugaji ng’ombe, mbuzi. Watoto wengine wanapelekwa Katika machimbo ya madini na kwenye migodi ya kuvunja mawe na kwenye boti za uvuvi ambazo hufanya shughuli zake kwenye bahari kuu.

Baadhi ya watu waovu hutumia vibaya taratibu za kitamaduni za kusaidia kuwalea watoto pale ambapo wazazi maskini wanawaamini na kuwatoa watoto wao kwa jamaa ambao ni matajiri au wanafamilia wanaheshimika katika jamii, ambapo wanawaingiza
watoto hao katika ajira za lazima kama wafanyakazi wa majumbani.

Watoto wengine huwekwa bondi kwa Wasafirishaji haramu wa dawa za kulevya mara nyingine huwashikilia binadamu kama ‘amana’ kwa muda hadi malipo yanayohitajika yatolewe kikamilifu.

Hapa chini nimeweka takwimu na visababishi kwa Nchi ya Afrika kulinganisha na Mabara Menigne.

picha takwimu 2.png

mbili chart.png
 
Back
Top Bottom