Pole sana mkuu, hii ilishawahi kutokea njia ya kwenda Mtwara wakati hakuna Daraja, Ndugu yetu kama alivyofanya huyo marehemu alijotosa kwa kujigamba kuwa yeye anaweza kuogelea, lakini alipoteza maisha hapohapo. Kweli kama huna imani waweza sema kuwa alilogwa lakini mara nyingi huwa ni msongo wa mawazo.
Pole sana mkuu pamoja na wote walioguswa na msiba huu. Jipe moyo mkuu, tunawaombea kwa Mungu Awape faraja yake katika kipindi hiki kigumu.
Kazi ya Mungu haina makosa.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe!