Tathmini: Matokeo ya Uchaguzi wa Udiwani uliofanyika Februari 9, 2014

CCM haina uwezo wa kuwabana watendaji Wazembe.Mtu anayelipwa Mshahara chini ya Tshs.200,000/=kwa Mwezi sawa na Dola 15 atawezaje kufanya kazi kwa ufanisi kama sio kugeuza Ofisi ya Serikali kuwa Sehemu ya Kupigia Dili zake.
We mburula nani analipwa hiyo hela weka majina hapa na viambatisho.
 
We mburula nani analipwa hiyo hela weka majina hapa na viambatisho.

Unaitetea CCM kila siku,Kumbu hujui hata Kima cha Chini wanacholipwa Wafanyakazi wa Serikali inayoongozwa na CCM hakifiki Tshs 200,000/= kwa Mwezi?.Ni wenye uelewa mdogo tu kama wewe wanaoishabikia CCM.
 
BAO LA kisigino!!Kuna matatizo 7 ambayo CHADEMA bado hawayafahamu:

1. Hawajui priority ya matatizo ya watanzania

2. M4C imekuwa na propaganda zaidi kuliko kuwa na idiolojia ya kudumu juu ya kile kinacholenga kutatua matatizo ya watanzania. Hivyo imekipaka matope zaidi chama kuliko kukijenga, kwani watanzania wanaona kama mchezo wa kuigiza. Na ndio maana Zitto hakushabikia wala kushiriki katika M4C.

3. CHADEMA wanadhani watanzania ni WAJINGA/MAJINGA ya kudanganya danganya tu. Hili ni kosa kubwa.

4. Ukabila na Udini

5. Kutoelewa DEMOKRASIA. (Hili ni tatizo kubwa sana, halitatuliwa leo wala kesho). Kwa maana hiyo kuwapendekeza wagombea wasionamvuta kwa wananchi. Hii ni pamoja na uchaguzi wa ndani ya chama na nje(udiwani/ubunge) hata uwakilishi mbali mbali.

6. Mgao wa Ruzuku.

7. Kudhani kuwa Fujo, mapigano, vurugu ndio siasa zinazohitajika Tanzania. Wakati mwingine wakisema hadharani kuwa watanzania ni WAOGA.

Na kwa hayo, ndio sababu kubwa ya wananchi kutojitokeza katika kupiga kura. Kwani walikuwa na imani sana na CHADEMA, na imewafikisha pabaya na wala hawanahaja na CCM. Hawa wamechagua kususia uchaguzi.

! Matokeo haya ni taswira tosha juu ya uchaguzi mkuu 2015. Awe Slaa, Mbowe , pindi wataposhindwa wasizingizie kuwa wamepigwa bao, bali hiyo ndio itakuwa hali halisi. Tena mgombea wa urais wa CHADEMA akipata 10% ashukuru Mungu
 
CHADEMA adui yao ni ubabe walionao viongozi Wa juu. Also hawa jamaa ni wabaguzi sn ,for sure we won't move!
 
Niliwashauri sana CHADEMA, siku watakayokubali kuacha ukabila na udini watasonga mbele! Vinginevyo wataendelea kuambulia KIBORLONI tu!
 
Vipi na hizo kata chadema walizoshinda daftafi la wapiga kura zilirekebishwa? ?

Bk 7 wengi wanauliza ili swali bila kujiuliza ushindi huo unapatikanaje. Hawaoni nguvu ya polisi inayotumika na ujasiri wa vijana ktk ulinzi wa kura. Hawaangalii matukio kabla ya uchaguzi huo yanamalengo gani na kwa nini yatokee.

Kujifanya vipofu wa matukio haya kutalipeleka taifa pabaya.
 
Wakuu,

Hivi hoja ya CDM kuwa vijana wengi hawajajiandikisha inamantiki? Hivi vijana wote wanafikiri wanakishabikia CDM pekee? Wanadhani vyama vingine hawana vijana wanaosubiri kuandikishwa? Hii ni fikra mfu, na kwa hakika daftari la wapiga kura likiboreshwa litawanufaisha zaidi CCM kuliko CDM!

Na huo ndio utakuwa mwisho wenu! Endeleeni kutumia viongozi toka makao makuu ndio tatizo kubwa kwa CDM na siyo daftari! Jengeni chama kiaminike na wazalendo toka Maeneo husika na siyo Dr Slaa na Mbowe
 
Labda mimi hapa niko nyuma kidogo...utafanyaje tathmini bila kuangalia haya katika kata hizo 27;

  1. Idadi ya waliojiandikisha kupiga kura mwaka 2010, waliopiga kura na kura halali ikilinganishwa na mwaka huu.
  2. Matokeo ya Chaguzi hizo kwa kila chama mwaka 2010 ikilinganishwa na mwaka huu.
Kwa kuwa Kata zenyewe ni 27 tu, sidhani kama ni kazi ngumu kupata hizo takwimu na kwa ninavyoijua mtandao wa JF nashangaa hadi sasa hajajitokeza mtu kutoa hizo takwimu lakini hapo hapo wanatokea watu eti wanatoa tathmini, based on what? Kama ni idadi ya madiwani, imebaki ile ile ya mwaka 2010, sasa swali langu ni hivi; kama kata ni zile zile, waliotegemewa kupiga kura kulingana na daftari ni wale wale, wasimamizi ni wale wale na mazingira ni yale yale, kwa nini matokeo yatushangaze? Kama namba ya madiwani imebaki ile ile kwa kila chama, tathmini hii ni ya nini?
 
Hii inanikumbusha wakati niko chuo na huu msemo...."msuli tembo matokeo sisimizi"...chopa tatu kata tatu...lol
 
miaka yote CHADEMA wanakuwa wanafuatia kwa karibu hivyo hivyo wala wasifikiri kuna improvement yoyote.
Mkuu watoa maoni wote hawaelezi tatizo la Tume ya uchaguzi kuwaachia viongozi wa serilkali na ccm kuendesha chaguzi katika kata na jimbo isipokuwa Said Kubenea.Katika mazingira ya sasa ccm ndio wanao simamia uchaguzi na kutangaza matokeo.Kimsingi wakiamua mnaweza msishinde hata kata moja.
 
Sijaona kama Chadema imepoteza kwenye huu uchaguzi, naona kuna wahuni mnapigapiga kelele tu humu, elezeni basi watu waelewe imepoteza vipi kwa haya matokeo.
 
Chadema tafakarini sana!Mna kazi nzito sana kuing'oa sisiemu,acheni maneno ya kujifariji mbivu na mbichi zimeonekana katika uchaguzi huu mdogo.Why ushindi ni Kilimanjaro na Arusha tuu kwa asilimia kubwa?

Watu wa jinsi kama ninyi ndiyo wanaochangia CCM kuwa na kiburi.... Hivi ww unadhani hao unaowanyooshea kidole wana hasara gani hata CCM ikitawala milele? Let say kila mmoja aamue kukubali maneno mnayolishwa oooh CDM ni NGO or chama cha watu wa kanda fulani wakashusha mikono yao chini na kuamua kupigania nafasi za majimbo yao tu kati yetu sisi ambao mshahara ni siku ya 40 ya mwezi huku PAYE ikiendelea kujaza mafuta ya hao wala nchi, kuwawashia viyoyozi maofisini kwao, kununua V8 zao na kwenda an informal tour abroad nani mwenye hasara?

Wengine family relation zetu ziko at stake tukiwafikirini watu kama ninyi msio na shukrani wala soni ya maisha dhalili huku tukizungukwa na rasilimali then badala ya kuwaunga mkono mko hand closed na maneno kebekebe kwa hawa watu wachache waliojitoa mhanga!


Mheshimiwa Mbowe kilichobaki nadhani tengeneza pension yako maana miaka zaidi ya ishirini uliyo invest inatosha kabisa kwa hawa watanzania wasio jitambua maana kesho ukidhalilika wengine hata mate watakutemea acha maisha yawapige sawasawa ndiyo watatia akili..!
 
Mkuu watoa maoni wote hawaelezi tatizo la Tume ya uchaguzi kuwaachia viongozi wa serilkali na ccm kuendesha chaguzi katika kata na jimbo isipokuwa Said Kubenea.Katika mazingira ya sasa ccm ndio wanao simamia uchaguzi na kutangaza matokeo.Kimsingi wakiamua mnaweza msishinde hata kata moja.

Tatizo la watanzania ni slavery mind.... Wamekuwa oppressed kwa muda mrefu mpaka subconscious imekubali kuwa they are worthy of such kind of life!

Kuliko uwe mind slave bora uwe na kilema kingine chochote! Ndiyo tunachokipata hata wa Africa wote dhidi ya wazungu!

Mimi nilikataa huo utumwa na nimeyaishi hayo maisha from when was kinder todate.... Nipo tayari kufa kuliko mtu kuikalia mind yangu....
 
Chadema tafakarini sana!Mna kazi nzito sana kuing'oa sisiemu,acheni maneno ya kujifariji mbivu na mbichi zimeonekana katika uchaguzi huu mdogo.Why ushindi ni Kilimanjaro na Arusha tuu kwa asilimia kubwa?

Ushindi ni knjaro na Arusha sababu ni Chagga Development Manifest.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom