Yanayojiri: Uzinduzi Mradi wa TACTIC awamu ya pili Desemba 15, 2023

Uchumi TV

Member
Apr 11, 2023
14
19
Leo Desemba 15, 2023 kuna Hafla ya Utiaji Saini Mikataba ya Usanifu wa Miradi ya Uboreshaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) Kwa Miji 15 ya Kundi la Pili (Tier 2) itakayofanyika Mjini Bukoba Mkoani Kagera.

Miji itakayotekeleza TACTIC Awamu ya Pili ni; Babati, Iringa, Bukoba, Bariadi, Kibaha, Korogwe, Lindi, Moshi, Mpanda, Mtwara, Musoma, Njombe, Singida, Shinyanga, Tanga,

Kikundi-kazi cha Utekelezaji wa Miradi inayotekelezwa kwa Ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na Benki ya Dunia kupitia TARURA kimetembelea maeneo ya miradi itakayotekelezwa Mjini Bukoba.

Miradi itakayotekelezwa Bukoba ni Ujenzi wa Stendi Mpya ya Kisasa Kyakailabwa, Barabara za Lami Kilomita (7),ufungaji wa taa za umeme wa jua, Ujenzi wa Soko kubwa la kisasa na Ujenzi wa Mto Kanoni wenye urefu wa KM 7.3.

Uzinduzi huo utafanywa na timu ya wataalam kwa ugeni wa Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa.

Tutakupatia updates ya kinachojiri.
 
Miji itakyotekeleza TACTIC awamu ya 3 ni Bagamoyo, Bunda, Chato, Handeni, Ifakara, Kasulu, Kondoa , Mafinga, Makambako, Masasi, Mbinga, Mbulu, Nanyamba, Nzega, Newala, Tunduma na Tarime
 
Back
Top Bottom