Bado asilimia kubwa sana ya watanzania hawajajua nguvu ipatikanayo kwa kusoma vitabu! Kiukwe vitabu vina mchango mkubwa sana katika kubadisha maisha, kiroho na kimwili pia, unapojenga tabia hii mara kwa mara huwa kuna mabadiliko yanayotokea kuanzia ndani hata ule uwezo wa kutoa hoja inaongezeka!! Binafsi tokea nimeansa kusoma articles na vitabu vya mafanikio, saikolojia, mahusiano, Dini na biographs za watu ninao wakubali sana! Nimeona mabadiliko mengi sana ndani yangu! So tujenge utaratibu wa kusoma vitabu! Kama una malengo ya kuwa mtu mkubwa lazima ujue vingi ili kukusaidia katika mazingira tofauti!!