TANZIA
Mwanamuziki nguli wa dansi nchini, Kassim Mapili amefariki dunia.
Mwanamuziki huyo aliyetamba na bendi za Shikamoo Jazz na Polisi Jazz, amefia nyumbani kwake maeneo ya TIOT Tabata.
Mapili alihudhuria mazishi ya mwandishi Fred Mosha.
Marehemu alifariki ndani kwake akiwa amelala na hakuna aliyejua mpaka jioni hii majirani walipoingia kutokana na kutoonekana kwake kwa siku tatu. Wakachungulia ndani na kuuona mwili.
Polisi wakataarifiwa na kufika na kuvunja mlango na kuutoa mwili wa marehemu!
Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un!
Soma pia: Buriani Sajini Kassim Said Mapili
Mwanamuziki mkongwe wa muziki dansi Kassim Mapili akicharaza nyuzi za Gitaa lake chini ya Kundi zima la Mjomba Band.
MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki dansi Kassim Mapili amefariki dunia akiwa chumbani kwake, Tabata jijini Dar es Salaam. Katibu mkuu wa Chama cha Muziki wa Dansi (CHAMUDATA) Hassan Msumari, amesema kuwa kifo cha Mapili kimegunduliwa usiku huu baada ya mlango wa chumba chake kuvunjwa.
Mlango huo ulivunjwa baada ya Kassim Mapili kutoonekana tangu alipokwenda kutazama mpira wa Arsenal na Barcelona Jumanne usiku.
Kwa mujibu wa Msumari, mara mlango ulipovunjwa Kassim Mapili alionekana akiwa ameshafariki akiwa amejifunga taulo, ishara inayoonyesha kuwa aidha alikuwa anakwenda kukoga au ametoka kukoga.
Jumatatu jioni Kassim Mapili alishiriki vizuri mazishi ya mwanahabari Fred Mosha makaburi ya Kinondoni ambapo alipewa wasaa wa kuongea machache na kama vile hiyo haitoshi, Mapili aliimba makaburini hapo kuomboleza kifo cha Fred Mosha.