Tatizo CHADEMA ni zaidi ya 'Kadi' ya Dkt. Slaa

Tatizo CHADEMA ni zaidi ya 'Kadi' ya Dkt. Slaa

kama umemaliza wahi lumumba ukachukue vocha za malipo ya ku-post jf

Umesoma bandiko au ni walewale wa kuwaza posho na mshiko tu? Na hiyo Lumumba ni ya nani na iko wapi? Waza nje ya itikadi bali hoja yenyewe.
 
Sio kukosa vyeo tu

mf.heche vs. Waitara, kukosekana busara kwa kila kijana ku'book jimbo kabla ya muda muafaka
ya zitto na shibuda
 
Afisa Uenezi wa CHADEMA Mh. Erasto Tumbo akimjibu Nape Nnauye ''Nape acha Propaganda; Zungumzia hoja za msingi ...............


source: chadematv youtube
 
Last edited by a moderator:
......hapa ni maji yamezidi unga au ni unga umezidi maji.......kazi ya kichwa sio kufuga nywele tu...........
 
Nadhani siyo lazima CHADEMA iwafanyie kila kitu vijana wetu,Kijana kama kijana yeye mwenyewe anatakiwa kuwa na upeo wa mawazo kuwa anahitaji nini katika maisha.Na changamoto yoyote itakayoonekana na kijana akaitolea maamuzi basi ikitolewa na kijana mwenyewe inaweza kumnufaisha yeye na vijana wenzake kuliko kupata "Ready Made decisons"
Kama vijana kuna changamoto kubwa ya ajira basi wawe wa kwanza kutatua tatizo hilo.Wawe "Problem Solvers na siyo Problem Makers"Tukiweza kuwaweka hivyo basi changamoto kubwa ya ajira itatatuliwa.
Siyo rahisi kumwambia kijana nenda uwe mjasiriamali,kuna ardhi kubwa,nenda.Akisha enda anafanyaje?Pembejeo,majembe,mahali pa kuishi,kula.Ni vitu vingi vinatakiwa kabla haujamwanbia kijana nenda shamba kalime au fanya mradi huu,bila kianzio ataweza?
Kikundi kitakapoona wanania na lengo la kuwa wakulima wadogo au wakubwa,wajasiriamali hapo ndipo jamii nzima inapokuja kutafuta njia gani nzuri ya kuisaidia kikundi au jamii hiyo iliyoamua na kuona mbele wanaweza kufanya nini.
Watanzania wengi tumelelewa katika maisha ya kuajiriwa zaidi kuliko kujiajiri ni msingi mbovu ambao inabidi tuubadilishe sisi wenyewe tusisubiri mtu kutoka nje atusaidie.
 
Dhambi ile ile ya kuwabagua wasiokuwa wa kasikazini,waislamu na zitto kabwe sasa inawatafuna.ahsante mungu.
 
kama umemaliza wahi lumumba ukachukue vocha za malipo ya ku-post jf

Kaka look like umekariri vibaya. Si kila mwenye kushauri au kuelezea changamoto au threaty basi ni adui. Lets eliminate our weekness but at the same time develop our strength
 
WOWOWO,

Next time ukiandika jaribu kuandika CHADEMA badala ya CDM.Hata hivyo ni article nzuri imetulia!

-Ukombozi wowote hauhitaji uroho wa vyeo.Mihemko ya inayotokana na kukosa vyeo ni mihemko ambayo ikiendekezwa inaweza kutuletea matatizo mengine huko baadae tukishachukua Dola.Mwanamageuzi yeyote ni lazima awe na uvumilivu badala ya kutolea macho vyeo.Kama ni vyeo watu waende CCM ambako kuna vyeo vingi ambavyo vinatungwa kila siku.Ni bora tubakie na wanamapinduzi au wanamageuzi wa kweli badala ya kutazama vyeo

-Kama kuna mapungufu (ofcourse( ni lazima yawepo ndani ya chama kikukubwa kama CHADEMA yatamalizwa ndani ya vikao.Vijana ni lazima waendelee kutoa maoni yao na kuendelea kufundishwa darasa la kiitikadi ili wazidi kukomaa hasa wanaotoka vyuoni.Hapa tusichanganye na wale traitors ambaio wanajulikana.Wale hawahitaji darasa lolote zaidi ya kuelekeza kimbunga cha M4C kiwatupe nje.ODM wamefanikiwa hili ndiyo maana wanakaribia kushika dola na wamekuwa instrumental katika reform Kenya.Vijana wasaliti wanaoangalia interest zao kwa gharama ya Taasisi si wenzetu na ni political liability.Wanajua wanachofanya.No apology!

