Tarehe ya maandamano ya Tanzania nzima

Tarehe ya maandamano ya Tanzania nzima

Binafsi, hamjanishawishi bado.

Mzee hakuna anaeshawishiwa kuandamana. Shida na ugumu wa maisha,rushwa iliyokithiri serikalini,wanasiasa na viongozi kutajirika kupindukia,serikali kukosa dira na ufujaji wa rasilimali na maliasili zetu ndizo zinanishawishi mimi nitake kuandamana.

Kama huna shida,ugumu wa maisha au huoni hayo ya juu,mkuu huwezi kuandamana! Utasubiri kushawishiwa mpaka kaburini!
 
True story mazee. Mimi pia nina mtazamo huo. Maandamano yatafanikiwa tu yakiwa initiated na watu/raia/wananchi wa kawaida na siyo na chama.

Mkuu, kwa sentensi na maono hayo uloandika, mimi nakupongeza sana, kwamba kwa sasa ushawishi wa chama fulani against kingine. Ni masilahi binafsi ya chama fulani. Tija ni pale tu maandamano ya namna hii yawe ya umma wote. Ndiyo maana inaitwa nguvu ya umma, na si nguvu ya chama fulani.
 
msione kirahisi namna hiyo. Maandamano ni kitu kingine kabisa. Kwa sababu mtakuwa mmejunja katiba ya inchi kwahiyo mkiona wanajeshi wanawafyatulia risasi muone kawaida. Kuigeza inchi tz kuwa kama somalia,kwa sababu mnaweza kuongeza shida zaidi ya tulizonazo,tuanze maandamano halafu gala la siraha lifunguliwe kila mtu awe bunduki yake tuone kama kuna mtu atabaki

Unamfaham MARIA SUGU? ni nani kwako? kwa sasa yuko wapi? Acha mawazo finyo wewe.
 
Mkuu, kwa sentensi na maono hayo uloandika, mimi nakupongeza sana, kwamba kwa sasa ushawishi wa chama fulani against kingine. Ni masilahi binafsi ya chama fulani. Tija ni pale tu maandamano ya namna hii yawe ya umma wote. Ndiyo maana inaitwa nguvu ya umma, na si nguvu ya chama fulani.

Huu ndo mtazamo wangu siku zote mazee. Ila chama,makundi mbalimbali ya kijamii,NGOs etc. zinaweza kuamsha wananchi katika kujua na kudai haki zao. Then wananchi wenyewe ndo tuanze kudai kuondoka kwa utawala dhalimu. Then kwa wananchi ku-run the show,maandamano yatafanikiwa 100%!
 
naungana na woote ila napropose kuwa hivi vyama vya siasa vitutie hamasa tu afu maandamano tuyainitiate sisi wenyewe either by trade/workers union au social organazations coz tukitumia vyama viongozi wake kwanza watashtakiwa kwa uhaini na hiyo movement itakuwa suppresed easily coz na propaganda itatumika ila tukitoka sisi kama sisi wananchi hamna wa kutuzuia sema tena vyama vya wafanyakazi viongozi wake mh! Nna shaka nao hao kina mkoba, mgaya hamna kitu ila dah mi nshachoka maisha ni migumu mshahara haikutani yaani ukipokea salary ya mwezi huu huwezi baki na hela iikute ya mwezi ujao mi niko tayari kutoka as long as iwe movement ya ukweli do or die
 
wewe si umesema kuwa ulikuwa Libya? mbona hutaki kusaidia wenzako na experiance ya huko? au kwenye ile post yako ulikuwa unawaingiza watu mjini?
wewee kijana acha kuwaogopehsa watu
ninyi waoga tunaomba mkae kimya kabisa na mtuachie sisi uwanja
ninyi ni mamluki tu au watoto wa hao mafisadi
kwa wanaoishi maisha ya kubangaiza ndio watzanania wa kweli na ndio wanaojua shida na mateso ya hii Tanzania, sio wewe hivyo kama unaona ni kazi sana,kaa ndani kunywa chai na mkate inatosha ila kumbuka kuwa tukishawatoa hao mafisadi na wewe kama ni mtoto wao basi jua kuwa ni lazima utafute eneo la kwenda kukaa..
msione kirahisi namna hiyo. Maandamano ni kitu kingine kabisa. Kwa sababu mtakuwa mmejunja katiba ya inchi kwahiyo mkiona wanajeshi wanawafyatulia risasi muone kawaida. Kuigeza inchi tz kuwa kama somalia,kwa sababu mnaweza kuongeza shida zaidi ya tulizonazo,tuanze maandamano halafu gala la siraha lifunguliwe kila mtu awe bunduki yake tuone kama kuna mtu atabaki
 
