Tathmini: Matokeo ya Uchaguzi wa Udiwani uliofanyika Februari 9, 2014

CHADEMA ilikuwa inatetea kata 3 na ikafanikiwa kutetea moja. Pia ikafanikiwa kushinda kata mbili ambazo zilikuwa ni za CCM. Kata ilizopoteza ni ile ya Bunda iliyoenda ccm na ile ya Kigoma iliyoenda NCCR MAGEUZI. IMETETWA kata ya Kiborlon, imepoka toka kwa ccm kata za sombetini na njombe. CCM ilikuwa inatetea kata 24. Imetetea kata 22, imepoteza kata 2. Pia imeshinda kata 1 ambayo ilikuwa ni ya CHADEMA, kule Bunda. Kwa hesabu za haraka. CCM ndo imefanya vizuri zaidi. Ni sawa na mzazi mwenye watoto wengi na ikafanikiwa kuwasomesha watoto wote isipokuwa wawili. Ni tofauti na yule mwenye mtoto mmoja halafu akasema kuwa anatunza vizuri mtoto wake huku akimcheka yule mwenye watoto 10 ambaye anatunza vizuri watoto wote isipokuwa wawili ambao hawafuati maagizo ya wazazi wao
 
Kulikuwa na bwana mmoja aliyepewa jiwe kubwa sana ambalo aliambiwa akiliponda likapasuka vipande vipande,atapata dhahabu.Bwana huyu baada ya kuponda jiwe lile mara miamoja,alikata tamaa,akaghafirika na kutupa nyundo chini na kuondoka.Mwingine aliyekuja aliponda nyundo moja tu na jiwe lile likapasuka vipande vipande,hatua moja au mpondo mmoja ulimkosesha yule bwana dhahabu.

Ni kwamba,katika hatua yoyote ya maisha,hatuna budi kujua changamoto na matatizo ni njia ya kuelekea kwenye neema.Hakika mwisho wa kitu,kiwe kizuri au kibaya hauji upesi.Kazi ambayo imeshafanywa na Chadema ni kubwa.Wenye kukata tamaa na kile wanachoona kimefanyika au na matokeo yaliyotangazwa,ni watu wabaya sana.Si watu wema,hawajui uchungu wa mapambano.Wengi wetu tunafanya maamuzi nyuma ya keyboards zetu,na kamwe hatuna uthubutu wa kujua kiwango cha mapambano.

Uchaguzi huu ukipimwa kwa mizania ya kisayansi,ni ukweli usiopingika kuwa Chadema ndio washindi and CCM stand loosers!! Bilioni moja ukiondoa shilingi moja si bilioni tena,tutaiita bilioni moja kasoro,Shilingi mbili ukiongeza Sh moja,pesa hiyo inakuwa imeongezeka.Katika hili CCM wakati wanatafakari kuzipoteza kata zao,CDM hawatafakari maumivu wanatafakari kwanini hawakuongeza zaidi.Haya ni mambo mawili tofauti.

Katika uhalisia wa mambo unavyokwenda,haya si matokeo ya chama chochote kujitapa,ni kujitafakari na kuchukua hatua.Niliwahi kuandika hapa jamvini,kuwa bila ya chadema kufanya decentralization,hali itaendelea kuwa hivi hivi.Nakumbuka huko kwetu kuna kijiji ambacho hata gari hawajawahi kuliona na mpaka sasa wanajua rais ni nyerere.Lakini mfumo wa uongozi ulio katika kijiji kile umejikita mizizi sana.Haiwezekani CDM mtake kila kijiji na matawi yote yamjue Dr.Slaa na Mbowe.Hebu vifanye vijiji,matawi na mashina yawe na imani na uongozi wa mahali pale.Wape uwezo hawa viongozi wa chini,wanyweshe majina ya bendera kama CCM walivyofanya.Nina babu yangu mpaka leo ukimwambia kwanini unaipenda CCM hana zaidi ya kusema kuwa ni kwa sababu ilileta uhuru.Hakuna cha ziada walichonacho watu juu ya ccm,haiwezekani mindset ya watu ikabadilika kwa chopa inayotua kwa masaa kadhaa,lazima mabadiliko yafanywe.

