Tanzia: Mzee Obed Masawe ''Masobe" hatunaye tena

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,372
Reaction score
37,909
Wanajamvi,

Mzee Masawe Obed "MASOBE supermarket" jengo la CCM Mkoa wa Arusha amefariki jana majira ya saa 12 jioni BOT Club katika mazingira ya kutatanisha.Mzee Masobe alifika BOT Club kwaajili ya kupata supu ya jioni na bia mbili tatu katika hali ya kushangaza na kustusha mzee alianguka ghafla na kufariki muda mchache baadae.

RIP Mzee Masobe.

WATU wawili wamefariki dunia, akiwemo mfanyabiashara mmoja maarufu jijini Arusha, aliyefia kwenya Klabu ya wafanyakazi wa benki Kuu ,BOT, tawi la Arusha, na mwingine ambae hajafahamika, aliokotwa akiwa amesokomezwa mtaroni.
LiberatusSabas_1.jpg

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amemtaja mfanya biashara huyo kuwa ni Obed Masawe, (50) ambae anamiliki duka la kuuza vinywaji vikali ,maarufu Masobe Treders, lililopo jengo la Chama cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Arusha.

Amesema mfanyabiashara huyo ambae ni mkazi wa Njiro jijini Arusha,alifikwa na mauti akiwa kwenye klabu ya wafanyakazi wa Benki kuu ya Tanzania, BOT,alipokuwa akiendelea kunywa bia.

Sabasi amesema tukio hilo limetokea Machi 23 mwaka huu, majira ya saa 1.30 usiku,ghafla alijisikia vibaya, na taarifa za awali zinaonyesha kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa presha.

Katika tukio lingine Kamanda, Sabas, amesema mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 25, alikutwa amefariki dunia na mwili wake kusokomezwa kwenye mtaro wa maji ya mvua jana, katika makutano ya bara bara ya Makongoro na Azimio, jirani na jengo la CCM Mkoa.

Amesema mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa hospital ya mkoa ya Mount Meru, ukisubiri ndugu kujitokeza kumtambua.

Ameongeza kuwa marehemu huyo ambae hajafahamika, mwili wake uligundulika baada ya kutoa harufu.

Uchunguzi unaendelea kufahamu vyanzo vya vifo hivyo.

Chanzo:IPP Media
 
Mkuu Mzee Masobe ni mfanyabiashara maarufu sana hapa Jijini Arusha enzi za ujana wake alikuwa mbabe wa vitongoji vya mji wa Kilimanjaro baadae akaja kutia nanga Arusha akaanzisha biashara za malori na supermarket.Huyu huwezi kumweka katika kundi la mabilionea wa Arusha.

ndo nani yani?
 
Nimesikia jana saa 2 nkastuka inawezekana alipata heartattack r.i.p masobe
 
Mkuu Mzee Masobe ni mfanyabiashara maarufu sana hapa Jijini Arusha enzi za ujana wake alikuwa mbabe wa vitongoji vya mji wa Kilimanjaro baadae akaja kutia nanga Arusha akaanzisha biashara za malori na supermarket.Huyu huwezi kumweka katika kundi la mabilionea wa Arusha.

Mbali na supermarket na malori pia ni mmiliki wa mabus ya engembensabo yanayosafiri mwanza dar es salam.
 
Mkuu Mzee Masobe ni mfanyabiashara maarufu sana hapa Jijini Arusha enzi za ujana wake alikuwa mbabe wa vitongoji vya mji wa Kilimanjaro baadae akaja kutia nanga Arusha akaanzisha biashara za malori na supermarket.Huyu huwezi kumweka katika kundi la mabilionea wa Arusha.

Kwa hiyo huyu si billionare?Mbona anaonekana ana mali nyingi?
 
Wanajamvi,

Mzee Masawe Obed "MASOBE supermarket" jengo la CCM Mkoa wa Arusha amefariki jana majira ya saa 12 jioni BOT Club katika mazingira ya kutatanisha.Mzee Masobe alifika BOT Club kwaajili ya kupata supu ya jioni na bia mbili tatu katika hali ya kushangaza na kustusha mzee alianguka ghafla na kufariki muda mchache baadae.

RIP Mzee Masobe.

Pengine amewekewa Sumu?Alikuwa na ugomvi na mtu kama mabilionaire wengine wa Arusha?
 
Sijui kama alikuwa na ugomvi ila kuna taarifa zinasema kabla mauti haijamkuta alikuwa akiongea na simu katika hali ya majibizano makali pengine HBP inaweza kuwa sababu.

Pengine amewekewa Sumu?Alikuwa na ugomvi na mtu kama mabilionaire wengine wa Arusha?
 
Mkuu Mzee Masobe ni mfanyabiashara maarufu sana hapa Jijini Arusha enzi za ujana wake alikuwa mbabe wa vitongoji vya mji wa Kilimanjaro baadae akaja kutia nanga Arusha akaanzisha biashara za malori na supermarket.Huyu huwezi kumweka katika kundi la mabilionea wa Arusha.
Naona umejihami mapema.
Anyway maadamu alikua anakunywa pombe na kafa nazo,najua kwasasa atakua anachezea kichapo cha ukaidi!!!
 
Kajipeleka mwenyewe sehemu anayostahili

rip mzee ila mlevi ni dhambi kubwa mno

Ila kifo bana wengine wanafia kanisani , misikitini, wengine kwenye pombe, wengine ajali , wengine wanafia gesti wakivunja amri ya sita ila kuna vifo vingine japo mimi sio mtoa hukumu ndugu au mpendwa wako akifa huwa unalia kwa machu gu mosi kwa kumkosa mpendwa wako , pili mazingira ya kifo yalipomkuta mwee kesheni mkiomba kwa vile hamjui siku wala saa mwana wa adamu atakapo kuja kulinyakuwa kanisa lake.
 
Back
Top Bottom