BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Tarime kuna tatizo na tatizo si CHADEMA, ni Barrick
TATIZO la Tarime si CHADEMA. Naam, lipo tatizo Tarime na ni tatizo la muda mrefu sana kwa yeyote mwenye kufuatilia historia ya eneo hilo. CHADEMA na CCM wanafunua tatizo ambalo lipo hapo, na kwa kadri ya kwamba watu wanafikiria tatizo hili ni la kisiasa ndivyo ambavyo tatizo hili litaendelea kuchukua mwanga wa kisiasa.
Tatizo la CHADEMA linahusiana kwanza kabisa na raslimali za watu. Huwezi kuwa na matajiri wanaonufaika na raslimali; huku wakiwa wamezungukwa na maskini ambao wanashindwa kupata nafasi ya kutumia raslimali hizo.
Kwa muda mrefu kumekuwa na matatizo kuanzia ya kutumia maji ya mto na sasa zaidi kutumia ardhi kama sehemu ya kujipatia maisha yao. Wananchi wa Tarime wanajikuta wanasukumizwa pembezoni mwa mafanikio.
Mgongano kati ya wachimba madini wadogowadogo na kampuni kubwa ya madini ya Barrick haujaanza leo na haujaanzia Tanzania tu. Kuna kitu ambacho hakiko sawa kati ya mahusiano kati ya kampuni hiyo ya Canada na wananchi ambao wanaishi karibu na machimbo yake.
Mapema mwaka huu, Barrick wamejikuta kwenye matatizo huko Papua New Guinea na tayari walishakuwa na migogoro huko Chile na hata Marekani kwenyewe. Matatizo haya yanahitaji kuangaliwa kwa karibu; kwani bila kuyashughulikia mgongano huu utaendelea na siyo Tarime peke yake lakini sehemu nyingine nchini.
Maafa yaliyotokea hayakupaswa kutokea na tusipoangalia yataaendelea kujitokeza tena na tena. Jambo ambalo linaonekana ni la hatari zaidi ni kuwa kuna kasumba ya kuwaona Watanzania ni waleta matatizo na katika jitihada ya kuwafurahisha wawekezaji, basi, tuko tayari kufanya lolote kwa hawa Watanzania wenzetu ili wawekezaji wasije wakasita kuwekeza nchini.
Kwa sababu hiyo, juhudi kubwa inatumiwa na vyombo vya dola na hata viongozi wa kitaifa kuhakikisha kuwa mikataba ya madini ina vipengele vinavyoweka jukumu la serikali kushughulikia wananchi wake ili wachimbaji wafanye kazi kwa amani.
Matokeo yake ni kuwa mahali popote ambapo madini yatagunduliwa na leseni kutolewa kwa kampuni ya kimataifa, serikali itatakiwa kufanya lolote linalowezekana kuwaondoa wananchi pale ili makampuni hayo yafanikiwe.
Kwa kufanya hivyo, japo jambo hilo linaonekana ni dogo lakini halizingatii hisia za watu kwenye ardhi yao. Watanzania kama binadamu wengine wanaamini wana haki katika ardhi yao; kwani ndio mahali pekee katika sayari hii ya dunia ambapo kwa haki kabisa wanapaswa kupata maisha yao.
Hatari yake ni kuwa Serikali ya CCM inaendeleza hizi fikra za kuwafurahisha wageni dhidi ya wananchi. Kuanzia kashfa ya kwanza ya Loliondo, Yaeda Chini, Bulyanhulu, Tarime, Buzwagi na hata Geita huko tayari wananchi wameanza kuona mwendelezo wa tabia ya kuwaona wananchi kama wanaingilia eneo la wawekezaji.
Yaani wananchi walioishi katika maeneo fulani kwa miaka na miaka leo wanaambiwa eneo hili ambalo lina utajiri wa dhahabu limeuzwa. Matokeo yake ni kuwa wananchi wanaona kuwa raslimali zao ambazo ni urithi wao unachukuliwa kama zawadi kwa wageni.
Kwa mfano, habari zilizoandikwa na gazeti hili wiki iliyopita kuhusu kusafirishwa kwa nyara za serikali usiku wa manane kunawakumbusha Watanzania habari kama hizo wakati fulani ambapo vitu kama hivyo vilijulikana au pale ambapo wawindaji wa kimataifa waliruhusiwa kuua wanyama wetu na wakati mwingine kuondoka na wengine ili wakapambe bustani zao huko Mashariki ya Kati.
