Tarime Wanaandaa Maandamano

Tarime Wanaandaa Maandamano

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2009
Posts
3,444
Reaction score
265
Habari nilizozipata hivi punde toka Tarime mjini ni kwamba, kuna ujumbe wa SMS unaosambazwa kuwahimiza wananchi kuamka na kuanza ukombozi. Wamepanga maandamano Alhamisi inayokuja na Ujumbe niliotumiwa unasomeka hivi

"CCM CHADEMA Tarime ni yetu. Alhamisi tunakutana Buhemba saa 3. Sasa CCM na polisi watuue wote, tumechoka na unyanyasaji wao na umaskini. Barik Gold na Mchina wakachimbe dhaabu bagamoyo"
 
Kama ni kweli watatia kichwani akili na kutekeleza mahitaji ya watu badala ya siasa na propaganda majukwaani
 
Mkwara bata huo, wao kwa wao kutwa kucha kuchinjana wana muda wa kuandamana?
 
Kama ni kweli, basi ni hatari, ingawa lisemwalo lipo. mambo haya yasipo patiwa ufumbuzi, nchi tunakwenda kubaya. kwa busara za mkuu wa kaya, iko haja ya kufanya marekebisho ndani ya vyombo vya dola, ili kuleta mwafaka kwa raia. kama mkuu wa kaya hajaliona hilo, basi kuna hatari hapo magogoni.
 
Naona huu mwaka umeanza kwa kwa kasi zaidi, nguvu zaidi na ari zaidi
 
saa+ya.JPG
Habari nilizozipata hivi punde toka Tarime mjini ni kwamba, kuna ujumbe wa SMS unaosambazwa kuwahimiza wananchi kuamka na kuanza ukombozi. Wamepanga maandamano Alhamisi inayokuja na Ujumbe niliotumiwa unasomeka hivi
 
kinachosikitisha hapa sio haya matokeo ya fujo na uaribufu wa mali za watu, bali watu wanakuja na vitisho vya wazi serikali badala ya kujipanga mapema na kuwa tayari ku-deal na any circumstances if things ever spiral out of control. wao bado wanachukulia upepo, tusipoangalia soon hizi ghasia zitatuingiza kwenye state emergency na jeshi lije kutoa kibano.

I mean we are not dealing with armed rebels it is just Tanzanians for the first time may be in our history are beginning to question their rights, the method untested yet within but surely they must be contained. Ni vitu vya kawaida sana hata nchi zenye liberal democracy haya mambo kutokea, wao wameshajifunza not to take chances with may-day marches or on G8 summits protests. Tatizo ni wahusika kufanya vitu kimzaa, kwengine duniani hao hawasumbui hawana silaha na jeshi na polisi bado wapo upande wa serikali ni mkwara heavy arudi mtu.

Mwisho wa siku viongozi wakubali their days as mafisadi without being challenged or questioned are numbered, people can longer tolerate poverty and left ignored by their government.
 
waswahili husema ukicheza na ngedere utavuna mabua. Haya ndo matokeo ya kuzichekea fujo na vurugu zinazofanywa na wanamtwara. Next time tutasikia mikoa ya kusini nayo imezuia mahindi yao yasitoke hadi Azam akajenge kiwanda cha kusindika sembe kule. Mwisho wa siku nchi itakuwa vipande vipande. Kama vipi tukubaliane na sera ya majimbo ya CHADEMA ili tuishi kwa amani. Though wasi wasi wangu ni kwamba mikoa iliyobarikiwa kuwa na rasilimali nyingi zaid itakuwa na advantage kuliko ile ilyo mikame kama vile Sindida na Dodoma.
 
dodoma rasilimali yetu ni wabunge....full kwenda kuomba mjengoni...kila mwaka wataongeza posho za wabunge ili nasi tunufaike!
 
waswahili husema ukicheza na ngedere utavuna mabua. Haya ndo matokeo ya kuzichekea fujo na vurugu zinazofanywa na wanamtwara. Next time tutasikia mikoa ya kusini nayo imezuia mahindi yao yasitoke hadi Azam akajenge kiwanda cha kusindika sembe kule. Mwisho wa siku nchi itakuwa vipande vipande. Kama vipi tukubaliane na sera ya majimbo ya CHADEMA ili tuishi kwa amani. Though wasi wasi wangu ni kwamba mikoa iliyobarikiwa kuwa na rasilimali nyingi zaid itakuwa na advantage kuliko ile ilyo mikame kama vile Sindida na Dodoma.

Sera ya majimbo aitosaidia rasimali za taifa kutumiwa sawa labda mikoa wajitoe tanzania na waweke sera zao za ujamaa, but if the central government still has a role of drawing up national policies and keep embracing the current mixed economy policies, wenye pesa watawekeza wanavyotaka wao na kwa kuzingatia business strategy zao na huwezo wao.

Kama kungekuwa na soko la unga wake huko kusini huyo baresa sidhani kama angefikiria mara mbili kwanza it would have been cheaper kwake kufungua kiwanda na kuokoa gharama za usafirishaji, considering many only live their lives hands to mouth huko kusini it is waste of money to open up a plant in those areas and same applies as building up a power plant in Mtwara, whereby the infrastructure in Dar es Salaam is ready and capable of accommodating the new transformation of production at the cheapest cost.

Watu wanafanya vitu kwa mipango na realistic returns on their investment na si porojo na kuongopeana, hizo sera za majimbo zitawapa watu hela za kuinvest au itamzuia mchaga mwenye hela zake kuacha kwenda kuchukua bidhaa mkoa fulani kwa biasharaa zake. How is this supposed to help the local communities embu toteleeni pumba hapa.
 
...WEWE ni...Mbunge wa lumumba ..au .ni Mbunge wa wanainchi......

.Chagua moja TUKUELEWE!!!!

sasa mtajua maana ya ubunge..kwenda kuwakilisha tumbo lako au kuwakilisha walio kuajiri....

Kwa sasa wabunge wa Magamba wenye mlengo wa Lumumba ..matumbo joto!!!!!

VIJANA WAMECHACHAMAAAAA CHA!!!
 
Habari nilizozipata hivi punde toka Tarime mjini ni kwamba, kuna ujumbe wa SMS unaosambazwa kuwahimiza wananchi kuamka na kuanza ukombozi. Wamepanga maandamano Alhamisi inayokuja na Ujumbe niliotumiwa unasomeka hivi

Huu ni uchochezi wa Chadema kutaka Nchi isitawalike kama walivyosema awali, mimi nafikiri mganga wao kawadanganya sana kwani kila kukicha wanahamasisha maandamano na madhara yake Watanzania wasio kuwa na hatia wanakufa. Tarime na Buhemba ni Wilaya mbili tofauti na zipo mbali mbali, je mtoa maada anatuhadaa yeye akiwa Dar sisi tuumie huku wao wanagawana pesa?. Wakurya huwa hatudanganyiki na ndo maana tukiamua kufanya kitu tunatenda kweli bila kuogopa. Acheni uchuro wenu wa kutuchonganisha tuanzekupigana tena.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom