Mwalimu anayedaiwa kumbaka Mwanafunzi afutiwa Dhamana

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Misungwi imemfutia dhamana Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kilimo, Paulo Charles (39) aliyetuhumiwa kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wake ili asiharibu ushahidi upande wa mashitaka.

Akimsomea mashitaka mawili kwenye kesi ya makosa ya jinai namba 79 ya mwaka 2023, Wakili wa upande wa Serikali, Liliani Mery akisaidiana na Mwendesha Mashitaka Ramsoney Salehe, alisema kosa la kwanza la kubaka lilitendwa na mwalimu huyo tarehe tofauti tofauti za Februari na Machi, 2023 katika Kijiji cha Ukiriguru.

Alisema alimbaka mwanafuzi mwenye miaka 15 kinyume cha sheria kifungu cha 130 (1) 2 (e) na 131 ya kanuni ya adhabu ya makosa ya jinai sura 16 ya marejeo ya 2002.

Alimsomea kosa la pili kuwa kwa tarehe tofauti za Februari na Machi mwaka huu kwenye kijiji hicho kufanya mapenzi na mwanafunzi huyo wa darasa la saba na kumpa ujauzito kinyume cha Sheria ya Elimu kifungu cha 60 (A) kifungu kidogo (4) sura ya 353 kama kilivyorejewa na sheria 2 ya 2002.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Misungwi, Amani Shao alimuuliza mtuhumiwa kama kweli alitenda makosa hayo, mwalimu huyo alikataa kuyatenda na kuiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa kupanga tarehe nyigine ili kumleta wakili wake atakaye mtetea.

“Naiomba Mahakama yako tukufu kupanga tarehe nyingine kwani nimetuma maombi kwenye Chama cha Walimu Tanzania Taifa (CWT) kuniwekea Wakili ili kunitetea bado hajafika kwa sasa,”aliiambia Mahakama

Naye, Wakili Mery aliileza Mahakama kuwa mtuhumiwa ameanza kuvuruga ushahidi kwa kuwa yuko nje kwa dhamana akidai kwakuwa ameomba tarehe ili aje wakili wake, upande wa mashitaka hauna pingamizi kuweka wakili ila kwa muda huo Mahakama ifute dhamana ili hasiharibu ushahidi wa upande wa mashitaka .

“Upande wa mashitaka hatuna pingamizi kuwa na wakili kwani ni haki yake, mtuhumiwa yuko nje anaingilia ushahidi, tunaomba Mahakama ifute dhamana kwa kifungu cha 150 sura ya 20 marejeo mwaka 2002, Mahakama ikiona inafaa kufanya hivyo,”alisema

Mtuhumiwa baada ya kusikia sheria hiyo aliiomba Mahakama kesi iendelee hata bila wakili wake na siku wakili akifika ataendelea, Mahakama baada ya kusikiliza pande zote mbili ilitoa uamuzi mdogo kwa hilo.

“Kwakuwa upande wa mashitaka umekuwa na uhakika kuvuruga ushahidi ukiwa nje, umeleta maombi ya kufutiwa dhamana mtuhumiwa kwa kifungu cha 150 ya makosa ya jinai sura 20 marejeo ya mwaka 2002, Mahakama imekufutia dhamana ili usiharibu ushahidi ukiwa nje, kuweka Wakili ni haki yako ya kimsingi,”alisema Shao

Hakimu Shao aliahilisha kesi hiyo hadi leo Julai 11, 2023 kwa ajili ya kuja kusomewa mtuhumiwa maelezo ya awali na upande wa mashitaka kuanza kusikiliza ushahidi huku mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi baada ya kufutiwa dhamana.

MWANANCHI
 
Mtoto wa 15yrs, darasa la 7, mbna ilitakiwa awe 4m 2 km sio 3.

Ila walimu wanachopatia kutokana na wanafunzii wao, bas tyuuh hekima na busara italamaki kwao, hawa watoto wa sahivi wanakuharibia future hivi hivi.

Polee yake huyo mwalimu mkuu.
 
Back
Top Bottom