Watanzania hawa wafanye nini wanapoona urithi wao unauzwa kwa wageni kama njugu kwa kisingizio cha kuvutia wawekezaji?
Hapa ndipo mgongano wa kifikra unapotokea sasa ambapo viongozi wa serikali na hasa vyombo vya dola vikitekeleza sera ya uwekezaji ya CCM vinapogongana na eneo ambalo lina viongozi wa Upinzani ambao sera yao ni kulinda maslahi na raslimali za taifa ili ziweze kutumika vizuri kuinua maisha yao. Hivyo, mgongano wa Tarime ni zaidi ya raslimali; kwani pia unahusisha utu wa wananchi wenyewe.
Wananchi hawawezi kujihisi kuwa ni wageni katika taifa lao na hasa yanapotokea mauaji. Kuna mtu katika Jeshi la Polisi ambaye hajui kuzuia maandamano au vurugu bila kuanza kumwaga risasi. Tumeliona Arusha mapema mwaka huu, na tumeshawahi kuliona huko nyuma huko huko Tarime.
Pamoja na kufanya Tarime kuwa mkoa maalumu wa Polisi, ni wazi kuwa juhudi za kuleta amani na utulivu zimeshindikana; kwani dhana ambayo inaongoza ina makosa.
Huwezi kuleta amani kwa kuleta polisi wengi, au kwa kuua watu wengi zaidi. Jamani, hili somo kwanini ni gumu hivyo wenzetu kulielewa? Kama ingekuwa rahisi hivyo, Assad wa Syria angekuwa anakula kuku kwa mrija tu baada ya kuua wananchi wake 700!
Kama kuua wananchi wanaopinga serikali au kupigania haki yao ingekuwa inatosha kuwanyamazisha, mauaji ya Sharpeville na yale ya Soweto yangeweza kuwafanya watu wa Afrika Kusini kukubali ubaguzi. Risasi hazijawahi kuzuia fikra za utu na kudai uhuru popote pale duniani.
Isitoshe, Serikali ya Tanzania haina risasi za kutosha kuwamaliza Watanzania wote wanaopinga uovu na maonevu. Serikali inakuwa kama kikolezo tu cha kizazi kingine.
Jamani; kama risasi zingewatisha watu, basi, baada ya mauaji yale ya Arusha wasingejitokeza tena watu kuandamana. Na naomba niwe mbebaji wa habari mbaya kwa watawala kwa kadri wanavyozidi kumwaga damu ya Watanzania ndivyo wanavyowafanya Watanzania kuanza kuona kuwa hawana cha kupoteza isipokuwa utu wao.
Na habari kuwa Mbunge wa Singida Mashariki na mwanaharakati ambaye anajua sana siasa za Tarime, Tundu Lissu kuwa aliwekwa ndani pamoja na wenzake; huku polisi wakizingira mochwari ambapo miili ya wana Tarime ilikuwa imehifadhiwa kusubiri ibada, zinashtua. Kumfunga Lissu au kuwafunga wale wote watakaokuja Tarime hakutoshi kuzuia fikra za mabadiliko, na serikali isipokuwa makini katika hili, amani inaweza kuvunjika zaidi Tarime.
Nawasihi sana watawala wetu na viongozi wetu wa kisiasa kukaa chini mara moja na kuzuia kulipuka kwa jambo hili kwa kutumia hekima zaidi kuliko kutumia nguvu. Risasi hazitazuia hili, jela hazijawahi kufunga fikra huru.
Ni mazungumzo tu yanayoweza kutuliza mambo. Na hapa naamini watu wa Barrick wana maswali ya kujibu; kwani tukianza kufuatilia na kuangalia mahusiano yao na vyombo vya dola na wananchi, tutaona jinsi gani kuna kitu hakiko sahihi.
Vinginevyo, Barrick ifunge mgodi huo na kuondoka; kwani uwepo wake haustahili kifo cha Mtanzania hata mmoja. Jamani, hizo dhahabu hazitaoza lakini katika umaskini wetu tusiwe tayari hata kuuza utu wetu.
Kama uwepo wa migodi hii unatufanya tuuane na kufungana na kupigana virungu, basi haitustahili. Tutumie hekima lakini kama hakuna wenye hekima kati yetu, tufunge mgodi ili watu wa Tarime watafute mambo mengine ya kufanya. Hatuwezi kukaa kama taifa katika hali ya wasiwasi wa kudumu.
Lula wa Ndali-Mwananzela
RAIA MWEMA
Mei 25, 2011RAIA MWEMA