TANZIA: Mufti Issa Shaaban Bin Simba afariki Dunia

Poleni sana Ndugu zetu Waislam. Kwa kweli Mufti alikuwa kipenzi cha Watanzania wote wa dini zote. Mufti alikuwa Mpole, Mpenda watu, Mpenda haki na kwa kweli ameacha pengo kubwa. RIP Mufti wetu wa Tanzania.
 
Sio kiongozi mkuu wa waislam ni kiongozi mkuu wa bakwata

Kisheria anatambulika kama mkuu wa waislam wote Tanzania, uwe unamkubali au humkubali yeye ndie kiongozi mkuu wa waislam wote Tanzania.

Hakuna mwingine anaetambulika kisheria kama kiongozi wa waislam.
 
Nimemsikia kupitia Radio DW Sheikh mkuu wa Dar akisema mazishi ya Mufti yatafanyima Shinyanga siku ya Alhamisi. HILI limenistua mno na naomba wasomi wa kiislamu waje watusaidie kuwa hili ni katika itikadi ya kiislamu au la. Kiongozi wa dini kufariki asubuhi ya leo na kuzikwa Alhamisi tena Shinyanga.

Kipi kimezuia asizikwe leo au hata kesho asubuhi?
 
Mod naomba uzi huu uachwe uelee wenyewe kwani kuna mafunzo makubwa ndani yake.
Nimemsikia kupitia Radio DW Sheikh mkuu wa Dar akisema mazishi ya Mufti yatafanyima Shinyanga siku ya alhamisi.HILI limenistua mno na naomba wasomi wa kiislamu waje watusaidie kuwa hili ni katika itikadi ya kiislamu au la.Kiongozi wa dini kufariki asubuhi ya leo na kuzikwa alhamisi tena Shinyanga.
Kipi kimezuia asizikwe leo au hata kesho asubuhi?

wanasubiriwa nduguze, itifakhi itimilike......
 
Kisheria anatambulika kama mkuu wa waislam wote Tanzania, uwe unamkubali au humkubali yeye ndie kiongozi mkuu wa waislam wote Tanzania.

Hakuna mwingine anaetambulika kisheria kama kiongozi wa waislam.

Hapana siyo kiongozi wa waislamu wote tanzania.Katiba ya bakwata ipo wazi kabisa,ndio maana ndani ya bakwata hakuna Shia,Answar Suna,Ismailia koja,wale wa pale kitumbini na wengi wengine.
 
Hapana siyo kiongozi wa waislamu wote tanzania.Katiba ya bakwata ipo wazi kabisa,ndio maana ndani ya bakwata hakuna Shia,Answar Suna,Ismailia koja,wale wa pale kitumbini na wengi wengine.

Hiyo haiondoi haki yake ya kua kiongozi mkuu wa waislam, ni sawa na kua mwanachama wa ukawa alafu ukasema kikwete sio rais wako kisa hukumchagua.

Hao wamegoma wenyewe kujiunga n bakwata kama ilivyo kwa vyama vya siasa.

Mufti ndio mkuu wa waislam wote Tanzania kisheria.
 
Back
Top Bottom