Si busara sana kulalamika kwa mapungufu yaliyojitokeza katika tukio la leo na si vibaya kupongeza na kudumisha yote mazuri katika tukio hili hapo SERENA HOTEL.
Nini Tathmini yako Mpenda mbadiliko na nini kifanyike siku zijazo?
Sikufuatilia yaliyotokea Arusha katika M4C Fundraising ya kwanza. Lakini naamini tukio la jana lingeweza kujifunza chochote toka kule.
Kwa upande wa ushauri,naona mengi yamesemwa na wadau, ila nitaongeza kidogo katika hayo:
1. Umuhimu wa kuandaa shughuli kwa umakini,kuwa na ratiba inayoeleweka, ratiba ambayo itaonyesha juu ya tukio fulani,msemaji wa tukio hilo,muda wa tukio hilo na washiriki wa tukio hilo. Kuwa na mshehereshaji anayefahamu dhumuni la shughuli. Mshehereshaji apewe kabisa ToR mapema,ili aweze kufanya kazi yake ipaswavyo.
2. Umuhimu wa uongozi wa M4C kutoa taarifa za mapato na matumizi ya pesa,si katika magazeti ila katika vikao husika vya chama. Wanaweza kutoa kwenye vyombo vya habari kama wakiona ni sawa kufanya hivyo. Hii itatoa moyo kwa wachingiaji tarajiwa kuona namna ambavyo pesa zao zinaweza kutumika na kuthaminiwa.
3. Kutoa mapema ratiba za M4C Fundraising. Kama sasa uongozi wa M4C unapaswa kusema mahala pengine ambako fundraising itafanyika. Tena ingekuwa vyema,uongozi uandae ratiba ya muda mrefu wa M4C Fundraising,kama almanac vile. Ili ifahamike kabisa,nini kitafanyika,wapi kitafanyika na lini kitafanyika. Hili litasaidia pia katika kufanikisha zaidi zoezi zima la uchangishaji.
Zaidi ya yote,hongereni M4C Dar kwa kufanikisha shughuli. Hongereni wana DSM kwa kukubali kujitoa kwa ajili ya kuchangia msingi wa mabadiliko.