TANZIA: Profesa Jahazi amefariki dunia

September 13, 2017

TAAZIA: DR. BUYUNI JAHAZI
Makala imetayarishwa na Mohamed Said

Dr. Jahazi amefariki mchana huu leo tarehe 13 September, 2017.

Kwake tumetoka na Kwake ni marejeo yetu.

Iko siku mwaka wa 1993 na ulikuwa mwezi wa Ramadhani nilikuwa nasafIri na ndege ya Air Tanzania Corporation (ATC) kuelekea Harare kwenye kozi ya Masoko ya Huduma yaani, ‘’Marketing of Services.’’ Wakati ule nilikuwa nikifanya kazi Bandarini Idara ya Masoko.

Ndege ilikuwa ya alfajir na kwa bahati nzuri Dr. Jahazi na yeye alikuwa anasafiri na ndege hiyo hiyo kuelekea Harare kwenye mkutano wa Madaktari. Wakati ule Dr. Jahazi alikuwa akisomesha pale Muhimbili Faculty of Medicine.

Basi nikamkuta Dr. Jahazi pale uwanjani amesimama anasubiri ATC wafungue ‘’desk,’’ lao abiria waanze mchakato wa ku -‘’check in,’’ abiria ili wapatiwe, ‘’boarding pass,’’ waelekee, ‘’departure lounge,’’ na kuingia katika ndege tayari kuwa kuruka.

Dr. Jahazi alikuwa amevaa kanzu nyeupe na amepiga kilemba cha tabligh.

Ukitamtazama picha ya haraka itakayokujia ni kuwa huyo ni sheikh wa tabligh siyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu.

Siku zile ilikuwa hakuna, ‘’security check,’’ kama hizi za siku hizi za kupitisha watu na mizigo katika, ‘’metal detector,’’ ambazo kwa sasa ziko kila mahali kuanzia viwanja vya ndege hadi katika mahoteli makubwa.

Wakati nasalimiana na Dr. Jahazi tukiubiri ATC wafungue, mara akatokea Balozi Ami Mpungwe wakati ule akifanyakazi Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje lakini alikuwa bado hajawa na cheo cha Ubalozi.

Ami akaja pale tulipokuwa tumesimama na akatusalimu.

Dr. Jahazi akamuuliza kama na yeye ni msafiri. Ami akajibu akasema yeye amekuja kuwasindikiza wageni wa serikali na alikuwa kawaingiza VIP Lounge na alikuwa anaondoka ndipo alipotuona akaona aje atusalimu.

Dr. Jahazi akamfahamisha Ami kuwa sisi tulikuwa tunakwenda Harare.

Dr. Jahazi alikuwa mkononi ameshika, ‘’briefcase,’’ na katika ile, ‘’briefcase,’’ alikuwa amefunga kidumu cha lita tano chenye maji.

Ami akawa kashangazwa na kile kidumu cha maji, akamuuliza Dr. Jahazi, ‘’Dr. haya maji ya nini?’’

Dr. Jahazi akajibu akasema, ‘’Haya maji natembea nayo kwa ajili ya kuchukua udhu isije wakati wa sala umeingia na mimi sina maji ya kutawadha.’’

Jibu lili lilimtosheleza Ami hata na mie pia kwani nami nilikuwa najiuliza yale maji yalikuwa ya nini ila tu sikupata fahamu ya kuuliza.

Ndani ya ndege tulikaa pamoja na ilikuwa safari nzuri sana kwangu.

Dr. Jahazi aliniwaidhi kuhusu utukufu wa Allah na Mtume Wake na akaniambia kuwa endapo nitaishika kamba ya Allah nitafanikiwa hapa duniani na akhera.

Siku ile tukiwa angani tukielekea Zimbabwe ndiyo kwa mara yangu ya kwanza nilipolisikia jina la Prince Badru Kakunguru wa Uganda.

Dr. Jahazi alipobaini kuwa mimi sikuwa namjua Prince Badru Kakunguru alianza kunieleza historia ya Uislam Uganda na vipi Prince Badru Kakunguru alivyofanya juhudi katika kuuepeleka Uislam mbele Uganda.