CDM punguzeni centralization,decentralize the party na nguvu ya umma inayohubiriwa ionekane.

Ni hayo tu!
 
Sikuzote huwa naamini mutu hufurahiha usindi wake pale anapo shinda chakuangalia hapo je!aliye sinda kasinda katika usindani wahaki hapo jibu hapo nihapana,nihapana kwasababu Kuna viasilia vingi vinaonyesha kwamba kuna upande haukutendewa hakikabisa tumesudia baadhi ya wagombea wachadema wakiwekwa ndani dakika zamwisho zakutangaza matokeo (b)kutobolesha dafutali lawa piga Kula hilo nitatizo kubwa sana Kuna vijana wapo wengi sana hajapiga Kula yote hayo yanatokana natume yauchaguzi kutokuwa Hulu inafanya mambo kwakufuata wale walio wachagua hapo sasa utajiitaje musindi wakati wakati ulingo wamapambano hukuweka sawa
 
Matokeo ya chaguzi ndogo yametangazwa katika zote 27, ikionyesha kuwa CCM wamepata ushindi kateka kata 24 na CHADEMA kata nne. Somo kubwa nililojifunza kutokana na matokeo haya ni kwamba watanzania 'wananchi walio wengi' hawajitambui kifikra kabisa. Haiwezekani katika hali hii ngumu ya maisha, iliyosababishwa na watawala wetu, wakaipatia CCM ushindi huu. Hii injenga picha kuwa tusijeshangaa CCM ikapata ushindi wa kishindo 2015. Ili kuepuka hali hii elimu inahitajika sana miongoni mwa wananchi hivyo basi wapenda ukombozi ni wakati muafaka kueneza elimu hii kwa kasi kubwa.
Nawasilisha
 
mimi huwa na walaumu sana vijana tuna siasa za mdomoni, kuliko vitendo vijana wengi huwa hawajiandikishi na hata kama wakijiandikisha huwa hawendi kupiga kura cha msingi niwasihi vijana wenzangu kupiga kura ni swala la mhmu sana hata kama ccm wanaiba kura zikiwa nyingi hawawezi kiba lazima wataogopa tu.
 
Maana uchaguzi huu mdogo umetupa taswira kwamba wananchi bado wana imani na ccm kwa kuipatia kata 23 kati ya 27 zilizoshindaniwa. Tulikuwa hatulali kila thread ni, chopa, M4C na makorokoro kibaao kama vile tayari chadema imechukua nchi! Bakora hii mliotandikwa na wananchi ni fundisho kwenu kuacha siasa za kibabe na visasi pengine wananchi watawaelewa.

ni kweli kabisa,waache siasa za chuki chuki na udini
 
CDM wanatakiwa wafanye homework yao kama viongozi, bado hawafaulu kujua ni kwa vipi kura zinaibiwa na safari hii wameibiwa tena kura feki kibao, haiwezekani kata ya kule kahama wapiga kura ktk daftari wako 4400 halafu wapige kura watu 1500 na bado CDM whawaji na majibu.CDM kukubalika tayari mmekubalika kwa wananchi tatizo lenu hamuwasaidii wananchi mbinu za kubaini wizi.Kazi kubwa iliyobaki ni kubaini wizi short of that mtakuwa kama Svangirai hadi leo haamini alishindwaje na mugabe.CDM mnapambana na wachina siyo ccm.take care
 
Uliyosema ni sahihi kabisa ila swala la maboresho ya daftari la wapiga kura lita chukua muda kwa sababu CCM na Serilali wana jua kuwa kama wataruhusu daftari kuboreshwa vijana wengi wataingia na huo ndio utakuwa ushindi wa vyama vya upinzan.
Mimi si msemaji wa CDM lakini naweza kusema kuwa; daftari lisipoboreshwa CDM haitakuwa tayari kushiriki kweye uchaguzi mkuu. Matokeo yaq chaguzi za udiwani ni mabaya kwa CDM kwa sababu ya daftari kutokuboresha na mmeguko uliomo ndani ya CDM kwa sasa.

