TANZIA: Rock City Wing

Ahsante dada mkubwa, tunamshukuru Mungu hata kwa hili. Kesho saa tisa alasiri tutampumzisha mpendwa wetu
pole sana mdogo wangu ram
Mungu akupe faraja kwa msiba uliokupata...
RIP binamu...
Pamoja sana Rock city
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana Ram pamoja na familia yote ya wafiwa. Mwenyezi Mungu awawekee wepesi katika shughuli zote za msiba. Asante kwa taarifa Charming Lady. Pamoja Saana.

Shukrani dada mkubwa...
 
Tunawashukuruni nyote kwa kutufariji JF Rock City Wing...

Leo ndio tunampumzisha dada yetu mida ya alasiri... :rip: :rip: :rip: Dada Martha!
 
Reactions: ram

Aksante kwa taarifa Charminglady. Nipo njiani naja kujiunga nanyi.
 
Pole sana dada ram, mitihani tumeumbiwa bin adamu
 
Last edited by a moderator:
Reactions: ram
RIP binamu. Poleni familia. Mungu awajalie faraja kuu
 
Reactions: ram
Pole kwa kumpoteza mmoja wa wapendwa wako,mwenyezi Mungu akupe faraja wew na familia yote ktk kipind hich kigumu
 
Habari zenu wa JF.....

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu kwa mambo mengi anayotufanyia katika maisha yetu, Kipekee nina mshukuru Mungu hata kwa mavuno aliyoyavuna shambani mwake.

Pili niwashukuru wanaJF wote kwa kuungana nami katika msiba huu ulinipata wa kumpoteza ndugu yangu, mdogo wangu na rafiki yangu mkubwa Mwl Martha. Hakika mmekuwa faraja kubwa kwangu na JF rocky city wing, nawashukuru sana sana, nilichojifunza ni kuwa JF ni zaidi ya mtandao bali ni familia ya watu tusiofahamiana (kwa member wengi) lakini ni watu tunaoishi kwa upendo, umoja na mshikamano, Mungu awabariki wote.

Shukrani zangu nyingi zimwendee, ndugu yangu, rafiki yangu na mdogo wang charminglady, kwanza kwa kuleta taarifa hizi hapa lakini pia kwa kushiriki nami kwa kila hatua katika msiba huu, Mungu akubariki sana CL na ninakushukuru sana sana mamii

Mwisho lakini sio kwa umuhimu, nawashukuru JF rock city wing kwa upendo, umoja na mshikamono mliouonesha kwangu tangu mlipopoata taarifa hizi za msiba, mmekuwa nami bega kwa bega hadi jana tulipohitimisha safari ya mdogo wetu Mwl Martha, Mungu awabariki jamani, sina cha kuwalipa ila Mungu atawalipa

Ahsanteni wote, pamoja sana....!
 
Last edited by a moderator:

Asante kushukuru mamie...... :welcome: :welcome:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…