Kaunga Ilumbu Lyane,
Ni kweli nina kamwanga kidogo ila si kakubwa.
Kuna kijana alikuwa anataka kuowa kwetu ila akataka kuwahusisha ndugu upande wa Baba wakati yeye alikuzwa kwa upande wa Mama. Maadamu baba yake alikuwa hajawahi kufika kwetu RASMI kuhusu kuhusu watoto zaidi ya kuwapitia na kuwaona tu, ilibidi taratibu zitumike.
Kilichofanyika ni kama walikuja kutoa POSA kwa ajili ya dada yetu ingawa dada mwenyewe alishafariki. Posa ilipokubaliwa na kupokelewa, jamaa akawa kama MUME halali kwenye familia na anatambulika RASMI. Kutoka hapo akawa Baba anayefahamika kwa upande wa mama official na kwenye harusi ya kijana, baba yake Mzazi akasimama kama Baba Mzazi kweli na si wa kusemwa pembeni.
Kijana mwingine na yeye alipotaka kuoa, utaratibu huo ulitumika kwa Baba kuja Rasmi kwa ndugu wa Mama mtu na kutoa POSA ya mtoto na hapo akawa BABA rasmi na kwenye harusi akawekwa High Table kama baba Mzazi maana vinginevyo ni wajomba tu wangelikaa na yeye asingeruhusiwa kuwa pale high table na sana sana kwa huruma kama Mgeni mualikwa.
Hivyo kwa ufupi, nenda na WAZEE nyumbani kwa huyo Mama na ukajitambulishe na kumtolea Posa huyo Mwanao. Ila mjulishe Bibi ya huyo mtoto mapema malengo ya nyie kwenda hapo kwake ili na yeye ajikusanye na ndugu zake/Marafiki na wawajadili kuhusu KULIPA FAINI ya Kum-mimba mtoto wa Kinyamwezi na kumuacha na Mtumbo wake - SHENZI sana shemeji weee....... 🙂
Nategemea itakusaidia hii habari kwa ufupi. Kama vipi uliza zaidi ntajitahidi kukupa maelezo kwa uelewa wangu.