CDM tuna lakufanya; nalo ni kujirekebisha
 
mie naamini tatizo kubwa chadema ni mwenyekt, tumbadilishe coming uchaguzi mkuu ndani ya chama mwezi june - tupate kiongozi atakayetupa dira mpya...........
hata ule mgogoro wa akina zito alichemsha namna ya kuushughulikia, mihemko ya akina lema ilichukua nafasi!
 
Habari wakuu,

Naomba wana-CHADEMA msiumize vichwa kuhusu huu ushindi wa CCM.Msidhani CCM inakubalika au inapendwa sana na wananchi.

Watanzania wataipenda CCM kwa vipi wakati kila siku wanalia na maisha magumu,ufisadi,mishahara midogo,bei za umeme,shida za maji,huduma mbovu za afya,ubovu wa miundo mbinu,migogoro ya wakulima na wafugaji,unyanyasaji wa polisi n.k

Wanachofanya watanzania kwa sasa ni kuchagua "mwenye chongo katika jamii ya vipofu awaongoze njia".Ndio maana watu wengi leo hii hawapigi kura kwani wamekata tamaa kabisa.Wasiopiga kura wengi wao ni wana CCM wanaona hakuna tena maana ya kuchagua viongozi.

Wapinzani kwa sasa mnachotakiwa ni kuonyesha kwa vitendo tofauti yenu na CCM.

Wapinzani,all you need to do is to walk the walk.

Mnapinga posho huku mnazichukua,mnapinga mashangingi wakati kiongozi wa kambi ya upinzani anatumia shangingi,mnaambiwa muungane hamtaki,vita ya madaraka katika vyama vya siasa hakuishii,boresheni na kujali viongozi na ofisi katika ngazi za chini hamtaki n.k

Wapinzani,wananchi bado wamewaweka katila "probation".

NB:Ingawa CCM ni wabovu,watanzania wengi wana hofu ya kufanya "majaribio" katika uongonzi wa nchi na hivyo wanaona ni bora "mwenye chongo katika jamii ya vipofu"
 
sawa tuu, mtawaita wananchi chongo, vipofu, lkn haitasaidia coz wanajielewa, uwezi kumdanganya mtu mwenye akili zake kuwa bomba la gesi linapita chini ya bahari linaenda kutokea ulaya, na akajua kuwa umemdanganya alafu akakupa kura!!!!!!
 
Habari wakuu,

Naomba wana-CHADEMA msiumize vichwa kuhusu huu ushindi wa CCM.Msidhani CCM inakubalika au inapendwa sana na wananchi.

Watanzania wataipenda CCM kwa vipi wakati kila siku wanalia na maisha magumu,ufisadi,mishahara midogo,bei za umeme,shida za maji,huduma mbovu za afya,ubovu wa miundo mbinu,migogoro ya wakulima na wafugaji,unyanyasaji wa polisi n.k

Wanachofanya watanzania kwa sasa ni kuchagua "mwenye chongo katika jamii ya vipofu awaongoze njia".Ndio maana watu wengi leo hii hawapigi kura kwani wamekata tamaa kabisa.Wasiopiga kura wengi wao ni wana CCM wanaona hakuna tena maana ya kuchagua viongozi.

Wapinzani kwa sasa mnachotakiwa ni kuonyesha kwa vitendo tofauti yenu na CCM.

Wapinzani,all you need to do is to walk the walk.

Mnapinga posho huku mnazichukua,mnapinga mashangingi wakati kiongozi wa kambi ya upinzani anatumia shangingi,mnaambiwa muungane hamtaki,vita ya madaraka katika vyama vya siasa hakuishii,boresheni na kujali viongozi na ofisi katika ngazi za chini hamtaki n.k

Wapinzani,wananchi bado wamewaweka katila "probation".

