Wale matapeli mje mjifunze kwa mwenzenu yamemkuta ya kumkuta na wewe ulie fanya hii msaidie mwenzio acha roho mbaya..


Za mwizi ni 40 hatimaye
View attachment 1217126
Kitu kama hiki kimetokea kama wiki imepita pale mbezi kwa msuguli.
Nilikuwa natoka zangu mbezi Mwisho naelekea ubungo, nafika pale mbezi kwa msuguli naona pembezoni mwa road kuna dogo anafinywa, anachezea kichapo. Kwa haraka haraka alionekana hazidi miaka 20, ni kadogo mno hadi muonekano.
Ikabidi nikatoka road, nikasogea. Sasa ile nashuka naona naratibu watu wanasogea zaidi na silaha walizozipata kwa urahisi, mwenye jiwe, fimbo, tairi na wengine wakigeuka Tyson. Nilicho waza ni kumchomoa kwanza ili nisikie nin chaendelea, maana raia unaweza kuta wanaua hata mtu bila hatia kisa, hata kasingiziwa mwizi na binti waliye kwazana tu.
Ikabidi nami nikajiunga kumsukum sukuma dogo, na kumpiga kofi za mgongoni, kumshtua tu pia raia wasiweke upinzani wa awali namimi. Vuta mkanda kijana wa huyo dogo nikamweka, biti kidogo kwa washkaj wale boda boda watulie.
Haikiwa rahisi kama mwalimu wa darasa kuwatuliza watoto wa shule ya msingi. Lakini shukrana iliwezekana. Story ilivyoenda dogo ni kweli aliiba tigo pesa, alifanya utapeli kwa kuelekezwa na watu walikuwa wamepaki pembeni na gari, baada ya tukion kunuka, wale wakakimbia na gari.
Kufupisha hadithi dogo nilimtoa hapo, lakini kubwa zaidi watu wawe makini mno, wizi wa tigopesa bado upo, mbinu nyingi lakini ya kijinga zaidi ambayo unaweza kujinasua nayo ni kuwa usitume pesa bila kupewa pesa kwanza.
Maana dogo alipoona mbinu elekezi zimegoma ndio akaomba awekew fedha, ilipowekwa akajifnaya amesahau kwenye iliyopaki, wale wa gari walipo wekewa hela waka washa gari kumsubili dogo kwa mbele, ndipo alipodakwa sasa na wadau.