TANZIA: Ali Mufuruki afariki dunia Afrika Kusini. Aagwa katika Ukumbi wa JNICC. Kuzikwa Makaburi ya Kisutu, Dar

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,499
86,037
Kuna taarifa za msiba wa Alli Mafuruki. Hakuna taarifa zaidi zilizopatikana hadi sasa. Pumzika kwa Amani

====

Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Infotech Investment Group, Ali Mufuruki amefariki dunia leo

Enzi za uhai wake Mufuruki aliwahi kuwa Mkurugenzi Huru, Mwenyekiti wa Bodi na Kamati ya Uteuzi ya Kampuni ya Vodacom Tanzania kabla ya kujiuzulu

Amefariki alfajiri ya leo akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Morningside jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Aliugua ghafla jana, akalazwa Aga Khan Hosp (jijini Dar) kabla hajapelekwa kwa haraka Afrika Kusini alikofia.

Marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa homa ya mapafu.

Mwili Kuagwa Desemba 10 JNICC

Kuanzia Saa 1:30 kesho asubuhi hadi saa 6:00 adhuhuri, wananchi watauaga mwili wa bilionea Ali Mufuruki aliyefariki Jumamosi iliyopita nchini Afrika Kusini.

Taarifa iliyotolewa na kamati ya msiba wa bilionea huyo ambaye mwaka 2012 utajiri wake ulikadiriwa kuwa Dola 110 milioni za Marekani sawa na Sh176 bilioni kwa wakati huo Dola moja ikiwa sawa na Sh1,600.

Ingawa mwakilishi wa Serikali bado hajajulikana, salamu za buriani zinatarajiwa kuongozwa na Balozi Ali Mpungwe atakayesoma wasifu wa marehemu huku Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakurugenzi wa kampuni nchini (CEO Roundtable), Sanjay Rughan akiiwakilisha sekta binafsi.

Dua ya kumuombea marehemu itaongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al Had Mussa Salum, Sheikh huyo pia ataongoza Mawaidha huku Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai atatoa salamu kwa niaba ya vyombo vya habari.

Waombolezaji watakaojumuisha wageni, viongozi na wanafamilia, wataruhusiwa kuingia katika ukumbi wa JNICC kuanzia Saa 1:30 asubuhi kabla mwili haujaondolewa ukumbini hapo kati ya saa 5:50 asubuhi na saa 6:00 kamili adhuhuri.

Mwili utawasili ukumbini hapo saa 3:00 asubuhi kutoka Msikiti wa Mmaamur uliopo Upanga ili kuruhusu ratiba iendelee.

IMG_20191208_110759.jpg


RAIS MAGUFULI AGUSWA NA MSIBA

Rais Magufuli ametoa salamu za rambi rambi kutokana na kifo cha ndugu Ali Mfuruki. Kupitia akaunti yake ya twitter Rais Magufuli ameonesha kuhuzunishwa na msiba huo.

"Nimehuzunishwa na taarifa za kifo cha rafiki yangu Ali Mufuruki (Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni - CEOrt) Nitamkumbuka kwa uzalendo na mchango wake katika kukuza sekta ya biashara na ushauri kwa Serikali.Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un"- Rais Magufuli