NB:Ingawa CCM ni wabovu,watanzania wengi wana hofu ya kufanya "majaribio" katika uongonzi wa nchi na hivyo wanaona ni bora "mwenye chongo katika jamii ya vipofu"

Kwa hiyo wapinzani ni vipofu na ccm ni chongo?
 
1.Chama hakiwezi kuimarishwa na mikutano ya hadhara tu.Je tujiulize tangu movement M4C na sasa M4C Pamoja daima,zimetumika shilingi ngapi na je chama kimepata wanachama wangapi wapya,mashina mangapi ya vyama yamejengwa?Wanaweza kuhubiri sana majukwaani kumbe wote ni mashabiki na sii wanachama kwa hiyo kubadilishwa ni rahisi (2) Je kuna succession plan ipi iliyopo?Kuna vijana makini wa kukiongoza chama? (3)Je mashabiki wengi wa chadema ni wapiga kura?Au wanaishia kwenye mikutano lakini kwenye kupiga kura hawana vigezo?
 
Mkuu Ngalikivembu pole sana, kwani wewe unaishi wapi???? Mbona chadema imeendelea kuongeza viti kwa kuvinyang'anya toka ccm??? Ok laskini pia hebu chunguza na uone kote tulikoshinda chadema ni kwa maumivu na vipigo tulivyopata kwa kulind kura zetu na sio vinginevyo, uchaguzi wote huu na kama kila mahali kungelindwa kwa vipigo na maumivu kama hayo hakika matokeo yangekuwa ccm 3, nccr 1 na chadema 23 bali ni sehemu chache zenye wabunge na watu jasiri kama kamanda lemma tu ndio tunapata ushindi na hakuna mahali ulinzi wa kura ulipoimarishwa na tukashindwaaaaaaa.

Ukweli ni kwamba kule tumeshindwa ni kwa nguvu za policcm, serikali, na tume yao ya uchaguzi, lakini ndani ya mioyo ya umma wa watanzania tumeshinda na tutashinda..................twende kazi mkuu tuko vyema.

ukiijifanya unalinda kumbe unaleta fujo nakutandika kisawasawa
we ulinde kula umekuwa kalani?
hao makalani mnaowaweka wana kazi gani,fanya fujo uchapwe ulishaona mtu anaetulia anachapwa sasa tutawachapa sana mkituzarau
 
Last edited by a moderator:
mtakumbuka shuka kunakucha, dawa huwa sio kuchukua radical dismissals kwa kisingizio cha wasaliti Bwana. Msemaji alisema "even the dull and the ignorant (so as you perceive them) they to have their stories" muhimu kutokudharau maoni ya mtu alimradi kakupinga nawe uko mahali pa juu. Basi yafanyieni kazi mapendekezo ya akina Kitila na Mwigamba japo hamnao tena acha ushabiki (fundamentalism) wa wasaliti wasaliti ndio mambo yaende mbele ndugu zanguni
 
Nchi hii ina kila kitu isipokuwa WATANZANIA tu!

Hivi kwa matatizo yote haya ambayo CCM imetusababishia,unaweza kupoteza muda wako kwenda kwenye kituo cha kupigia kura kuipigia CCM kura kweli?

Itanichukua miaka kuamini watanzania wanawapigia kura CCM....

CCM ni chama dola ina mbinu nyingi sana za kulazimisha ushindi....

Wanatengeneza mazingira ya kuonyesha wao wanapigiwa kura kumbe laa!

Kwamfano huko Arusha- Sombetini siamini kabisa hizo kura walizopata.

CCM wanahakikisha morale ta wapiga kura haipandi hata siku moja hivyo wapo tayari kwa lolote ilimradi isionekane kwa vitendo upinzani unakua...Hiki kinawahakikishia wao wanaendelea kumanipulate kura. Naamini siku CCM wakishindwa ku manipulate kura kwa njia zake zote watakuwatayari kuilinda dola yao kwa ncha ya upanga....kwa wengi wao wenye nguvu hawajui maisha nengine zaidi ua kuitumia dola kupata kila wanachokihitaji!
 
Kulikuwa na bwana mmoja aliyepewa jiwe kubwa sana ambalo aliambiwa akiliponda likapasuka vipande vipande,atapata dhahabu.Bwana huyu baada ya kuponda jiwe lile mara miamoja,alikata tamaa,akaghafirika na kutupa nyundo chini na kuondoka.Mwingine aliyekuja aliponda nyundo moja tu na jiwe lile likapasuka vipande vipande,hatua moja au mpondo mmoja ulimkosesha yule bwana dhahabu.

Ni kwamba,katika hatua yoyote ya maisha,hatuna budi kujua changamoto na matatizo ni njia ya kuelekea kwenye neema.Hakika mwisho wa kitu,kiwe kizuri au kibaya hauji upesi.Kazi ambayo imeshafanywa na Chadema ni kubwa.Wenye kukata tamaa na kile wanachoona kimefanyika au na matokeo yaliyotangazwa,ni watu wabaya sana.Si watu wema,hawajui uchungu wa mapambano.Wengi wetu tunafanya maamuzi nyuma ya keyboards zetu,na kamwe hatuna uthubutu wa kujua kiwango cha mapambano.

Uchaguzi huu ukipimwa kwa mizania ya kisayansi,ni ukweli usiopingika kuwa Chadema ndio washindi and CCM stand loosers!! Bilioni moja ukiondoa shilingi moja si bilioni tena,tutaiita bilioni moja kasoro,Shilingi mbili ukiongeza Sh moja,pesa hiyo inakuwa imeongezeka.Katika hili CCM wakati wanatafakari kuzipoteza kata zao,CDM hawatafakari maumivu wanatafakari kwanini hawakuongeza zaidi.Haya ni mambo mawili tofauti.

Katika uhalisia wa mambo unavyokwenda,haya si matokeo ya chama chochote kujitapa,ni kujitafakari na kuchukua hatua.Niliwahi kuandika hapa jamvini,kuwa bila ya chadema kufanya decentralization,hali itaendelea kuwa hivi hivi.Nakumbuka huko kwetu kuna kijiji ambacho hata gari hawajawahi kuliona na mpaka sasa wanajua rais ni nyerere.Lakini mfumo wa uongozi ulio katika kijiji kile umejikita mizizi sana.Haiwezekani CDM mtake kila kijiji na matawi yote yamjue Dr.Slaa na Mbowe.Hebu vifanye vijiji,matawi na mashina yawe na imani na uongozi wa mahali pale.Wape uwezo hawa viongozi wa chini,wanyweshe majina ya bendera kama CCM walivyofanya.Nina babu yangu mpaka leo ukimwambia kwanini unaipenda CCM hana zaidi ya kusema kuwa ni kwa sababu ilileta uhuru.Hakuna cha ziada walichonacho watu juu ya ccm,haiwezekani mindset ya watu ikabadilika kwa chopa inayotua kwa masaa kadhaa,lazima mabadiliko yafanywe.

CDM punguzeni centralization,decentralize the party na nguvu ya umma inayohubiriwa ionekane.

Ni hayo tu!

mkuu, naona umetunga santuri nzuuuri kweli kwel ya kujaribu kujifariji lakini kiuhalisia bado haiondoi ukwel kwamba CDM imeboronga vibaya ktk uchaguzi wa jana ikilinganishwa na nguvu kubwa iliyotumika.
mie nakwenda mbali zaidi ktk kusaka ufumbuzi - tumn'goe kiongozi mkuu ndani ya chama na kusimika mawazo mapya, huyu wa sasa mbali ya kuzongwa na uchafu kibao, zaidi imethibitika hana jipya!!
chadema tuna hazina ya viongozi wazuri zaidi - tubadili safu ya uongozi vinginevyo kuwatoa maccm itakuwa ni ndoto!!
 
Back
Top Bottom