Tanzia- tangazo la msiba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,722
2,000
577251_10202094275151833_1703000588_n.jpg


TANGAZO LA MSIBA:

Jumuiya ya Watanzania Roma pamoja na Jumuiya ya Watanzania Italia zinasikitisha kutangaza kifo

cha Ndugu Abdulli Abuu(HATIBU CLEAN HEART) kilichotokea tarehe 08-12-2013 mjini Rome

kwenye Casa di Cura (HOSPICE S. ANTONIO DA PADOVA) baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kutokana na msiba huu ambao sisi sote kama watanzania unatugusa, tunaombwa tujumuike kwa

pamoja tuweze kuangalia mpang
o mzima wa msiba huu! Mjini Rome tumeamua kuwa na kikao siku

ya Jumanne tarehe 17 Disemba saa kumi na moja kamili, maeneo ya Termini kwenye restaurant ya

Wahindi iliyopo kwenye Mtaa wa Via Principe Amedeo. Na kwa wakazi wa NAPOLI na mkoa mzima

wa CAMPANIA kutakuwa na mkutano siku ya jumamosi tarehe 14/12/2013 PENITAMARE kwa dada

MARY kuanzia saa kumi Jioni. Tunaombwa tujumuike kwa wingi. Mwenyezi Mungu amlaze

marehemu Abdulli Abuu mahali pema peponi amina.


MAWASILIANO:

ROMA: 3391597134 KATIBU

NAPOLI: 389 8583370 KATIBU
 

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,145
2,000
Mwenyezi MUNGU mwingi wa Rehema na awape Amani yake wote wale waliopatwa na msiba huu mzito.
Na roho ya Marehemu ailaze mahala pema peponi. Amina!
 

Mapi

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
6,852
1,250
apumzike kwa amani. Mungu mwenye Rehema atupe tuliobakia tafakuri njema ya fumbo hili.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom