Mtaka Haki
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 492
- 149
Mimi ni miongoni mwa watu ambao wanahimiza amani na kuihubiri.
Vilevile ni muumini mzuri wa utawala wa sheria na haki kama njia ya kuidumisha amani hiyo.
KATIKA MAMBO YANAYOIFANYA NCHI IWE YA AMANI NI UTAWALA WA SHERIA NA MATENDO YA HAKI KUTOKA KWA VYOMBO VYA UTAWALA.
Bunge letu lililopita lilisaidia kuwepo kwa uvumilivu wa watanzania dhidi ya udhalimu uonevu na ufisadi. Matarajio yalikuwa kuwa haki itaonekana.
Kila mmoja aliamini kuwa hatua madhubuti zitachukuliwa dhidi ya maonevu mbalimbali mbali.
Bunge la sasa limeanza kwa dhihaka, vijembe na hata mambo yanayofanana na umbeya. Wengine wameenda mbali na wamesema ni bunge la kimbeya na ndicho CCM ilichokuwa ikitafuta kwa kusisitiza gender wakati huu badala ya sifa.
Sikubaliani na hao waliofika huko kwenye kujibu dhihaka kwa dhihaka.
Wako wanawake wengi serious na pia wako wanaume wengi wambeya.
Bunge letu, serikali yetu, chama tawala vimepoteza matumaini ya watanzania kuwa ufisadi utakemewa pia kuondolewa, na hatimaye haki itafuatwa.
Utawala thabiti wa demokrasia na wa haki ndio ambao watanzania wanaulilia.
Watu wamekata tamaa hata katika kupiga kura kwani hawaamini kuwa haki itatendeka.
SASA KAMA HAKUNA MATUMAINI KWA WATUNGA SHERIA NA KAMA HAKUNA MATUMAINI KWA UONGOZI WA SERIKALI NINI KIFANYIKE?
Njia pekee inayobakia ni maandamano ya kuukataa udhalimu. Mimi ninaunga mkono maandamano ya kudai haki. Na hivi karibuni nitakuwa nikiyasema kwa nguvu na uwazi kwa njia mbalimbali.
NAOMBA MAPENDEKEZO YA TAREHE ZA MAANDAMANO NA ENEO LA KUKUSANYIKA KILA MKOA: VINGINEVYO CCM WATUPE TAREHE ZA KUCHUKUA HATUA ZA KUONDOA UDHALIMU NA KUSHUGHULIKIA KERO. Tunajua hapajawahi kutokea utawala mkamilifu au usio na madoa labda ule ujao wa Yesu Kristo kama wanavyoamini wakristo, lakini angalau utawala uonyeshe kujali raia na kukemea maovu yaliyo wazi.