Tanzia: Salome Kiwaya afariki dunia katika ajali iliyotokea Dodoma

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Mwenyekiti wa Umoja wa Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Dodoma, Salome Kiwaya amefariki dunia kufuatia ajali iliyohusisha magari matatu leo mkoani Dodoma.

Pia alikuwa Mwandaaji wa Miss Dodoma na Kanda ya Kati. Ikumbukwe ndiye aliyemtoa Miss Tanzania 1995, Emilly Adolf. R.I.P Mama Kiwaya
IMG_20161008_092221.jpg

1.jpeg

Ajali hii imetokea leo katika eneo la Emaus, Mkoani Dodoma ambapo imehusisha gari kubwa mbili na moja dogo aina ya Toyota Noah. Inadaiwa kuwa Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika mpaka sasa.

2.jpeg

Askari Polisi wakiwa eneo la tukio kuokoa majeruhi.

3.jpeg
 
Mkuu
figganigga ww mkali, mm nipo Dodoma picha hizo sijazipata wala chanzo cha ajali
hivi ilikuwaje Mkuu mpaka Noah ikabanwa na kumpoteza Mama yangu Salome Kiwaya Mwenyekiti wa UWT na mmiliki wa bendi ya SAKI Star
 
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Dodoma, Salome Kiwaya amefariki dunia leo kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha magari matatu mkoani Dodoma.
Ajali hiyo iliyotokea leo mchana imehusisha lori la mizigo, gari dogo aina ya Noah na Costa. Taarifa za awali zinaeleza kuwa chanzo ni dereva wa Noah kushindwa kuchukua tahadhari kabla ya kuingia barabara kuu.
Hapa chini ni video fupi kuonyesha ajali hiyo.
 
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Salome Kiwaya amefariki dunia kufuatia ajali iliyohusisha magari matatu leo mkoani Dodoma.

Pia alikuwa Mwandaaji wa Miss Dodoma na Kanda ya Kati. Ikumbukwe ndiye aliyemtoa Miss Tanzania 1995, Emilly Adolf. R.I.P Mama Kiwaya
1.jpeg

Ajali hii imetokea leo katika eneo la Emaus, Mkoani Dodoma ambapo imehusisha gari kubwa mbili na moja dogo aina ya Toyota Noah. Inadaiwa kuwa Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika mpaka sasa.

2.jpeg

Askari Polisi wakiwa eneo la tukio kuokoa majeruhi.

3.jpeg
 
Nimempoteza rafiki yangu kipenzi. Tulikuwa wote wakati anaanza Saki star, wakati huo bado yupo CDA. Salome shoga yangu, I wish I could be there to rest you in peace. Pole shemeji yangu, Sera na wadogo zako. Daima tutakukumbuka Salome. Heri ungeumwa ukalazwa ukauguzwa shoga yangu. We will miss you.
 
Bongo noma sana..Nilipita kwenye eneo la tukio. Kuna mdada alikandamizwa na lori na bado alikua hai kwa zaidi ya masaa mawili. Bado tuna changamoto kubwa sana ya emergency. Siasa zimetawala utendaji.
Kumbe uliona hili wangewahi kuja na vifaa angetoka mzima yani nchi hii kweli tunashindwa kuwa na vifaa vidogo tu kama hivi huku tukijinasibu kununua pangaboi
 
Back
Top Bottom