-Naamini katika Taifa lisilo na ubaguzi na linalojali raia wake ili siku moja mtanzania ajivunie kuwa mtanzania.Naamini fursa ya kufikia huko ni kupitia CHADEMA imara itakayotoa dira na taswira ya baadae kama Taifa kubwa.Nipo tayari kwa lolote kufikia huko kupitia CHADEMA.So kupitia CHADEMA ndipo ndoto ya mababu zetu waliokufa kishujaa itakapokuwa realized.Hawakupigania vyeo isipokua dignity na pride ya mtanzania na mwafrika kwa ujumla.

-Tanzania is my country and I have a great sense of love, passion, and commitment to contribute and impact greatly to its second birth

-Tanzania is not going to be changed by the growing mountain of prayers that booms out of our churches and mosques daily; rather, the transformational revolution which our country needs would be possible through redefining our patriotism. Only Tanzanians in Tanzania through formidable institutions like CHADEMA can do this. If the radical transformation of Tanzania is dependent upon my dying, then I'm ready to die for my homeland. That would mean: the new nation after my death shall serve the needs of the future generation equally; build a transparent, air and truly independent judiciary.

An executive totally incorrupt and accountable to both the man in suit as well as market women on their duty...then I'm ready to die in order to stop this gross economical assault, unbalanced deprivation and inhuman treatment of generations past and present

Ben Saanane nimekuelewa sana.Nadhani kazi iliyopo kwa CHADEMA ni kuwafanya vijana hawa wenye mihemuko na mori kuamini pia katika haya unayoyaamini. Itakuwa ni kama kucheza ping pong kama kundi la vijana lililo ndani ya chama halitakuwa na ndoto moja kama ulivyojaribu kueleza.

Mwisho wa siku lazima chama kiwe na mikakati ya kupika vijana na kuwaandaa kweli katika kuleta mabadiliko chini ya uzalendo na uaminifu uliotukuka. Hali iliyopo sasa kwa miongozi mwa vijana wa CHADEMA si tu haireflect utayari na commitment katika kuyaendea mabadiliko bali wanaonekana kama agent wa kupoza mabadiliko yenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Chadema kama chama mbadala wa CCM inabidi vijana wake wajipambanue kwa kuweka maslahi ya nchi mbele na sio kukumbwa na fikra za vijana wa CCM ambao wako radhi kujitoa fahamu na kulamba miguu ili wafikiriwe u-DC, ujumbe wa tume na vijisafari vya hapa na pale.

Nitaendelea kusema kwamba, kama ukijitathmini ukaona umeingia kwenye siasa for personal gain, basi umechagua njia ambayo sio sahihi. Tumefika hapa kwa sababu ya watu wa aina hii ambao kwao wao uongozi sio mzigo ambao inabidi kujitolea kuubeba bali wanaona uongozi ni dili, yaani umeula.

Si lazima kila mtu awe kiongozi wa kisiasa, yapasa wengine kuwajibika katika nafasi nyingine za kutumikia nchi yetu. Na hatuwezi kuruhusu siasa kuwa sehemu ya watu kutoka kimaisha. Ni kujenga jamii ya watu wa hovyo hovyo ma-opportunist na wenye kusikilizia nani mwenye dau kubwa ili wahujumu na kisha kutangaza uasi.
 
Mkuu hakuna haja kwa chama makini kama CHADEMA kupoteza muda na genge dogo sana la vijana wachache wanaojua nini wanachokitaka kukifanya dhidi ya CHADEMA.

*Swali ni kwanini mara tu baada ya kukosa vyeo au kushtumiwa kuwa wao ni mamluki ndani ya CHADEMA wanatoa kucha zao na kuonyesha rangi zao halisi?

Kuweka rekodi vizuri siyo kukosa vyeo anachozungumzia mtoa mada ni kukosa ajira kwa maana wanategemea ajira kutoka chadema mfano kufunguliwa labda ofisi za chama katika wilaya na mikoa na baadaye kuwaajiri
 
Back
Top Bottom