Tatizo CHADEMA ni zaidi ya 'Kadi' ya Dkt. Slaa

Tatizo CHADEMA ni zaidi ya 'Kadi' ya Dkt. Slaa

WOWOWO

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2011
Posts
599
Reaction score
457
Wana Bodi

Heshima kuu

Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia mtifuano unaoendelea ndani ya Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) ukianza na mikiki mikiki ya uchaguzi wake, uhasama uliojengeka baada ya uchaguzi huo na sasa kile kinachoitwa usaliti wa baadhi ya vijana na kuanza kumuona Dkt. Wilbroad Slaa kama pandikizi na mtu aliyewekwa na CCM kukimaliza CDM nimejiridhisha pasi na shaka kwamba uongozi wa CDM chini ya Freeman Mbowe na Dkt. Slaa mwenyewe umebeba gunia zito sana kichwani.

Kwa vijana hawa wa CDM ni wazi gunia hili la Mbowe na Dkt. Slaa hawalioni hata kidogo wao wanachoona ni ajira ndani ya CDM.Wanataka kuona wanapata mianya ya ajira na kuweza kuendesha maisha yao ya kila siku.

I once said, kama kuna changamoto na kazi kubwa iliyopo mbele ya CDM na uongozi wake wa sasa ni uwezo wa kuhimili mihemuko ya vijana wake ambao wengi wao ni graduates wa vyuo na ambao ajira kwao ni moja ya changamoto kuu. Na kwa kuwa wamekuwa wakishiriki mikutano na maandamano ya chama wanachoona mbele yao ni ajira ndani ya CDM na si vinginevyo.

Matumaini yao wanapovaa magwanda vyuoni ni kuona viongozi wa juu wana waajiri chamani na wanaanza maisha yao mapya ya ajira. And don't forget once unapojitolea kuvaa gwanda la CDM kama wanavyofanya vijana wengi probability ya kupata ajira ndani ya Serikali ya CCM inabaki kuwa ndogo au sawa na hakuna kabisa. Facts za hili zipo hata humu JF wanaweza kujitokeza wahanga.Note'wengine hata vyuoni wametimuliwa.

Generally ninapomtazama Dkt. Slaa na Mbowe kwa kweli unaona kazi ngumu na iliyojaa kila aina ya mateso mbele yao. Wao wako tofauti na uongozi wa CCM. CCM inaweza kabisa kutawanya ajira zake katika kuwapoza vijana wenye mihemuko na mori za ajira kutokana na kwanza kuwa na mtandao mpana, resources za kuweza kuwalipa vijana hawa lakini pia CCM ndiyo inaendesha Serikali na fursa zake zote.

Unapokuwa na kundi kubwa la vijana wanaovuliwa na chama kutoka vyuoni na ambao pengine tayari wako black marked na system ya ajira huku wakitegemea chama kama ajira zao lazima utegemee chokochoko na matatizo makubwa sana.

Kwanza vijana watanunulika kirahisi, pili hata wanaposhiriki chaguzi na kushindwa kihalali hawataridhia maana ni sawa na kukosa ajira, tatu kutazuka makundi yasiyo na mlengo wa kutetea maslahi ya taifa bali ya wivu, fitina, usaliti na majungu. Ikifikia hapa huwezi ukajenga taasisi iliyokamaa na imara maana wakati kundi fulani likikitetea chama na taifa kwa ujumla lingine litakuwa tofauti na kuibua chokochoko.

CDM na uongozi lazima uwe makini sana na kundi la vijana. Bahati nzuri ndiyo walio wengi katika chama na wana matumaini makubwa ya kutengeneza maisha yao humo.Ni lazima CDM inapoendelea na mkakati wake wa kuchonga vijana kwa ajili ya chama wasisitize mambo makuu manne. Kwanza uzalendo uliotukuka kwa taifa, pili, ajira zao, tatu, kujitolea na kuwa tayari kufia mageuzi ya kimfumo nchini na nne vijana waeleweshwe kuwa hakuna uwezekano wa chama kuweza kuaccomodate kila kijana anayehitimu chuo bali wengine watabaki kuwa wanachama na wafuasi tu huku wakifanya shughuli zao zingine.

Naliona tatizo ndani ya CDM na tatizo ni vijana wenye muhemuko, mori na hasira zaidi za kukosa fursa ndani ya chama na si 'kadi' ya Dkt. Slaa maana kwa kweli ni hoja ya kitoto na anayeibeba na kuishikia bango naye anakuwa mtoto pia.
 
CDM pesa iko, viongozi wanatumbua na spouses wao!
 
kama umemaliza wahi lumumba ukachukue vocha za malipo ya ku-post jf
 
Uzuri ni kwamba wanafiki na waroho wanajulikana kila leo na kujitaja! Ndio maana wanapo vuliwa uanachama msishangae kwani ni lazima chama kiendelee kusafishwa!
 
umeandika vyema, wala haitaji akili nyingi kujua kuwa ulichosema kina ukweli ucopungua 80%.
big up
 
WOWOWO,

Next time ukiandika jaribu kuandika CHADEMA badala ya CDM.Hata hivyo ni article nzuri imetulia!

-Ukombozi wowote hauhitaji uroho wa vyeo.Mihemko ya inayotokana na kukosa vyeo ni mihemko ambayo ikiendekezwa inaweza kutuletea matatizo mengine huko baadae tukishachukua Dola.Mwanamageuzi yeyote ni lazima awe na uvumilivu badala ya kutolea macho vyeo.Kama ni vyeo watu waende CCM ambako kuna vyeo vingi ambavyo vinatungwa kila siku.Ni bora tubakie na wanamapinduzi au wanamageuzi wa kweli badala ya kutazama vyeo

-Kama kuna mapungufu (ofcourse( ni lazima yawepo ndani ya chama kikukubwa kama CHADEMA yatamalizwa ndani ya vikao.Vijana ni lazima waendelee kutoa maoni yao na kuendelea kufundishwa darasa la kiitikadi ili wazidi kukomaa hasa wanaotoka vyuoni.Hapa tusichanganye na wale traitors ambaio wanajulikana.Wale hawahitaji darasa lolote zaidi ya kuelekeza kimbunga cha M4C kiwatupe nje.ODM wamefanikiwa hili ndiyo maana wanakaribia kushika dola na wamekuwa instrumental katika reform Kenya.Vijana wasaliti wanaoangalia interest zao kwa gharama ya Taasisi si wenzetu na ni political liability.Wanajua wanachofanya.No apology!

-Naamini katika Taifa lisilo na ubaguzi na linalojali raia wake ili siku moja mtanzania ajivunie kuwa mtanzania.Naamini fursa ya kufikia huko ni kupitia CHADEMA imara itakayotoa dira na taswira ya baadae kama Taifa kubwa.Nipo tayari kwa lolote kufikia huko kupitia CHADEMA.So kupitia CHADEMA ndipo ndoto ya mababu zetu waliokufa kishujaa itakapokuwa realized.Hawakupigania vyeo isipokua dignity na pride ya mtanzania na mwafrika kwa ujumla.

-Tanzania is my country and I have a great sense of love, passion, and commitment to contribute and impact greatly to its second birth

-Tanzania is not going to be changed by the growing mountain of prayers that booms out of our churches and mosques daily; rather, the transformational revolution which our country needs would be possible through redefining our patriotism. Only Tanzanians in Tanzania through formidable institutions like CHADEMA can do this. If the radical transformation of Tanzania is dependent upon my dying, then I'm ready to die for my homeland. That would mean: the new nation after my death shall serve the needs of the future generation equally; build a transparent, air and truly independent judiciary.