Nilishangaa sana kwani sikujua kuwa Dr. Jahazi juu ya kuwa Bingwa wa Micro Bio-Chemistry Uganga wenyewe alikuwa pia ni mjuzi wa historia.

Niliona safari ni fupi sana katika ya Dar na Harare.

Mimi nilikuwa sijafika Harare lakini yeye Dr. Jahazi alinifahamisha kuwa alikuwa akienda huko mara nyingi kwa shughuli za mikutano na makangamano ya kitaaluma.

Basi nikamuomba Dr. Jahazi anifahamishe hoteli nzuri ya mimi kwenda kukaa.

Ilikuwa kozi ya takriban mwezi mzima na nilitaka nikae mahali pazuri.

Dr. Jahazi alinitazama usoni akaniambia, ‘’Sikiliza mdogo wangu Mohamed, mimi sikai hoteli, mimi nalala msikitini.’’

Ukweli ni kuwa nilishtuka na kushangaa sana.

Juu ya mshtuko wangu sikusema kitu nilinyamaza kimya.

Wakati tunatoka nje ya uwanja wa ndege wa Harare mie nikawa nimemganda Dr. Jahazi niko ubavuni kwake. Mara tu tulipokuwa tushapita, ‘’Customs,’’ kundi la vijana wa kila rangi nikaona wamemvamia Dr. Jahazi wakimpokea mizigo yake na kutokana na mazungumzo yao nikajua hawa ni madaktari wanataaluma wanzake.

Ghafla Dr. Jahazi akawa kageuka si yule aliyekuwa na mimi ndani ya ndege. Hapa alikuwa Dr. Jahazi ‘’Lecturer,’’ yuko darasani anasomesha.

Mara atamjibu huyu hiki mara atamjibu huyu kile kwa Kiingereza kilichonyooka kisawasawa. Hakika wale jamaa ilionyesha walikuwa wanamuusudu Dr. Jahazi na walikuwa wamengoja kwa hamu.

Yalikuyokuwa yanazunguzwa pale mie sikuambulia hata moja.

Baada ya kutulia tukaingia katika gari kuelekea mjini na akanambia kuwa atanipeleka Ambassador Hotel iko katikati ya mji na akamwambia dereva apite barabara fulani ili anionyeshe msikiti nitakaokuja kuswali tarweh.

Nakumbuka kichekesho kimoja.

Dr. Jahazi aliposema neno, ‘’mosque,’’ yule dereva akawa hajui lina maana gani.

Dr. Jahazi alipomfahamisha dereva kuwa ni ‘’msikiti,’’ yule bwana akajibu akasema, ‘’Oh! You mean Muslim church.’’

Dr. Jahazi alikuwa rafiki kipenzi wa kaka yangu Prof. Mgone toka wote wakiwa wanafunzi pale Muhimbili na nilikuwa nafurahishwa na kitu kimoja kila tunapokutana.

Ingawa sasa mimi ni mtu mzima lakini yeye hakuacha kuniangalia mimi kama, ‘’bwana mdogo,’’ wake na katika mazunguzo yetu siku zote hiki kikijitokeza na mimi nilikuwa siachi kutanguliza, ‘’kaka,’’ kila ninapozungumza na yeye.

Miezi michache iliyopita tulikuwa sote tukaachana Msikiti wa Shadhly baada ya kuzungumza njia nzima.

Mwaka wa 2002 Tanzania ilipopitisha Sheria ya Ugaidi, Dr. Jahazi alivamiwa nyumbani kwake na kutiwa nguvuni kwa kushukiwa kuwa ni gaidi. Wapelelezi walipekuea nyumba yake chini juu juu chini kutafuta ushahidi wa ugaidi lakini walichokutananacho katika nyumba na maktaba yake ni mavolumu na mavolumu ya majarida na mabuku na mabuku ya taaluma yake ya udaktari.

