TANZIA: Mwanasiasa mkongwe na Mwanzilishi wa CUF, James Mapalala afariki dunia

Technology

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
769
284
Mwanasiasa mkongwe Mzee James Mapalala amefariki dunia leo katika hospitali ya Kairuki. Mungu amuweke mahali pema. Mzee Mapalala alizaliwa Februari Mosi, 1936.

Mtoto wa Mzee Mapalala, Bernard James amesema baba yake amefariki dunia leo saa 4:30 asubuhi hospitali ya Kairuki alikokuwa tangu wiki mbili zilizopita baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kupumua.

Msiba uko nyumbani kwao Kinondoni.



james_mapalala.jpg

Pia soma










====

Dar es Salaam. Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, James Mapalala amefariki dunia katika hospitali ya Kairuki alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Oktoba 23, 2019 mtoto wa mwanasiasa huyo, Bernard James amesema baba yake amefariki dunia leo saa 4:30 asubuhi.

“Alikuwa hospitali tangu wiki mbili zilizopita baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kupumua,” amesema James.

Amesema familia imekusanyika nyumbani kwao Kinondoni kupanga ratiba ya mazishi.

Mapalala aliyezaliwa Februari Mosi, 1936 ameacha mke na watoto kadhaa.

Alikuwa miongoni mwa wanasiasa wa kwanza waliojitosa kudai mfumo wa vyama vingi urejeshwe nchini Tanzania.

Kufuatia madai hayo, Mapalala alifungwa miaka miwili mkoani Lindi kuanzia mwaka 1986 hadi 1989 na baada ya kutoka aliwekwa kizuizini kwa kipindi cha mwaka mmoja katika kisiwa cha Mafia baada ya kuanzishwa chama cha siasa wakati sheria ilikuwa hairuhusu.

Alianzisha Chama cha Wananchi (CCW) mwaka 1991 na baadaye kiliungana na chama cha Zanzibar – Kamahuru na mwaka 1993 kuzaliwa Chama cha Wananchi (CUF).
 
Mwanasiasa mkongwe mzee James Mapalala amefariki dunia leo katika hospitali ya Kairuki. Mungu amuweke mahali pema. ameen

Pia soma



apunzike kwa amani
 
Siku historia ya nchi ikiandikwa kwa uhalisia wake basi jina la James Mapalala halitakosekana!
Nyakati zake watu wengi walijua kuwa mambo hayakuwa sawa lakini walikaa kimya ila yeye alisimama na kusema "haya mawazo yenu sio...". Of course naye alikumbana na 'uhalisia' wa watz kwa kusalitiwa ila mpaka mauti nadhani bado anaamini alichokiamini tangu awali (mwenye kujua kama aliunga mkono juhudi anikosoe tafadhali).
R.I.P
 
VIC tushushie nondo kidogo,katika hili ili nasi watoto tumjue huyu Mzee!
Alikuwa mwanzilishi wa CUF,pia ni mwenyekiti wa kwanza wa CUF Tanzania bara.Sema wakamletea figisu kuwa ni msaliti na anashirikiana na CCM.Maalim Seif ndo alianza figisu kusema kuwa wafadhili hawataki kutoa misaada,wafadhili hapa nasemea Waarabu,kisa eti James ambae ni Mkristo ni Kafiri.Yaani chuki zilianzishwa na viongozi wa Zanzbar ambao ni maalim Seif na genge lake.Walifikishana kwa msajili wa vyama kipindi hicho akiwa George Liundi.Mwaka 1994 Ndo alitolewa uenyekiti;Alishinda mwaka 1993 hivyo hata hakukaa sana.
Ndo ukawa mwisho wa James Mapalala kuwa Mwenyekiti CUF Bara.
 
Back
Top Bottom