Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Imamu mkuu wa msikiti maarufu nchini Tanzania na Afrika mashariki Masjid Mtoro uliopo jijini Dar es salaam eneo la Kariakoo, Sheikh Zubeir bin Yahya Mussa, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Machi 5, 2019.
Sheikh Zubeir ni miongoni mwa masheikh maarufu jijini Dar es salaam alifahamika sana kutokana kuwa ni Imamu katika msikiti huo, ambao ni katika misikiti mikubwa na maarufu zaidi nchini Tanzania na Afrika mashariki.
Pamoja na Uimamu wake, Sheikh Zubeir aliwavutia watu wengi sana kutokana na darasa zake alizokuwa akiziendesha (akizisomesha), kwa ufundi mkubwa katika msikiti huo wa Mtoro na maeneo mengine.
Sheikh Zubeir alikuwa ni katika masheikh waliojiweka karibu sana na jamii na kuwa na mahusiano mazuri na masheikh wenzake kutoka taasisi mbalimbali.
Sheikh Zubeir alipata elimu yake ya juu katika chuo kikuu cha Madina, (Ummul- Quraa) akiwa pamoja na Sheikh Juma Omar Poli, Sheikh Muharram Juma Doga, Sheikh Abdallah Ahmad Bawazir na wengineo.
Taarifa kuhusu maandalizi na taratibu zote za mazishi ni kwamba; kisomo cha kumuombea kitaanza saa 4: 00 leo asubuhi katika msikiti wa Mtoro na ataswaliwa hapo hapo Masjid Mtoro baada swala ya alasiri kisha kwenda kuzikwa katika makaburi ya Kisutu maeneo ya Upanga jijini Dar es salaam.
•••Mungu amlaze Sheikh Zubeir mahala pema wanapolazwa wema..amein
••••Inna lillah wainna illayh rajiun