Kosa lake Dr. Jahazi ilikuwa ni yake mapenzi yake katika dini yake na kuenzi kivazi chake cha kanzu na kilemba hata anapokuwa darasani Chuo Kikuu Muhimbili akihadhiri.

Allah ampe kaka yangu Dr. Jahazi kauli thabit na amweke mahali pema peponi.

Amin.

Source: Makala hii ya taazia kwa hisani kubwa ya Mdau wa JamiiForums Mohamed Said Source: Mohamed Said: TAAZIA: DR. BUYUNI JAHAZI
 
Prof Jahazi aliweza kuwafundisha na kuwavuta watu ambao hawaamini kwenye imani yake kwa matendo na mwenendo wake tu alikua mpole,mcheshi na mkarimu aliufanya Uislamu kua sio dini ya vitisho na ghadhabu pamoja kua mimi imani yangu ni tofauti ila nilipenda kumsikiliza kila anapotoa nasaha na elimu nakumbuka aliwahi kuletewa kizaaza pale Muhimbili kisa mavazi yake wakidhani ni gaidi,siku za karibuni nilipata kusikia maradhi ya moyo na sukari yalimuandama sana.
Inshaallah nikutakie heri uendako na Mungu akupe kauli thabiti na upunguziwe adhabu za kaburi hakika Prof Jahazi umeitika wito ambao na sisi sio muda tutaitika pia.
 
Inna Lillahi wa inna ilayhi raajiuun,..

Prof. Jahazi amefariki Dunia muda huu.

Allah amsamehe, atie Nuru ktk kaburi lake na ampe kauli thaabit ndugu yetu [Allahummagh'firllahu].

Maziko ya Prof. Jahazi leo. Ata Swaliwa Masjid Shadhily na kuzikwa Kisutu baada ya Asir

Professa jahazi alikuwa mhadhiri katika chuo kikuu cha afya Muhimbili(Muhas) upande wa Microbiology.
mwenyezi mungu amrehemu,ila nijuavyo mimi Dr Jahazi miaka ile alipokuwa anafundisha MUCHS (kwa sasa MUHAS) alikuwa idara ya Biochemistry iliyokuwa ikiongozwa na Dr Nyambo.
Huyu mtu namkumbuka alikuwa ni msomi mwenye elimu pana,mcha mungu wa kweli, asiye na majivuno,mpenda watu na siku zote alijichanganya na watu tena hasa wa profile za chini,ukimuona kwa mara ya kwanza ni ngumu kumjua kama ni mtu wa hadhi ya juu, na muda wote alipenda kuvaa vazi la kanzu, kilemba na open shoes.
Ni masikitiko makubwa kupoteza msomi wa aina yake tena anayejua nini maana ya utu pamoja na kukwea ngazi ya mafanikio kimaisha,tofauti na wasomi wetu wa kizazi hiki ambapo mtu hata akimaliza elimu ya msingi tu tayari anaanza kuweka kifua mbele na mabega juu.
SISI SOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE NDIO MAREJEO YETU.
 
September 13, 2017

TAAZIA: DR. BUYUNI JAHAZI
Makala imetayarishwa na Mohamed Said

Dr. Jahazi amefariki mchana huu leo tarehe 13 September, 2017.

Kwake tumetoka na Kwake ni marejeo yetu.

Iko siku mwaka wa 1993 na ulikuwa mwezi wa Ramadhani nilikuwa nasafIri na ndege ya Air Tanzania Corporation (ATC) kuelekea Harare kwenye kozi ya Masoko ya Huduma yaani, ‘’Marketing of Services.’’ Wakati ule nilikuwa nikifanya kazi Bandarini Idara ya Masoko.

Ndege ilikuwa ya alfajir na kwa bahati nzuri Dr. Jahazi na yeye alikuwa anasafiri na ndege hiyo hiyo kuelekea Harare kwenye mkutano wa Madaktari. Wakati ule Dr. Jahazi alikuwa akisomesha pale Muhimbili Faculty of Medicine.

