Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Tanzania ni chanzo, mkondo, na nchi kusudio la safari kwa wanaume, wanawake na watoto
wanaokabiliwa na ajira za kulazimishwa pamoja na biashara ya ngono. Kasi ya matukio ya biashara haramu ya usafirishaji wa ndani inazidi ile ya matukio au kiwango cha biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu kimataifa na biashara hii hurahisishwa na ndugu, marafiki, au madalali wa wahanga ambao hutoa ahadi za msaada wa elimu au kupata ajira yenye faida sehemu za mijini ama nje ya nchi.

Idadi ndogo ya watoto wa kitanzania na watu wazima wanakabiliwa na utumwa wamajumbani, aina nyingine za ajira ya kulazimishwa, na biashara ya ngono mara nyingi kutoka kwa Watanzania wengine katika nchi nyingine ikiwa pamoja na Msumbiji, Ethiopia, Afrika Kusini, Uganda, Yemen, Oman, Falme za Kiarabu, Saudi Arabia, Pakistan, Uingereza, Marekani, Ufaransa, Italia, na pia katika nchi nyingine za kiafrika, mashariki na kati.

Kuna taarifa za vyombo vya habari kwamba watoto wa kitanzania wenye ulemavu wa viungo wanasafirishwa hadi Kenya ili wafanywe ombaomba wa kulazimishwa na kwamba wasichana wa kitanzania wanaingizwa kwenye biashara ya ngono nchini china, Kudstar (Iraq) na India

TAKWIMU ZA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI WA BINADAMU
Watu 49.6 MilionI waliishi kwenye hali ya utumwa mamboleo mwaka 2021, kati ya hao, 27.6 milionI
walitumikishwa katika kazi za shuruti na 22 milioni katika ndoa za lazima. Kati ya watu milioni 27.6 waliotumikishwa kwenye kaz zai shuruti, 17.3 milioni walinyoywa kwenye sekta binafsi, 6.3 milioni kwenye biashara ya ngono bila hiari na 3.9 milioni kwenye kazi za shuruti zilizodhaminiwa na nchi husika (State-sponsored trafficking).

Wanawake na wasichana wanasadikika kuwa 4.9 milioni miongoni mwa wale wanaotumikishwa kazi kwa shuruti na wale wa soko la ngono na 6 milioni wanatumikishwa kwenye sekta nyinginezo za uzalishaji mali (ILO Report, 2021).

Kwa mujibu wa Ripoti ya UNODC 2022, asilimia 65% ya wahanga wote wa biashara ya usafirishaji
haramu wa binadamu duniani ni wanawake, watoto, na wasichana. na Kichwa kimoja kinasadikika kumuingizia mhalifu (perpetrator/ trafficker) kati ya dola za kimarekani 3000-15,000.

Pia soma: BIASHARA HARAMU YA BINADAMU: Umeshawahi kujiuliza wauza karanga na kahawa za kutembeza wanatokea wapi hapa Dar?
 
Asante sana kwa bandiko hili. Pengine ungetusaidia maandiko na takwimu zaidi kuhusu mambo haya (Human Trafficking) hususani kwa nchi ya Tanzania, ili wanaharakati tuzidi kujenga hoja kwa watunga sheria na sera nchini. Asante sana.
 
Tanzania ni chanzo, mkondo, na nchi kusudio la safari kwa wanaume, wanawake na watoto
wanaokabiliwa na ajira za kulazimishwa pamoja na biashara ya ngono. Kasi ya matukio ya biashara haramu ya usafirishaji wa ndani inazidi ile ya matukio au kiwango cha biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu kimataifa na biashara hii hurahisishwa na ndugu, marafiki, au madalali wa wahanga ambao hutoa ahadi za msaada wa elimu au kupata ajira yenye faida sehemu za mijini ama nje ya nchi.

Idadi ndogo ya watoto wa kitanzania na watu wazima wanakabiliwa na utumwa wamajumbani, aina nyingine za ajira ya kulazimishwa, na biashara ya ngono mara nyingi kutoka kwa Watanzania wengine katika nchi nyingine ikiwa pamoja na Msumbiji, Ethiopia, Afrika Kusini, Uganda, Yemen, Oman, Falme za Kiarabu, Saudi Arabia, Pakistan, Uingereza, Marekani, Ufaransa, Italia, na pia katika nchi nyingine za kiafrika, mashariki na kati.

Kuna taarifa za vyombo vya habari kwamba watoto wa kitanzania wenye ulemavu wa viungo wanasafirishwa hadi Kenya ili wafanywe ombaomba wa kulazimishwa na kwamba wasichana wa kitanzania wanaingizwa kwenye biashara ya ngono nchini china, Kudstar (Iraq) na India

TAKWIMU ZA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI WA BINADAMU
Watu 49.6 MilionI waliishi kwenye hali ya utumwa mamboleo mwaka 2021, kati ya hao, 27.6 milionI
walitumikishwa katika kazi za shuruti na 22 milioni katika ndoa za lazima. Kati ya watu milioni 27.6 waliotumikishwa kwenye kaz zai shuruti, 17.3 milioni walinyoywa kwenye sekta binafsi, 6.3 milioni kwenye biashara ya ngono bila hiari na 3.9 milioni kwenye kazi za shuruti zilizodhaminiwa na nchi husika (State-sponsored trafficking).

Wanawake na wasichana wanasadikika kuwa 4.9 milioni miongoni mwa wale wanaotumikishwa kazi kwa shuruti na wale wa soko la ngono na 6 milioni wanatumikishwa kwenye sekta nyinginezo za uzalishaji mali (ILO Report, 2021).

Kwa mujibu wa Ripoti ya UNODC 2022, asilimia 65% ya wahanga wote wa biashara ya usafirishaji
haramu wa binadamu duniani ni wanawake, watoto, na wasichana. na Kichwa kimoja kinasadikika kumuingizia mhalifu (perpetrator/ trafficker) kati ya dola za kimarekani 3000-15,000.

Pia soma: BIASHARA HARAMU YA BINADAMU: Umeshawahi kujiuliza wauza karanga na kahawa za kutembeza wanatokea wapi hapa Dar?
Hiyo biashara ina hela balaa kama unataka nikuunganishe nicheki mkuu PM iko wazi
 
Back
Top Bottom