Taratibu za Kisheria za kipuuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taratibu za Kisheria za kipuuzi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by mzanganyika, Sep 15, 2009.

 1. m

  mzanganyika JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 257
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi nimekuwa nikisoma habari kwamba mtuhumiwa amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka mazito kama ya mauwaji lakini mtuhumiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka na uwezo wa kusikiliza kesi za namna hiyo.

  Hivi mtu mwenye akili zake anaweza kwenda sebuleni kwa lengo la kujisaidia halafu akasema hapa hapafai kujisaidia, natakiwa niende msalani?

  kwa nini muda hauheshimiwi katika kutekelezxa sheria wakati sote tunajua 'justice delayed is justice denied'.

  Pengine hapa kuna wanasheria wanaoweza kutusaidia kwa nini mwenye haja asiende msalani moja kwa moja na kwanza apitie sebuleni.
   
 2. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Mimi si mwana sheria ila hizi ni taratibu za kiutendaji tu, kwamba ni lazima kupitia mahakama ya chini ndo ufike ya juu. Kama vile huwezi kwenda ahera kama ujafa, ni lazima ufe kwanza n then ------.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Inategemeana na architectural design.... kama toilet iko uwani na inabidi upitie ukumbini ndio utoke nje... hunabudi kufuata njia.Hutaacha kupita sebuleni kwa vile unaenda toilet.Likewise mfumo wetu/architecture ya mahakama zetu iko kama hivyo.... utaanza kwenda mahakama za chini kwa ajili ya kusomewa mashtaka na hatimaye PI kabla ya commital to High Court. Tulikopi ramani za wenzetu hivyo tutaishi hivyo hivyo na inconviniences.Sababu ya kwenda mahakama za chini ni kusomewa mashtaka huku taratibu nyingine zikiendelea ikiwa ni pamoja na kukamilisha upelelezi/uchunguzi.Kumbuka mahakama za juu ni chache na hivyo huwezi kwenda kuzidisha msongamano, na hata wangesomewa mashtaka huko bado ksei isingeweza kuendelea.
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Sep 23, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wewe, hata kupitia mahakama ya chini na wenyewe ni utaratibu wa kisheria kwa ajili ya kuiandaa kesi kufikishwa High Court.
   
Loading...