Kumbukumbu: tarehe kama ya leo miaka 12 iliopita Manchester United iligaragazwa bao 6 kwa 1 na majirani zao Manchester City.

bakundande jr

JF-Expert Member
Oct 22, 2021
507
670
Ikiwa leo ni siku ya 23 katika mwezi wa kumi sawa kabisa na tarehe ambayo vigogo wa soka nchini uingereza nazungumzia mashetani wekundu Manchester United ambapo waliwaalika majirani zao Manchester City katika mchezo wa ligi kuu soka nchini humo mzunguko wa tisa.

Siku hiyo haitasahaulika kwa mashabiki wa pande zote mbili ambapo ilishuhudiwa timu mwenyeji akivurumishwa kwa kipigo cha mbwa mwizi katika uwanja wao wa nyumbani ikiwa ni miazi michache toka wakongwe hao na timu bora ya enzi hizo kumchakaza mpinzani wao mahili namaanisha washika mitutu toka jiji la London arsenal kwa kipigo cha mabao nane kwa mawili.

Hakika siku hiyo ndio siku ambapo mapinduzi ya soka katika jiji hilo la Manchester yalitokea na ukubwa wa jina la Manchester City uliibuka na hatimae safari ya mafanikio kuanza kushamiri.

Ikumbukwe kipindi hicho Manchester United ilikuwa chini ya kocha nguli na maarufu mzee wetu sir alex ferguson ikiwa na wachezaji hatari kama kipa david de gea, nani pamoja na Wayne Rooney.
Huku upande wa Manchester City iliongozwa na kocha Roberto Mancini akiwa na wachezaji kama mtukutu mario balloteli,david silva pamoja na kun aguero.

Magoli ya Manchester City yaliwekwa kambani na balotelli pamoja na edin dzeko ambao kila mmoja aliingia nyavuni mara mbili, huku mengine yakifungwa na aguero pamoja na david silva. Huku goli pekee na lakufutia machozi lilifungwa na D.Fletcher
hqdefault.jpg
1200.jpg
 
Ama kweli miaka inakwenda Kasi sana.

Rafiki zangu walitoroka SEMINARY kwenda kuangalia Hiyo Mechi nikiwa kadogo sana.

Nilitamani Mwenda lakini nikaogopa sheria za shule.

Jamaa wakatuletea msemaji why always Me
Manchester city 6-1 man u.

Miaka inakwenda Kwa Kasi sana dahhhhhh
 
Ama kweli miaka inakwenda Kasi sana.

Rafiki zangu walitoroka SEMINARY kwenda kuangalia Hiyo Mechi nikiwa kadogo sana.

Nilitamani Mwenda lakini nikaogopa sheria za shule.

Jamaa wakatuletea msemaji why always Me
Manchester city 6-1 man u.

Miaka inakwenda Kwa Kasi sana dahhhhhh
Sikua hazigandi.
Ngoja tuone next weekend wanakutana tena
 
Back
Top Bottom