Tapeli yamtokea puani, tumbo lajaa maji

Tapeli yamtokea puani, tumbo lajaa maji

Sio utapeli mpya uo utapeli upo mda tuu mkuu ni wale wanakwambia pata vifurushi kwa bei nafuu (tigo,voda, halotel au airtel) na unakuta package imejaa GB,Dakika na SmS za kutosha kwa bei chee alafu ni kwa mwaka mzima sasa jamaa kaingia mkenge alitaka kutapeli mtu kumbe huduma yenyewe hana na mwizi.Ukisikia kenge kaingia mkenge ndio iyo sasa
Hivi huwa najiuliza, inakuwaje mtu akwambie anauza kifurushi kwa bei nafuu kuliko mzalishaji mwenyewe, hawa wananunua wapi mpaka watuuzie kwa bei nafuu na ya kutupa kuliko mzalishaji mwenyewe?, ukijiuliza kama mimi hili la kutapeliwa vifurushi halitokupata kamwe.
Tuache kupenda miteremko ndo maana wengi wetu tunaumizwa.
 
People tend to associate everything with witchcraft. Some things happen due to nature and one's lifestyle, and its sad our first impulse is to think we have been bewitched.

I suggest we check out with doctors before making such inept conclusions.
 
Kitu kama hiki kimetokea kama wiki imepita pale mbezi kwa msuguli.

Nilikuwa natoka zangu mbezi Mwisho naelekea ubungo, nafika pale mbezi kwa msuguli naona pembezoni mwa road kuna dogo anafinywa, anachezea kichapo. Kwa haraka haraka alionekana hazidi miaka 20, ni kadogo mno hadi muonekano.

Ikabidi nikatoka road, nikasogea. Sasa ile nashuka naona naratibu watu wanasogea zaidi na silaha walizozipata kwa urahisi, mwenye jiwe, fimbo, tairi na wengine wakigeuka Tyson. Nilicho waza ni kumchomoa kwanza ili nisikie nin chaendelea, maana raia unaweza kuta wanaua hata mtu bila hatia kisa, hata kasingiziwa mwizi na binti waliye kwazana tu.

Ikabidi nami nikajiunga kumsukum sukuma dogo, na kumpiga kofi za mgongoni, kumshtua tu pia raia wasiweke upinzani wa awali namimi. Vuta mkanda kijana wa huyo dogo nikamweka, biti kidogo kwa washkaj wale boda boda watulie.

Haikiwa rahisi kama mwalimu wa darasa kuwatuliza watoto wa shule ya msingi. Lakini shukrana iliwezekana. Story ilivyoenda dogo ni kweli aliiba tigo pesa, alifanya utapeli kwa kuelekezwa na watu walikuwa wamepaki pembeni na gari, baada ya tukion kunuka, wale wakakimbia na gari.

Kufupisha hadithi dogo nilimtoa hapo, lakini kubwa zaidi watu wawe makini mno, wizi wa tigopesa bado upo, mbinu nyingi lakini ya kijinga zaidi ambayo unaweza kujinasua nayo ni kuwa usitume pesa bila kupewa pesa kwanza.

Maana dogo alipoona mbinu elekezi zimegoma ndio akaomba awekew fedha, ilipowekwa akajifnaya amesahau kwenye iliyopaki, wale wa gari walipo wekewa hela waka washa gari kumsubili dogo kwa mbele, ndipo alipodakwa sasa na wadau.
Kuna mmoja na yeye jana kaokolewa na askari pale msimbazi karibu na fire, yeye baada ya kushtukiwa akakimbilia msikiti wa makonde akaingia ndani akapanda ghorofani kwa hiyo wanachi wakajaa hapo nje ,ilibidi polisi waje fasta wakapanda juu ghorofani wakamchomia wakasepa naye.
 
woi
Mleta uzi hautupati..Najua umetega ili watu waje wasaidiwe kuwakomesha wezi wao ....Tumestuka
Mimi sijui lolote kuhusu uchawi mkuu wala ata sipromoti biashara ya mtu..uyo jamaa apo yamemkuta anaomba alie mfanyia yaliyo mpata amsamehe na amrudishie hali yake ya awali...ivyo tu
 
Exactly mkuu sema wapo kweli wanao fanya iyo biashara (wizi huu) na wengi ni wafanyakazi wa hayo hayo makampuni sema sasa kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani
Hivi huwa najiuliza, inakuwaje mtu akwambie anauza kifurushi kwa bei nafuu kuliko mzalishaji mwenyewe, hawa wananunua wapi mpaka watuuzie kwa bei nafuu na ya kutupa kuliko mzalishaji mwenyewe?, ukijiuliza kama mimi hili la kutapeliwa vifurushi halitokupata kamwe.
Tuache kupenda miteremko ndo maana wengi wetu tunaumizwa.
 
Uyo alie mjaza maji na aliye jazwa wote siwajui labda umuulize uyo mlalamikaji kama anamjua na kama anamjua asinge omba msamaha nmeshara hapa Jf kama kweli kuna mtu kafanya uo mchezo amrescure uyo jamaa maana inaonekana yamemfika kweli na pia iwe funzo kwa wapenda shortcuts

Na kwa nini hufanye biashara ya wizi aidha kwa kuuza au kununua? mtaishia kupigwa kila siku Maana kila uzi utakao ona una mada za wizi utajua ni mtego kumbe mengine ni mafunzo
Naaam, ukiingia kingi tu umeliwa, mara nyengine matapeli hutumia njia mfano wa hii sasa kama wewe ushapigwa na bado una kiwewe hasira na mawenge ya kupigwa ni lazma uingie pm kuanza kuulizia aliye mjaza maji huyo tapeli anapatikana wapi ili nawe ukamchome sindano aliyekutapeli, kumbe unakwenda kumalizwa na tapeli mwengine.
Kaa mbali ukishaumizwa, jigange majeraha yako, jipange upya anza upya tayari ushapatata somo.
 
Aache ung'ombe uyo pimbi aende hospital fasta akatibiwe ,hawa matapeli wanapataga shida sana ata wakiumwa mafua tu wanajua mahakama za jadi zimehukumu tiari . Kuna boya mmoja kariakoo juzi kati aliugua ghafra miksa kuishiwa nguvu ghafra jamaa akaanza kutoa wosia kwamba ugonjwa wake sio wakupona yeye niwakufa full kuwaomba wana waangalie familia yake pind atakapo ondoka hilo wenge lote kumbe alimliza mtu af akapigwa mkwara wa kiafrika alivyo develop tu hizo symptoms akajua kweli wahuni sio watu kumbe dengue ndio ilikua inamuandama muhuni yule .
 
...kawaida ya mali ya wizi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom