Tarehe kama ya leo, 27 October miaka 26 iliyopita!

Hussein J Mahenga

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
745
633

Tarehe kama ya leo, 27.10. siku ya jumapili miaka 26 iliyopita Bi. Aisha, akiwa mjamzito, alitoka kidogo nyumbani akifanya mazoezi kama ilivyo ada ya kina mama Wajawazito. Katika mazoezi yake, mama huyu pia alidhamilia kuokota kuni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, na hii ni kawaida kabisa ya kina mama wa kijijni.

Hatua chache toka nyumbani kwake, katika kijiji cha Kayombo, huko Bukene, siku hiyo alipata kuokota kuni kwenye kipori kidogo.
Akiwa anakusanya kuni, ghafla mama huyu alishikwa na uchungu. Kwa kuwa alikuwa peke yake, mama huyu, kwa jina la Bi. Isha Nzingula, aliamua kuingia kwenye kichaka kidogo, kwa kinyamwezi huita ‘kasokola’ na kujilaza taratibu kabisa akiwa ametandika nguo yake moja tayari kabisa kwa lolote lile ambalo lingetokea.

Alhamdulillah, Mungu alivyo mkubwa, jioni ile Bi. Isha alifanikiwa kupata mtoto chini ya kichaka kile. Kwa kawaida, wakati mwingine mzazi huamua kumpa jina litokanalo la sehemu alipozaliwa, Bi. Isha alimuita kidume huyu kwa jina la ‘Kasokola’, yaani kichaka.

Furaha kubwa sana kwake kumpata mtoto wa kiume kwa kuwa tayari alikuwa na watoto saba wakiwa wote wa kike.

Tarehe kama ya leo, ‘Kasokola’ alikamilisha furaha ya Bi. Isha aliyoingojea kwa miaka mingi tena katika upweke mkubwa sana.
Happy birthday Kasokola, Happy birthday Uncle Kaso!
 
Nimependa sana ulivyojielezea mkuu ni wachache wenye kuelezea mbele za watu hasa jf kwamba walizaliwa sehemu kama hiyo.

Hongera sana kwa Bi Aisha M'mungu amtunze na hongera kwako pia mkuu M'Mungu akupe kila la kheri.
 
Nataman nijibu kila meseji, lakini kwa ajili ya majukumu nashindwa.
Niseme tu kwamba, nashukuruni sana wadau wa JF, na Mungu awabarikini sana
 
Back
Top Bottom