TARURA, Mradi wa TACTIC Kuanza Mwezi Agasti Baada ya WB Kutoa Mkopo Wa Dola Milioni 410

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,119
49,840
TARURA imesema Mradi wa kuboresha Miji yaani TACTIC unatarajia kuanza kutekeleza mwezi Agosti mwaka huu wa 2023 baada ya Benki ya Dunia kutoa Mkopo wa masharti nafuu Kwa Serikali wenye thamani ya dola milioni 410 sawa na shs.Bil.950.

Hayo yameelezwa wakati wajumbe wa sabuni wakikutana Tanga Kwa Ajili ya kuainisha Wakandarasi watakaotekeleza mradi..
===

Uboreshaji wa Miundombinu katika miji 12 kati 45 ambayo inanufaika na mradi wa TACTIC unatarajiwa kuanza Agosti, 2023 kufuatia Benki ya Dunia (WB) kuridhia kutoa Dola za Kimarekani milioni 410 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Hayo yamebainishwa wakati Wajumbe wa Bodi za Zabuni za halmashauri 12 mkoani Tanga ambazo ziko katika awamu ya kwanza ya mradi huo kukutana kujadiliana na kupewa mafunzo kuhusu utekelezaji wake.

Mratibu Msaidizi wa Miradi ya TACTIC, Mhandisi Emmanuel Manyanga amesema mradi unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kupitia mkopo wa masharti nafuu wa benki ya dunia.

“Mwezi Julai wasimamizi wataingia katika maeneo ya miradi kwa ajili ya kupata takwimu za awali na mwezi wa Agosti wakandarasi wataingia na kuanza ujenzi kwa awamu hiyo,” amesema Manyanga.

Pia, Manyanga amesema mradi huo unaratibiwa na Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) na kutekelezwa na Halmashauri za Miji 45 nchini.

Manyanga amesema Miji hiyo imegawanywa katika makundi matatu. Kundi la kwanza litakaloanza mradi huo linahusisha miji 12 ambayo ni Arusha, Dodoma, Geita, Ilemela, Kahama, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Songea, Sumbawanga na Tabora.

Kundi la pili ni lenye miji 15 ambayo ni Babati, Bariadi, Bukoba, Iringa, Kibaha, Korogwe, Lindi, Moshi, Mpanda, Mtwara, Musoma, Njombe, Singida, Shinyanga na Tanga,” alisema Manyaga.

Bagamoyo, Bunda, Chato, Handeni, Ifakara, Kasulu, Kondoa, Mafinga, Makambako, Masasi, Mbinga, Mbulu, Nanyamba, Newala, Nzega, Tunduma, Tarime na Vwawa ni miji 18 ilipo katika kundi la tatu.

“Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kuanza kwa utekelezaji wa miradi hii ya TACTIC ambayo imesambaa karibu nchi nzima yenye lengo la kuboresha miundombinu ya miji na kuzijengea uwezo halmashauri ambazo zitatekeleza miradi hii,” alisema.

Amesema wameanza utekelezaji baada ya kutimiza matakwa yote ambayo walipewa na benki ya Dunia huku akisema kuwa awamu ya kwanza usanifu umeshakamilika na zabuni zimeshatangazwa na sasa wako katika hatua za mwisho kupata wakandarasi.
 
Dar mbona hatupo kwenye hii list? Na sisi huku kwetu ati tuliambiwa tusubiri awamu ya pili lakini hapa tumepigwa kavu kavu!
Halmashauri/manispaa za Dar zinakusanya pesa nyingi sana,wanaweza wakajenga hizo barabara za mitaani, maji, kupanda miti na bustani etc bila matatizo ila tatizo madiwani wenu na Meya ni wezi na wajinga kiwango cha SGR
 
Back
Top Bottom