msione kirahisi namna hiyo. Maandamano ni kitu kingine kabisa. Kwa sababu mtakuwa mmejunja katiba ya inchi kwahiyo mkiona wanajeshi wanawafyatulia risasi muone kawaida. Kuigeza inchi tz kuwa kama somalia,kwa sababu mnaweza kuongeza shida zaidi ya tulizonazo,tuanze maandamano halafu gala la siraha lifunguliwe kila mtu awe bunduki yake tuone kama kuna mtu atabaki

Kat$$$%%^^& wewe kila siku ni negative tuuuuuuuuuuuuuuuuu nenda kalale siku ccm siku ya maandamano uepuke zali period kwani lazima uandamane bana. Mijitu mingine sijui ipoje. Tangu CDM wameanza kuandamana umeona fujo yoyote au wewe tu fikra zako na hadithi za kutunga. hebu tuondokee kule
 
Mkubwa:
Wengi humu ndani ni mazungumzo ya kijiweni tu wala si ya kuyapa kipaumbele. Utawasikia wanasema oooh, naunga mkono, tupo pamoja nk lakini wao wenyewe pengine wamejilipua USA na kwingine hawawezi hata kurudi nchini kwa sababu wamechemsha. Sasa wanataka pa kutoke,, kwamba kuwe na machafuko nchini wapewe hifadhi za kisiasa huko walipo,, utumbo mtupu!
Hizi ni dalili halisi za frustrations. Msitake kuwachuuza watu na raia wema waache kujitafutia riziki eti wakaandamane. Kuna atakayeweza kukaa siku 18 kama wamisri? au mnaongeaongea tu?

KWA HIYO WAVUMILIE HATA HII YA NORTH MARA
 
msione kirahisi namna hiyo. Maandamano ni kitu kingine kabisa. Kwa sababu mtakuwa mmejunja katiba ya inchi kwahiyo mkiona wanajeshi wanawafyatulia risasi muone kawaida. Kuigeza inchi tz kuwa kama somalia,kwa sababu mnaweza kuongeza shida zaidi ya tulizonazo,tuanze maandamano halafu gala la siraha lifunguliwe kila mtu awe bunduki yake tuone kama kuna mtu atabaki

Du! kuna watu niwaoga sana hujui bila damu kumwagika hakuna mapinduzi ya kweli, 2napozungumzia mapinduzi lazima damu imwajike na siyo lelemama. Kalalabao
 
mi navyoona source nzuri iwe ktk madai ya wafanyakazi Tucta itoe ultimatum hadi mei mosi kima cha chini 315,000/= pamoja na madai mengine ya msingi ambayo najua serikali yetu kiziwi haitayafanyia kazi so siku ya maandamano ya mei mosi ndo tunaliendeleza hadi kung'oa huu utawala usiojali wananchi wake, na hii itakuwa fursa ya kuwahusisha watu wa vyama vyote kuliko yakiwa organized na cdm kuna watu though wana tabu hawatajitokeza coz wana itikadi tofauti. Cha muhimu ni vyama vya wafanyakazi kuplay their role, na workers unions zimeplay part kubwa sana ktk ukombozi wa wanyonge hata kwa tanganyika ziliplay hyo role , so kuanzia mei mosi tulianzishe

Mimi hii nimeipenda. Tuanzie hapahapa mpaka kieleweke.
 
True story mazee. Mimi pia nina mtazamo huo. Maandamano yatafanikiwa tu yakiwa initiated na watu/raia/wananchi wa kawaida na siyo na chama.

Ila la kujua tunachotaka ndo tuandamane,umenishtua kama si kunishangaza! Upo TZ au? Yaani huoni maisha yalivyokua magumu sana sasa? Bei za vyakula juu! Nauli za mabasi juu! Mfumuko wa bei juu! Bei za umeme na maji juu! Tatizo la umeme halijaisha toka 1961 wakati tuna gesi,makaa ya mawe,bahari,jua na upepo! Bado akina mama wajawazito wanakufa ovyo wakati serikali ina tumia magari ya milioni zaidi ya 200! Wakulima wanakosa masoko ya mazao yao,ivyo mazao kuoza au kuuza kwa bei za hasara!