2234770_20191208_142020.jpeg


---
ABOUT Ali Mufuruki:
Birth Date: 15 Novemba, 1958 Kagera Tanzania

Education
  • 1971 Katerero Primary School
  • 1976 Lake Secondary School, Mwanza
  • 1978 Old Moshi High School, Moshi
  • 1978-1980 Makutupora Camp, Dodoma
  • Reutlingen Technical University, German
His Proffesional Life:
  • 1985- 1987 Worked for Daimler Benz AG of German (Sindelfingen Plant) as Mechanical Engineering Design Department
  • 1987 -1989 National Engenering GO, LTD Dar es Salaam
Bussiness Experience
  • Set up Infotech Compters Limited 1989
  • Setup M&M Communication in 1994
  • Set up W-Stores (WOOLWORTHS) in 1999- Currently Operating ratail outlets in Dar es Salaam, Kampala
  • Established real estate Company Infotech Place in 2006 with properties in Dar es Salaam
  • invested in Media/ telecom company Wananchi Group of Kenya in 2008 and served as Chairman of the Bodyfor five years until 2015
  • Joined Private Equity Company ECAP LTD of Kenya in 2008 as founding partiners
  • Invested in Chai Bora in 2012
  • Invested in internrt sevice provider Blue Town ApS of Copenhagen, Dermark in 2004.
Board Experience
During different times over the last 25 years, Ali Mafuruki has served in various capabilities in Boards of Directors of Public, Private and not for profit Companies. Some of the body he has served on over the period iclude:
  • Founder, ChairMan and CEO Infotech Investiment Group
  • Chairman of Vodacom Tanzania PLC
  • Chairman of Msingi East Africa, Nairobi Kenya
  • Chairman of TradeMark East Africa, Nairobi, Kenya
  • Chairman of Chai Bora limited, Tanzania
  • Chairman, AMSCO, The Natherland
  • council Member and Chairman of Grants Commitee, Muhimbili University of Health and allied Sciences (MUHAS)
  • Chairman, Tanzania Public Safety Trust Fund
  • Chairman, Legacy Capital Partners LTD
  • Partner, East Africa Capital Partners, Kenya
  • Trustee, Mandela Institute of Development Studies (minds), South Africa
  • Trustee, ATMS foundations, The Netharlands
  • Member of Tanzania National Business Council (TNBC)
  • Member ot the International Monetary Fund (IMF) Advisory Group on Sub Sahara Africa (AGSA)
  • Founder and Chairman, The CEO's Roundtable of Tanzania
  • Member of the Board of Directors, Bank of Tanzania
  • Member of the Body of Directors Technoserve, inc Washngton DC
  • Member of the Body of Directors , National Media Group of Kenya
  • Chairman Body of Directors, Mwananchi Communication Limited
  • Chairman Body of Directors of Air Tanzania Co Limited
Other Notable Appointments and Achievements
  • Named Henry Crown Fellow of the Aspen Institute in USA IN 2001
  • Co- Founded Africa Leadership Initiative (ALI) Fellowship in 2002 now witj more than 500 fellows in West Africa, South Africa and East Africa
  • Appointed Co- Chairman of the UK parliamentary Commision of Inquiry into the Africa Free Trade Initiative in March 2016
  • Named Bellagio Policy Resident Fellow by the Rockfeller founding in 2017
=======
Zaidi kuhusu Mufuruki soma hapa chini:
Alipoongea kuhusu utajiri wake na kueleza alikotokea: African Millionaires: Ali Mufuruki

Kama Mkurugenzi Mkuu wa Infotech: Ali Mufuruki: Chairman and CEO Infotech Investment Group

Fikra zake juu ya Siasa na Uongozi (hasa wa awamu ya Tano):

Mufuruki aipa somo Serikali kuhusu Tanzania ya viwanda na

Ali Mufuruki: Magufuli’s unwavering war against graft and the impact on the economy na

Ali Mufuruki on electoral process and union eventuality: Let Tanzanians solve their own problems na

Ali Mufuruki on ITV: Kilimo kwanza kiliishia wapi? Viwanda vya Saruji kupata hasara si ishara nzuri
 
Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Infotech Investment Group, Ali Mufuruki amefariki dunia leo

Enzi za uhai wake Mufuruki aliwahi kuwa Mkurugenzi Huru, Mwenyekiti wa Bodi na Kamati ya Uteuzi ya Kampuni ya Vodacom Tanzania kabla ya kujiuzulu

Taarifa zaidi kuhusu kifo chake zitaendelea kukujia...
 
Ali Mufuruki amefariki dunia leo asubuhi huko Afrika ya Kusini.
 

Attachments

  • Screenshot_20191208-104514_Twitter.jpg
    Screenshot_20191208-104514_Twitter.jpg
    88.3 KB · Views: 14
Back
Top Bottom