Tanzia: Professor Wambali hatunae tena duniani

Tanzia: Professor Wambali hatunae tena duniani

Namkumbuka prof. Wambali kama mwalimu wangu wa Law of Tort na nilipata alama A na pia alikuwa supervisor wangu kwenye disertation mwaka wa nne na akanipa alama B+. RIP frof.
 
He was a fair man....He will surely be missed by many!
Kweli alikuwa very fair, hamna mtu aliye supp katika somo lake law of tort, nakumbuka sana ucheshi wake na vituko vyake, alikuwa akija kutupa lecture baada ya 30 toka muda wa kipindi umeanza na hapo tax inamsubiri nje, huku kwenye lecture akituacha hoi kwa mifano ya matusi. RIP
 
Acha kutafuta visingizio, mtu kesha kufa basi, nendeni mkazike Muendelee na Maisha!

Kama hayo uliyoyaandika ni kweli na wewe uliguswa sana na kutotendewa haki kwa Marehemu kwa nini hukuja hapa kuleta huo ulalamishi kabla hajafa?

Pia wewe na huyo unayemlaumu hamna tofauti, basi wote mmechangia kifo chake kwa maana ulijua kwamba hapewi matibabu anayostahili, na ulijua ni nini kinamsumbua, na kutokana na maelezo yako pia ulijua wapi anaweza kutibiwa na hatimaye kuokoa Maisha yake, lakini ukakaa kimya, sasa Amekufa ndio unakuja hapa na kuanza kuleta Umbeya na kutafuta Mchawi!

apa anaejibu ni muajiri (udsm) au mihemko ya mtu tu anaejifanya anakijua sana chuo? kwa usomi uliopo pale ud we ulitaka uletewe malalamiko ndo hatua za makusudi kumpeleka india zichukuliwe? kweli hatuna wasomi, ni mamiwani tu makubwa usoni kumbe kichwani mapwo mpwo pwo!
 
Kweli ni pigo kwa kitivo cha sheria. kweli alikuwa mcheshi na vituko sana lecture anakuja dak 30 za mwisho na anafundisha kwa mifano ya matusi na kuchekesha basi kwenye mtihani unakumbuka vizuri sana. Kesho nitamkumbuka kwa kuangalia copy ya disertation yangu nione sahihi yake!
 
Pumzika kwa amani mwalimu wangu. Nitakukumbuka kwa fairness yako.
 
Prof. Wambari

Mwenyenzi MUNGU akupe pumziko la milele shambani mwake!
 
Professor Nguli wa sheria wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam A.K.Wambali,amefariki dunia muda mfupi uliopita,kwenye hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa.Katika uhai wake,atakumbukwa kama Mwalimu wa sheria aliyetukuka na mpigania haki za binadamu.Mungu amlaze mahali pema peponi.Amen

R.I.P Prof wangu ntakukumbuka daima. Pole Tundu Lissu.
 
Nimfahamuvyo Prof Mukandala, hakuwahi kuwa mtu mwema kwa watu wote kwa kuwa amejawa sana na ubaguzi tukianzia kwa ukabila na kuwaona wa maana wale watu wake wa karibu tu (walio katika cycle yake). Mukandala, is not a goog administrator and manager. Wakati wanateua hawa ma VC busara itumike zaidi kuliko kuangalia CV zisizo za maana. Rest in Peace Prof. Wambali.

Nadhani hili la Administration ya Prof. Mukandala halina budi kufanyiwa kazi na mamlaka husika, maana ni mara kwa mara wanajf wanazungumzia sana "unfair" treatment yake. Anyway,
 
Dah!..... RIP Prof Wambali....poleni sana wafiwa......
 
Kweli alikuwa very fair, hamna mtu aliye supp katika somo lake law of tort, nakumbuka sana ucheshi wake na vituko vyake, alikuwa akija kutupa lecture baada ya 30 toka muda wa kipindi umeanza na hapo tax inamsubiri nje, huku kwenye lecture akituacha hoi kwa mifano ya matusi. RIP

kumbe ulikua unafurahia matusi? Ndio mana 2nazalisha wasomi mabogaz!
 
Professor Nguli wa sheria wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam A.K.Wambali,amefariki dunia muda mfupi uliopita,kwenye hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa.Katika uhai wake,atakumbukwa kama Mwalimu wa sheria aliyetukuka na mpigania haki za binadamu.Mungu amlaze mahali pema peponi.Amen

R.I.P Prof. Wambali, he was my supervisor at the faculty.
 
Really prof was the best,he never wanted to see any of his student fail .He was a man of funny,was kind,and hard worker....he was the best among all at the fa......kweli wema hawadumu ....
 
Back
Top Bottom