An executive totally incorrupt and accountable to both the man in suit as well as market women on their duty...then I'm ready to die in order to stop this gross economical assault, unbalanced deprivation and inhuman treatment of generations past and present
 
kama umemaliza wahi lumumba ukachukue vocha za malipo ya ku-post jf

Tumia akili ndogo tu kuangalia post angalau tatu nyuma za mtoa mada kabla hujakurupuka.Jamaa ameonyesha ukweli halisi lakini kwa kuwa wewe ni ndizi huwezi ona hiyo.Inawezekana kabisa wewe ni mmoja wa vijana hao ambao mna hasira ya kukosa ajira hivyo mnaitegemea CDM kwa kuwatafutia ajira zenu.Jamani si kila anayetoa ushauri unaopingana na mawazo yako basi awe ametumwa toka Lumumba.
 
Wenye njaa wanajulikana kabisa kuwa ni wakina Mtela Mwampamba na genge lake.
 
Mkuu hakuna haja kwa chama makini kama CHADEMA kupoteza muda na genge dogo sana la vijana wachache wanaojua nini wanachokitaka kukifanya dhidi ya CHADEMA.

*Swali ni kwanini mara tu baada ya kukosa vyeo au kushtumiwa kuwa wao ni mamluki ndani ya CHADEMA wanatoa kucha zao na kuonyesha rangi zao halisi?
 
Uzuri ni kwamba wanafiki na waroho wanajulikana kila leo na kujitaja! Ndio maana wanapo vuliwa uanachama msishangae kwani ni lazima chama kiendelee kusafishwa!

Je chama kina uwezo wa kuhimili challenges zinazoletwa na wanaojitoa au kufukuzwa. CCM yenyewe haijawa na uwezo huo. Nadhani fukuza inayotegemewa kwa kutumia nguvu ya washkaji wa Tanga, Lindi, Mtwara, Msumbiji na kwingineko are so temporal kukidhi maslahi ya muda mrefu.
 
watanzania na tanzania..........
Ipo siku kitaeleweka....
Siku moja tutatoka ICU....siku moja tutaacha kupumulia mashine. Mda huo hatutaitaji CDM wala CCM, mda huo tutahitaji IQ zetu.
 
Je chama kina uwezo wa kuhimili challenges zinazoletwa na wanaojitoa au kufukuzwa. CCM yenyewe haijawa na uwezo huo. Nadhani fukuza inayotegemewa kwa kutumia nguvu ya washkaji wa Tanga, Lindi, Mtwara, Msumbiji na kwingineko are so temporal kukidhi maslahi ya muda mrefu.

CHADEMA ni tofauti na CCM...Ndiyo maana ni mbadala.Hutegemei Rais atakayetoka CHADEMA awape masharti nafuu wezi wa EPA.No no no!
 
Mkuu hakuna haja kwa chama makini kama CHADEMA kupoteza muda na genge dogo sana la vijana wachache wanaojua nini wanachokitaka kukifanya dhidi ya CHADEMA.

*Swali ni kwanini mara tu baada ya kukosa vyeo au kushtumiwa kuwa wao ni mamluki ndani ya CHADEMA wanatoa kucha zao na kuonyesha rangi zao halisi?

Ni kwa sababu zilizotajwa hapo juu.
 
Hii hoja ina mashiko sana na ndo tatizo la watawala wetu ukishajitambanua wewe ni mpambanaji dhidi ya serikali utakosa na hata fursa ya elimu utandamwa ndo ilivyo hivyo haiwezi kuepukika.

Kuna kipindi cha nyuma tuntamenke alileta hoja hapa kwanini mnyika na vyeo vingi kwa chama hoja ili ukiiangalia ilijaa chuki ya mtu kukosa cheo fulani ndani ya chama sasa anaona mambo hayaendi lazima aanzishe chuki.

Kwa chama kama chadema chenye operation nyingi za kufanya kinashindwa kuajiri vijana wengi au hata kuwalipa vijana sasa vijana wasipo pewa posho wakati M4C vinapopita hata maandamano wanaanza kujenga chuki fulani.

Tukubali kabisa kuna vijana wako kwenye vyama kutumiza malengo yao ya kimaisha sasa anapoona kitu fulani hajafanikiwa kashindwa sehemu fulani kiuhalali lazima chokochoko zianze.

Sasa chama bado kichanga sana ukizingatia ruzuku inayotoka ni milioni 200 na ushee bado ndogo kulipa tu watu walioko makao makuu na operation zote za chama inakua ngumu sana.

Solution
1:vijana walioko kwenye mapambano wasitegemee ajira za uongozi tu ndani ya chama wanaweza kubuni miradi midogo sehemu walipo hata kujikita kwenye kilimo cha kisasa atakaye hitaji msaada anione nimpe mbinu.

2:chadema ni chama kinachokua kwa kasi sana na kukua kwa kasi kwa chadema kuna watu nao wanapenyeza mikono yao kumekua na uuzaji holela wa combat za chama na vifaa vingine chama kinakosa mapato pia kinashindwa tengeneza ajira kwa vijana wake.

Chama kifungue duka pale makao makuu ambapo vifaa vyote vya chama vitapatikana pale hapa chama kitajua kwa mwezi zimetoka combata 200 chama kimeingiza sh ngapi,chama kitajua pia kwa mwezi zimeuzwa vifaa vingine vingapi.

Sasa kama tutaanzia pale makao makuu halafu taratibu tunafungua maduka mengine mikoani kama arusha,mwanza,kigoma na sehemu nyingine kwenye haya maduka kutakua na kanda za cd kuanzia kampeni za sangara na operation nyingine hapa unawapa vijana 20-30 ajira za muda mfupi na mrefu huku mapambano yakiendelea na chama kikipata pesa.

2:chama kibuni miradi ya kuingizia pesa zaidi
Hapa chama kinaweza kufungua miradi mifupi na mirefu ambapo vijana wengi ndani ya chama watapata ajira ndani ya chama
I:gazeti za chama chadema
Hili likitoka mara mbili kwa week haliwezi kukosa kutoa ajira kwa vijana 20 hivi inahitaji mbinu na ubunifu kuanzisha gazeti ambalo litatoa report nzuri za chama kwa haraka.
Mfano leo kuna mkutano kesho tuone picha na vingine kama linaweza kuuza nakala hata 20000 kwa siku kwanini usiweze kutoa ajira.

ii:Radio na tv
Ukiwa na hivi vitu tv tusijidanganye bado sana inahitaji pesa nyingi lakini radio tunaweza mudu kwa muda mfupi na kuweza kuajiri vijana.

Na miradi mingine mbali mbali.

Huwezi kuwa mwanaharakati au mpambanaji kama huna pesa ya kula utanunulika tu lazima.

Fk
 
Umesema vyema mkuu,hoja sio kadi ni ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana.mfano wale waliojiita Bavicha walilamika baadhi kutoshirikishwa kwenye shughuli za kampeni. Ningeshauri Chadema yafuatayo: 1) chadema itoe nafasi za vijana wa kawaida (wasio viongozi) waliotayari kuingia kwenye operesheni za chama sehemu mbalimbali nchini,vijana hao wanaweza wakachanganywa kutoka mikoa mbalimbali.hii itasaidia kupata ujira mdogo/posho kutoka kwenye chama. 2) chadema ianzishe media mbalimbali kama gazeti,Redio na Tv. Pia waajiriwe wengi kwenye hizo media wawe vijana,hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana. 3) chadema waendelee kuwa na vijana wakiwapa hope,kwamba lengo la kudai uhuru/ukombozi kwa mara ya pili ni kutaka raslimali zetu ziwanufaishe watanzania, wakiwemo vijana. Ni hayo kwa muda.
 
SIYO SIRI, Makala imeenda shule. Namuona Kitila Mkumbo hapa na nina imani atalifikisha kwa wahusika ili walione hili.

Kuna haja ya kuongea na kila kijana anayekuja kwenye chama ili asiwe na mawazo ya kuwa "Kwa kutumia Chadema, nitatoka".

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom