Dr. Ngwazi
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 723
- 289
Pamoja na kutoshinda kwa Ndugu Edward Ngoyai Lowassa, bado kuna haja ya kufahamu kuwa Lowassa amemzidi na kumfunika Dr. Slaa aliyegombea mwaka 2010 kupitia CHADEMA. Mwaka 2010, kura zilizopigwa zilikuwa 8,398,394 na Dr. Slaa alipata kura milioni 2.2 ambazo ni sawa na asilimia 26.34 ya kura zote. Mwaka huu, zilipigwa kura 15,193,863 na Lowassa kupata kura milioni 6 na ushee sawa na asilimia 39.97.
Mshindi wa mwaka 2010,Rais Kikwete alipata asilimia 61 na wa mwaka huu amepata asilimia 58.46. Ukitazama kwa jicho kali, utaona na kujua kuwa Lowassa amemzidi kwa mbali sana Dr. Slaa. Pia, CCM imeendelea kupungua kwa asilimia za kura zake. Ni wazi sasa kuwa, Lowassa ameongeza hta majimbo ya uchaguzi kwa CHADEMA na CUF pamoja na vyama hivyo kupoteza baadhi ya majimbo yao.
Lowassa amesaidia kupoka ngome mbalimbali za CCM na kuzikabidhi CHADEMA na CUF. Mwaka huu, kwa uwiano wa kura za wagombea wa Urais wa Tanzania, CHADEMA itapata nafasi za viti maalum kwa wingi zaidi na kutoachwa mbali na CCM kama ilivyokuwa mwaka 2010. Haya pia ni mafanikio yaliyoletwa na Lowassa huko CHADEMA na kumzidi kwa mbali Dr. Slaa wa mwaka 2010. CHADEMA ilicheza karata zake vyema.
Kila la kheri watanzania!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Mzee tupatupa, kuna mahali padogo tu umesahau. Mwaka 2010 Dr. Slaa alipata 27 point somethimg percent, lakini kumbuka wakati ule alisimama peke yake sio kama ilivyokuwa kwa lowassa mwaka huu Lowassa amechukua kura za vyama vinne. prof Lipumba naye alikuwa na asilimia zake kupitia CUF 2010 na Hashim Sipunda naye alikuwa na asilimia zake kupitia NCCR. Ukichanganya za hao wote mwaka 2010 utapata ukweli na hesabu halisi iliyoongezeka kwa lowassa. Lakini vilevile usisahau za NLD.
Lakini kumbuka watu walianza kuiona chadema imeanza kuonyesha upinzani wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014. na hii nayo hujaiweka kwenye tathimini yako, ukifanya mahesabu sahihi, utagundua kwamba Lowassa amevuruga mwenendo mzuri wa chadema uliokuwepo na hakuna alichoongeza