Taratibu za Mahakama

AMOS PHILMON

New Member
Aug 6, 2018
1
1
MSAADA.
1.Mlalamikaji mmoja anaweza fungua kesi moja kwenye Mahakama mbili tofauti tofauti akimlalamikia mtu yuleyule na kwa kosa lilelile?
2.Ukitaka kuandika barua ya kuomba kubadilishiwa Hakimu wa kesi yako ambyo iko Mahakama ya Mwanzo yenye Hakimu mmoja barua hiyo unamwandikia nani?
 
Naomba kukujibu japokuwa usirely sana kwenye majibu yangu yakikupoteza ukaja kunilaumu jitahidi uwatafute wahusika wa hayo mambo wakupe ushauri walipe sitahiki zao, sababu nao wanahitaji kulipa bills mbalimbali.
Kwa swali lako la kwanza kisheria hiyo inaitwa res-subjudice, yaani ukifungua kesi mahakamani na kesi hiyo ikiwa inaendelea haijaisha huwezi kufungua kesi kama hiyo katika mahakama uliyofungua kesi ya kwanza au mahakama nyingine. Maana yake ni kwamba mahakama haiwezi kusikiliza kesi mbili zenye mahadhi sawa na lengo ni kuhakikisha kesi zinafikia ukomo. Ila kuna mazingira lazima yazingatiwe ili tuseme kesi mbili zinafanana mfano hoja bishaniwa kwenye kesi ya kwanza ni sawa na hoja bishaniwa kwenye kesi ya pili lakini pia Wadaawa katika kesi ya kwanza ni wale wale katika kesi ya pili pamoja na mazingira mengineyo. Lakini Kwasababu hujaeleza kiundaji juu ya kesi yako hatuwezi jua kama hayo mazingira yanafit au lah.

Katika swali la pili kwa utaratibu maombi yako yanapaswa kwenda kwa hakimu huyo huyo anaesikiliza kesi yako, kwa mahakama ya mwanzo unaweza kuyapeleka kwa mdomo au kwa maandishi utakavyoona inafaa, unapaswa kueleza sababu za msingi za kwanini hutaki hakimu huyo asikilize kesi yako mfano ana maslahi na hiyo kesi yako. Hakimu akiyasikiliza maombi yako anatakiwa kuyatolea maamuzi kama anajiondoa au hajiondoi, in case akikataa kujiondoa ataendelea kusikiliza kesi yako mpaka iishe na kama hutoridhika na maamuzi hayo inaweza kuja kuwa moja ya sababu yako ya rufaa. In case akikubali kujiondoa mahakama zina utaratibu utatafutiwa hakimu mwingine wa mahakama ya mwanzo nyingine iliyopo karibu atasikiliza kesi yako.
 
Back
Top Bottom