S.Liondo
JF-Expert Member
- Apr 20, 2011
- 3,408
- 1,712
Mkuu naamini hoja yako. Na pia nimeona mojawapo ya marungu ambayo ccm inafaidika nayo kwa sasa ni Daftari la wapiga kura kutoboreshwa. Ninaamini kuna vijana wengi sana waliokuwa na umri kati ya miaka 15-17 wakati wa uandikishwaji wa mara ya mwisho ambao leo wangeweza kupiga kura lakini hawana nafasi hiyo. Ni kweli watajazana kwenye mikutano ya chadema na hata kushangilia kwa hamasa lakini wakati wa kutumia sanduku la kura kutimiza haki yao nafasi hiyo hawana. Daftari la wapiga kura sio Rungu pekee lakini ni mojawapo ya mengi ambayo CCM wanayo. Kibinafsi nimechoka na utawala wa CCM na ninatamani mabadiliko.Hivi kweli mkuu unaamini ccm wanaweza kushiriki uchaguzi bila ujanja wowote?Hivi uingie kwenye mtihani ambao majibu unatunza mwenyewe na kusahihisha unasahihisha wewe na matokeo unatangaza wewe, halafu ujipe F.Inawezekana?