Basi nikamkuta Dr. Jahazi pale uwanjani amesimama anasubiri ATC wafungue ‘’desk,’’ lao abiria waanze mchakato wa ku -‘’check in,’’ abiria ili wapatiwe, ‘’boarding pass,’’ waelekee, ‘’departure lounge,’’ na kuingia katika ndege tayari kuwa kuruka.

Dr. Jahazi alikuwa amevaa kanzu nyeupe na amepiga kilemba cha tabligh.

Ukitamtazama picha ya haraka itakayokujia ni kuwa huyo ni sheikh wa tabligh siyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu.

Siku zile ilikuwa hakuna, ‘’security check,’’ kama hizi za siku hizi za kupitisha watu na mizigo katika, ‘’metal detector,’’ ambazo kwa sasa ziko kila mahali kuanzia viwanja vya ndege hadi katika mahoteli makubwa.

Wakati nasalimiana na Dr. Jahazi tukiubiri ATC wafungue, mara akatokea Balozi Ami Mpungwe wakati ule akifanyakazi Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje lakini alikuwa bado hajawa na cheo cha Ubalozi.

Ami akaja pale tulipokuwa tumesimama na akatusalimu.

Dr. Jahazi akamuuliza kama na yeye ni msafiri. Ami akajibu akasema yeye amekuja kuwasindikiza wageni wa serikali na alikuwa kawaingiza VIP Lounge na alikuwa anaondoka ndipo alipotuona akaona aje atusalimu.

Dr. Jahazi akamfahamisha Ami kuwa sisi tulikuwa tunakwenda Harare.

Dr. Jahazi alikuwa mkononi ameshika, ‘’briefcase,’’ na katika ile, ‘’briefcase,’’ alikuwa amefunga kidumu cha lita tano chenye maji.

Ami akawa kashangazwa na kile kidumu cha maji, akamuuliza Dr. Jahazi, ‘’Dr. haya maji ya nini?’’

Dr. Jahazi akajibu akasema, ‘’Haya maji natembea nayo kwa ajili ya kuchukua udhu isije wakati wa sala umeingia na mimi sina maji ya kutawadha.’’

Jibu lili lilimtosheleza Ami hata na mie pia kwani nami nilikuwa najiuliza yale maji yalikuwa ya nini ila tu sikupata fahamu ya kuuliza.

Ndani ya ndege tulikaa pamoja na ilikuwa safari nzuri sana kwangu.

Dr. Jahazi aliniwaidhi kuhusu utukufu wa Allah na Mtume Wake na akaniambia kuwa endapo nitaishika kamba ya Allah nitafanikiwa hapa duniani na akhera.

Siku ile tukiwa angani tukielekea Zimbabwe ndiyo kwa mara yangu ya kwanza nilipolisikia jina la Prince Badru Kakunguru wa Uganda.

Dr. Jahazi alipobaini kuwa mimi sikuwa namjua Prince Badru Kakunguru alianza kunieleza historia ya Uislam Uganda na vipi Prince Badru Kakunguru alivyofanya juhudi katika kuuepeleka Uislam mbele Uganda.

Nilishangaa sana kwani sikujua kuwa Dr. Jahazi juu ya kuwa Bingwa wa Micro Bio-Chemistry Uganga wenyewe alikuwa pia ni mjuzi wa historia.

Niliona safari ni fupi sana katika ya Dar na Harare.

Mimi nilikuwa sijafika Harare lakini yeye Dr. Jahazi alinifahamisha kuwa alikuwa akienda huko mara nyingi kwa shughuli za mikutano na makangamano ya kitaaluma.

Basi nikamuomba Dr. Jahazi anifahamishe hoteli nzuri ya mimi kwenda kukaa.

Ilikuwa kozi ya takriban mwezi mzima na nilitaka nikae mahali pazuri.

Dr. Jahazi alinitazama usoni akaniambia, ‘’Sikiliza mdogo wangu Mohamed, mimi sikai hoteli, mimi nalala msikitini.’’

Ukweli ni kuwa nilishtuka na kushangaa sana.

Juu ya mshtuko wangu sikusema kitu nilinyamaza kimya.

Wakati tunatoka nje ya uwanja wa ndege wa Harare mie nikawa nimemganda Dr. Jahazi niko ubavuni kwake. Mara tu tulipokuwa tushapita, ‘’Customs,’’ kundi la vijana wa kila rangi nikaona wamemvamia Dr. Jahazi wakimpokea mizigo yake na kutokana na mazungumzo yao nikajua hawa ni madaktari wanataaluma wanzake.

Ghafla Dr. Jahazi akawa kageuka si yule aliyekuwa na mimi ndani ya ndege. Hapa alikuwa Dr. Jahazi ‘’Lecturer,’’ yuko darasani anasomesha.

Mara atamjibu huyu hiki mara atamjibu huyu kile kwa Kiingereza kilichonyooka kisawasawa. Hakika wale jamaa ilionyesha walikuwa wanamuusudu Dr. Jahazi na walikuwa wamengoja kwa hamu.

Yalikuyokuwa yanazunguzwa pale mie sikuambulia hata moja.

Baada ya kutulia tukaingia katika gari kuelekea mjini na akanambia kuwa atanipeleka Ambassador Hotel iko katikati ya mji na akamwambia dereva apite barabara fulani ili anionyeshe msikiti nitakaokuja kuswali tarweh.

Nakumbuka kichekesho kimoja.

Dr. Jahazi aliposema neno, ‘’mosque,’’ yule dereva akawa hajui lina maana gani.

Dr. Jahazi alipomfahamisha dereva kuwa ni ‘’msikiti,’’ yule bwana akajibu akasema, ‘’Oh! You mean Muslim church.’’

Dr. Jahazi alikuwa rafiki kipenzi wa kaka yangu Prof. Mgone toka wote wakiwa wanafunzi pale Muhimbili na nilikuwa nafurahishwa na kitu kimoja kila tunapokutana.

Ingawa sasa mimi ni mtu mzima lakini yeye hakuacha kuniangalia mimi kama, ‘’bwana mdogo,’’ wake na katika mazunguzo yetu siku zote hiki kikijitokeza na mimi nilikuwa siachi kutanguliza, ‘’kaka,’’ kila ninapozungumza na yeye.

Miezi michache iliyopita tulikuwa sote tukaachana Msikiti wa Shadhly baada ya kuzungumza njia nzima.

Mwaka wa 2002 Tanzania ilipopitisha Sheria ya Ugaidi, Dr. Jahazi alivamiwa nyumbani kwake na kutiwa nguvuni kwa kushukiwa kuwa ni gaidi. Wapelelezi walipekuea nyumba yake chini juu juu chini kutafuta ushahidi wa ugaidi lakini walichokutananacho katika nyumba na maktaba yake ni mavolumu na mavolumu ya majarida na mabuku na mabuku ya taaluma yake ya udaktari.

Kosa lake Dr. Jahazi ilikuwa ni yake mapenzi yake katika dini yake na kuenzi kivazi chake cha kanzu na kilemba hata anapokuwa darasani Chuo Kikuu Muhimbili akihadhiri.

Allah ampe kaka yangu Dr. Jahazi kauli thabit na amweke mahali pema peponi.

Amin.

Source: Makala hii ya taazia kwa hisani kubwa ya Mdau wa JamiiForums Mohamed Said Source: Mohamed Said: TAAZIA: DR. BUYUNI JAHAZI
Hii ni makala maridhawa kuhusu Dr Jahazi,mwandishi amekuwa mkweli na sijaona sehemu "iliyotiwa chumvi" katika wasifu wake.
Mungu amrehemu Dr Jahazi.
 
Sijapata nafasi ya kukutana naye, ila nilijuana na mwanawe Bori. Kwa kumuangalia mwana mara nyingine waweza kujua familia aliyotoka na malezi aliyopata.

Kwa hulka ya Bori Jahazi alivyokuwa, sishangai hata kidogo kusikia sifa hizi kwa mzazi wake.

Apumzike kwa amani Profesa Jahazi.
 
Back
Top Bottom