Tathimini ya Leo, Lowassa V/S Magufuli

Tathimini ya Leo, Lowassa V/S Magufuli

inols

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2010
Posts
283
Reaction score
98
Katika vijiwe kumi nilivyotembelea leo kuanzia Lumumba hadi Ofisi za NEC. Vijiwe nane vilikuwa vinamuongelea Lowassa wakati wanaCCM wako kwenye harakati za kuchukua fomu ya Urais.

Vijiwe viwili ambavyo vilikuwa na wavaaji nguo za kijani, wengine boxers zao ni za CCM walijisahau na kujikuta wanaongelea Lowassa mazungumzo yao yote, vilevile walionyesha dhahiri pasipo shaka kukosa amani na raha kabisa kwa mamvi kubadili kambi.

Kwa hiyo basi kwa hali ya sasa ilivyo, ni vizuri UKAWA washughulike na hawa undecided voters, na wale wanaojifanya Ccm damu, kumbe ndani ya mioyo yao, wako msibani wa kumpoteza Lowassa.
 
Hiyo pia ni mbinu nzuri ya kupata pich. Muhimu ni jinsi ulivyokuwa unachagua vijiwe ulivyovishirikisha kwenye utafiti. Kama hukuwa na upendeleo hasa wa kukwepa vijiwe vya wafi bendera ya kijani basi matokeo yako yapo karibu na ukweli
 
Ungeuliza hao mateja wa vijiweni kama wa kadi za kupigia kura...zumbukuku we
 
tukutane oktoba ndio kuna majibu ya kweli.
 
Kumbe umetembelea vijiweni! Watu wenye akili timamu wanashinda vijiweni?
 
Magufuli ni housegirl. Bomba sana kufuata maagizo ya mwanaume mwenye mji wake. Urais ni maji marefu kwake. Lowasa haangalii makunyanzi, ni baba la mbegu. Isitoshe magufuli yupo Choo cha kike. Sisiem ni majambazi yasiyotakiwa kuanzia Oktoba. Ni sawa na Choo cha kike kisichokubali wadindishaji. Lakini Choo cha kiume, aaah, ni cha kila mtu mradi unajiamini na upo tayari kwa lolote.
 
USHAURI WA BURE KWA CHADEMA.

Mfanyieni rehearsal ya kutosha Edward Lowasa ili aendane na falsafa ya chama na salamu ya chama.

Pili muambieni CHADEMA sio chama tawala hivyo ili wananchi wamuelewe awaeleze maovu ya serikali ya CCM na asilete mambo ya ustaarabu wa CCM kwa CHADEMA.

Ikumbukwe CCM huwa inashinda sio kwa ustaarabu wa kampeni bali kwa wingi wa wanachama na hila za uchaguzi. Na ajue kuwa CHADEMA imekuwa ikiendelea kukua sio kwa ustaarabu wa kampeni bali kwa kufichua maovu ya watawala.

Hivyo mfundisheni kuendana na organization culture ya CHADEMA na ajitambue kuwa sasa yupo upinzani hata kama sio kwa hiari yake.

Nawasilisha
 
Jukwaa hili ni vyema tukajenga hoja badala ya kutukana na kukejeli.Mleta hoja anasema kafanya rough or random survey ktk eneo fulani na kupata majibu fulani.Mtu mwingine anakuja kutukana.Kweli Bongo tunayo safari ndefu sana.
 
Back
Top Bottom