Miaka 12 Sasa dada yangu bado upo moyoni mwangu
Sent using
Jamii Forums mobile app
Pole sana ndugu,
Nafsi yako, moyo na akili vyote vinamaumivu juu ya kuondokewa na ndugu yako.
Naomba uniruhusu niseme haya, pengine ikasaidia kupunguza sumu unazobeba tangu dada yako aage dunia.
Mimi si mwanasaikolojia ila unahitaji kuhama (kimawazo, kifikra, kimtazamo) hapo ulipo ili maisha yako mengine yaendelee. Naomba ufungue ufahamu wako twende pamoja...
1. Wakristo tumeagizwa kwenye neno la Mungu, Linda sana MOYO wako kuliko vyote ulindavyo maana ndiko zitokako chemchem za UZIMA. Ukitaka kuendelea kuishi kwa amani, usiruhusu MOYO wako ujeruhiwe au ubebe mawaa, uchungu, chuki, au kushikilia watu kwa hasira.
2. Kuna mahali umesema marehemu alikuwa ndo baba yako na mama yako kwa maana alikuwa anasimamia makuzi yako ili uweze kujitegemea (aidha alikuwa anakusomesha au akutafutie kazi au akupe mtaji wa biashara au akuunganishe na biashara) bahati mbaya umauti ukamkuta kabla alichokuahidi hakijatimia au kukikamilisha. Wakristo tunaagizwa kwenye neno la Mungu, ALAANIWE AMTEGEMEAYE MWANADAMU NA KUMFANYA KUWA KINGA YAKE.. sina hakika hilo neno liko kitabu gani ila najua linazungumza namna hiyo. Ndugu yangu, jitahidi na anza kufikiri kwa upya namna ya kumtoa dada yako kwenye moyo wako kuwa yeye ndo alikuwa amebeba DESTINY ya maisha yako. Hujatamka hivyo ila maneno yako yanaonesha hivyo.
3. Ulishawahi kufikiri pengine dada yako angefariki siku hiyohiyo mwaka huo huo ila kwa ajali ya gari au angeumwa na nyoka au angeumwa malaria na kabla hajafika hospitali akafa bado ungekuwa na maumivu kama uliyonayo leo...? Jaribu kuwaza zaidi na zaidi... Je angekuwa hai hadi leo ila angebadilisha msimamo wake juu yako wa kuto kukushughulikia kama mdogo wake ilhali uwezo anao, Je, bado ungekuwa na uchungu ulionao leo?
4. Tangu 2016 umeandika huu uzi hadi leo bado mtuhumiwa hajapata hukumu inayostahiki, kwa mara nyingine wakristo tunaaswa, DUNIANI MNAYO DHIKI, ILA JIPENI MOYO.... (The World is NEVER fair)
Sasa unawezaje kujipa moyo ilhali una uchungu, kufarijiwa ya pole kwa msiba wa dada haitoshi. Yapasa kufanyika jambo, chukua hatua ondoa uchungu moyoni ili Mungu aliyekuleta duniani aruhusu njia zake kwa kumhukumu muuaji, upate amani ya moyo na maisha mengine yaendelee. Usisahau tena wakristo tumeendelea kuaswa...TAFUTENI KUWA NA AMANI NA WATU WOTE.... Pia tumeambiwa, MAMBO MENGINE HAYAWEZEKANI ILA KWA KUFUNGA NA KUOMBA...
Kwa maana VITA TUNAYOPIGANA SI YA DAMU NA NYAMA BALI YA ROHO....
Tena... NITWIKENI MIMI SHIDA NA FADHAA kwa maana MIMI NIRA YANGU NI LAINI NA MZIGO WANGU NI MWEPESI...
Aiseeh, mie sio mhubiri ila sijui kwanini maneno haya yamenijia kichwani wakati naandika hapa...
Naweza sema unahitaji mwanasaikolojia kuutibu moyo wako ila ukitulia na neno la Mungu ukayasoma hayo maandiko na kufuata kipengele kimoja kimoja hapo juu; kwa uponyaji wa MOYO wako kwanza, kisha mengine yote yatafunguka.
Sijui ni kwa namna gani ila wakati unajihudumia, utashangaa watesi wako wanajipeleka kwa kadhi kujistaki...mambo ya rohoni ni ya ajabu sana...
Usisahau hili, ZABURI 23:.....WAANDAA MEZA MBELE YANGU MACHONI PA WATESI WANGU.....
Yaani ile unataka ufanikiwe ndoto zako zinazimwa paap, kama kibatari... kibinadamu hasira na huzuni lazima zikushike....kumbuka tumeaswa, JUA LISIZAME BADO MNA HASIRA MIOYONI MWENU....
Niseme tuu pole sana kwa yaliyokusibu, ila hapa ilipofika yatosha, okoa muda maana muda haurudi tena, ni miaka 12 sasa. Kama moyo umekamatia mtu na bado marehemu pia amejaa moyoni si rahisi mambo mengine kuendelea kwenye maisha yako kwa ufasaha, kumbuka hili.....NDIKO ZITOKAKO CHEMCHEM ZA UZIMA.... (MOYO)
Alamsiki na uwe na wakati mwema.
Usiache kuchukua tahadhari kujikinga na Korona na hata siku moja usimuombee adui yako mabaya bali ....MSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO.
KASINDE.