Kama huna sababu ya kuandamana mkuu pole sana. Lakini mimi nipo tayari kwa sababu nina sababu za kutaka kuona utawala dhalimu wa CCM ungeanguka.
kwa hiyo tukiandamana ndio hayo mambo yote yatakuwa fresh?...na unamaanisha kuwa tukiandamana ccm itakubali kuondoka?na kumbuka usifananishe roho za wabongo na roho za waarabu ndugu yangu,mimi mwenyewe nataka kuandamana lakini nitaandamana kama tutaandamana wananchi wote na sio chama kimoja kwa sababu maisha yanatupiga wote
 
Ninadhani tunahitaji kujua tarehe ya maandamano. Toa mapendekezo yako tafadhali.
Vinginevyo CCM na serikali yake ichukue hatua kukabili ufisadi kabla haijawajibishwa.
 
mi navyoona source nzuri iwe ktk madai ya wafanyakazi Tucta itoe ultimatum hadi mei mosi kima cha chini 315,000/= pamoja na madai mengine ya msingi ambayo najua serikali yetu kiziwi haitayafanyia kazi so siku ya maandamano ya mei mosi ndo tunaliendeleza hadi kung'oa huu utawala usiojali wananchi wake, na hii itakuwa fursa ya kuwahusisha watu wa vyama vyote kuliko yakiwa organized na cdm kuna watu though wana tabu hawatajitokeza coz wana itikadi tofauti. Cha muhimu ni vyama vya wafanyakazi kuplay their role, na workers unions zimeplay part kubwa sana ktk ukombozi wa wanyonge hata kwa tanganyika ziliplay hyo role , so kuanzia mei mosi tulianzishe

Hili nalo ni wazo zuri
 
Yap yap JF sasa naona kunakucha kama hoja za hivi znaanza kuingizwa uku! Maandamano lazima yapangwe tena kama kuna kiongozi yeyote wa ngazi za juu CMD or chama chocote pinzani ambacho kinaguswa na hii hali ya Tz anayenisoma uku JF tafadhari sana naomba kikao kikaliwe mapema mpange vizuri siku, tarehe na muda wa kuanza maandamano nchi nzima, vituo vitajwe ili kila mkoa na watu wake siku hiyo wakutane tayari kwa kuanza maandamano. Kwa Dar, mwanza, mbeya na Arusha naombeni mikoa hii iwe ya mfano na ipewe viongozi wa ngazi za juu katika kuongoza hayo maandamano coz ndo vitovu muhim katika nchi hii. Maandamano yanayoendelea mkoa kwa mkoa kwa kuongozwa na CMD yasisisme naomba yaendelee huku yakiandaa maandamano mengine makubwa zaidi! Big up man kwa kutoa thread hii! Nakukubal!:usa2:
 
:wink2:
THE TIME................................ NOW 2011!

REGIONAL VENUES...................WAKUU WA MIKOA -NYUMBANI NA OFISINI

CENTRAL VENUE........................DODOMA

MAJOR TARGET...........................DAR ES...SALAAM.....IKULU

The game is over!
 
Mimi ni miongoni mwa watu ambao wanahimiza amani na kuihubiri.
Vilevile ni muumini mzuri wa utawala wa sheria na haki kama njia ya kuidumisha amani hiyo.
KATIKA MAMBO YANAYOIFANYA NCHI IWE YA AMANI NI UTAWALA WA SHERIA NA MATENDO YA HAKI KUTOKA KWA VYOMBO VYA UTAWALA.

Bunge letu lililopita lilisaidia kuwepo kwa uvumilivu wa watanzania dhidi ya udhalimu uonevu na ufisadi. Matarajio yalikuwa kuwa haki itaonekana.
Kila mmoja aliamini kuwa hatua madhubuti zitachukuliwa dhidi ya maonevu mbalimbali mbali.

Bunge la sasa limeanza kwa dhihaka, vijembe na hata mambo yanayofanana na umbeya. Wengine wameenda mbali na wamesema ni bunge la kimbeya na ndicho CCM ilichokuwa ikitafuta kwa kusisitiza gender wakati huu badala ya sifa.
Sikubaliani na hao waliofika huko kwenye kujibu dhihaka kwa dhihaka.
Wako wanawake wengi serious na pia wako wanaume wengi wambeya.
Bunge letu, serikali yetu, chama tawala vimepoteza matumaini ya watanzania kuwa ufisadi utakemewa pia kuondolewa, na hatimaye haki itafuatwa.
Utawala thabiti wa demokrasia na wa haki ndio ambao watanzania wanaulilia.
Watu wamekata tamaa hata katika kupiga kura kwani hawaamini kuwa haki itatendeka.

SASA KAMA HAKUNA MATUMAINI KWA WATUNGA SHERIA NA KAMA HAKUNA MATUMAINI KWA UONGOZI WA SERIKALI NINI KIFANYIKE?
Njia pekee inayobakia ni maandamano ya kuukataa udhalimu. Mimi ninaunga mkono maandamano ya kudai haki. Na hivi karibuni nitakuwa nikiyasema kwa nguvu na uwazi kwa njia mbalimbali.

NAOMBA MAPENDEKEZO YA TAREHE ZA MAANDAMANO NA ENEO LA KUKUSANYIKA KILA MKOA: VINGINEVYO CCM WATUPE TAREHE ZA KUCHUKUA HATUA ZA KUONDOA UDHALIMU NA KUSHUGHULIKIA KERO. Tunajua hapajawahi kutokea utawala mkamilifu au usio na madoa labda ule ujao wa Yesu Kristo kama wanavyoamini wakristo, lakini angalau utawala uonyeshe kujali raia na kukemea maovu yaliyo wazi.

Kwanini mchukue nchi wakati uchaguzi umepita na Rais Kikwete amepeta na kuapishwa kisheria kama Rais wa JM Tanzania.

Sasa mnataka leta vurugu.... Naomba vyombo vya Doula viwashughulikie ipasavyo na ipasavyo na sheria ichukue mkondo wake
 
:wink2:
THE TIME................................ NOW 2011!

REGIONAL VENUES...................WAKUU WA MIKOA -NYUMBANI NA OFISINI

CENTRAL VENUE........................DODOMA

MAJOR TARGET...........................DAR ES...SALAAM.....IKULU

The game is over!

IGP mwema kaa tayari wanakuja hao.

Mlete Kamanda Zubari (OCD ARUsha Town) awashughulikie kama anavyomshughulikia Godbless Lema (MB Arusha town)
 
moz-screenshot-1.png
quote_icon.png
Originally Posted by Salimia
Mkubwa:
Wengi humu ndani ni mazungumzo ya kijiweni tu wala si ya kuyapa kipaumbele. Utawasikia wanasema oooh, naunga mkono, tupo pamoja nk lakini wao wenyewe pengine wamejilipua USA na kwingine hawawezi hata kurudi nchini kwa sababu wamechemsha. Sasa wanataka pa kutoke,, kwamba kuwe na machafuko nchini wapewe hifadhi za kisiasa huko walipo,, utumbo mtupu!
Hizi ni dalili halisi za frustrations. Msitake kuwachuuza watu na raia wema waache kujitafutia riziki eti wakaandamane. Kuna atakayeweza kukaa siku 18 kama wamisri? au mnaongeaongea tu?

UNA MAANA GANI UNAPOSEMA RAIA WEMA? NI WALE KONDOO MLIOZOEA KUWATOA SADAKA HATA KELELE HAWAPIGI? aka MATESO BILA CHUKI?
 
msione kirahisi namna hiyo. Maandamano ni kitu kingine kabisa. Kwa sababu mtakuwa mmejunja katiba ya inchi kwahiyo mkiona wanajeshi wanawafyatulia risasi muone kawaida. Kuigeza inchi tz kuwa kama somalia,kwa sababu mnaweza kuongeza shida zaidi ya tulizonazo,tuanze maandamano halafu gala la siraha lifunguliwe kila mtu awe bunduki yake tuone kama kuna mtu atabaki

Hakutakuwa na sababu ya mtu yeyote kufyatua risasi wala kurusha mawe. Ni maandamano ya amani, ni nguvu ya umma ya kutaka mabadiliko katika utawala wa nchi. Naamini hata polisi na wanajeshi ambao tunakaa nao huku mitaani wataungana na raia kushinikiza kung'oka kwa utawala unaolea ufisadi na kuwaacha wananchi wakiangamia kwa dhiki.
 
Back
Top Bottom