Tathmini yako mpaka muda huu mwaka unaelekea kuisha umesoma vitabu vingapi???

CTX

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
1,273
984
Bill Gates, tajiri namba moja duniani, yeye anasoma vitabu 50 kwa mwaka (wastani wa kitabu kimoja kwa wiki).

Warren Buffet, Tajiri namba Mbili duniani, anasoma kurasa 600 kwa siku (wastani wa vitabu vitatu kwa siku),unadhani kwa mwaka anasoma vitabu vingapi???,,,noma sana!!!

wewe mpaka sasa umesoma vitabu vingapi?

mimi mwenyewe kiukweli nimegusagusa tu vitabu mbalimbali hata sijamaliza kuvisoma na wakati mwingine sisomi kabisaa...nafanya mambo mengine...ila sasa hivi najitahidi kusoma vitabu tofauti na mengi nazidi kujivunza vitu mbalimbali na kuongeza maarifa zaidi.
 
Bado asilimia kubwa sana ya watanzania hawajajua nguvu ipatikanayo kwa kusoma vitabu! Kiukwe vitabu vina mchango mkubwa sana katika kubadisha maisha, kiroho na kimwili pia, unapojenga tabia hii mara kwa mara huwa kuna mabadiliko yanayotokea kuanzia ndani hata ule uwezo wa kutoa hoja inaongezeka!! Binafsi tokea nimeansa kusoma articles na vitabu vya mafanikio, saikolojia, mahusiano, Dini na biographs za watu ninao wakubali sana! Nimeona mabadiliko mengi sana ndani yangu! So tujenge utaratibu wa kusoma vitabu! Kama una malengo ya kuwa mtu mkubwa lazima ujue vingi ili kukusaidia katika mazingira tofauti!!
 
nmesoma namba za magufuri tu, hadi kirumi tayari nasubiri tu alete mtaala mpya..............mwaka wangu huu mie looh!
 
Vitabu nilivyosoma mwaka huu
1.uchumi kuwa mzuri sio lazima muwe na mapesa ndani,hata kuipata hela kwa shida ni uchumi mzuri
2.fedha za kulipa watumishi mishahara na nyongeza ipo tayari lkn had Leo hiki kitabu hakijatoka
3.bomoa bomoa ni kwa mikoa mingine tuu,mwanza HAPANA
4.Viwanda vitaajiri watu wengi sana lkn serikali haitaki kuajiri
5.Tutatumia fedha zetu kujenga reli na barabara bila mikopo kutoka nje ,Leo deni la taifa limeongezeka
Mwandishi wa hivi vitabu mungu anamuona
 
Mie sijui ila ni vile vya shule miaka ile labda nimebaki na kimoja biblia ukijumlisha na vile havizidi 30
 
Kusoma vitabu inaweza hisiwe ishu sana, ila aina ya vitabu unavyo soma ndio tatizo linapoanzia.

Tujiulize hivi leo hapa kwetu kuna watunzi wa aina zipi za vitabu?
 
Tatizo Wengi Wetu Tunasoma Tu Any Books Bila Kujua Akili Zetu Zinahitaji Nini...Muhimu Ni
"KuSoma Kwa Target Na Malengo"
 
Mimi sisomag kabisa vitabu aisee
Mwenzangu na mie...! Kwanza kizungungu chenyewe chenga. Na vya sijui ni vipi, maana vitabu vyote vinavyozungumziwa ni vya KIINGEREZA....! kwakifupi utamaduni huo hatuna labda mlioanza utamaduni huo na kuona hayo mabadilko tunaomba mtushauri tuanzie wapi kujizoesha huo utamaduni. Au tuanzie kwa ras simba?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom